Nimpeleke mtoto shule ya milioni 1.5 au hela nimuwekezee UTT au hisa?

Nimpeleke mtoto shule ya milioni 1.5 au hela nimuwekezee UTT au hisa?

Experience and real world.....hivi kusoma kwa shida na karaha ndio experience nzuri ya maisha?? Watanzania kwa nini tunautukuza umasikini kama ni sifa?? Unasema unamuandaa aje kufanya biashara kama zako yet unamuandaa kwenye mazingira magumu serious??
Huyu Jamaa ni kizazi, na ange kuwa karibu yangu ninge mchapa Kofi.

public school nazi heshimu, ila kwakweli hapana kabisa.

ni vile tu Sija oa, ila ninge mchukua dogo angu aje huku niliko.
ada ni 3m na safari hii nime lipa Mimi, na still naona kawaida mno kwa anacho jifunza huko.
 
We jamaa umesoma Urusi ipi hata kauandika tu ni shida?

Mbona unataka kutuchota hapa?
Nimesomea rudn ama pfur formerly known as Patrice Lumumba, mie sijui kuandika I know to solve maths and physics problems.
Am ain't a writer or author. Mtaani wa mikluho maklaya rector wetu wa African section alikuwa bwana slava aliyefundisha must kwa miaka zaidi ya 20 baadaye akaenda kwao.
 
Kulipa hio 1.5 au 3 sio issue, issue nikua unakuta unalipa ada zote hizo lakini mtoto ukimlinganisha na watoto wa Kayumba unakuta wanazidiwa uwezo wa kufikili katika mazingira halisi.
Hii hoja sio kweli.

Watoto walio soma private schools (Sio English medium, elewa tofauti) They are more formal, Kuliko sisi watoto wa kayumba.

Sisi watoto wa kayumba tuna uswahili mno, ambao tumekua trained nao tangu tukiwa shule.
 
Kijana umesoma Tabora ila uelewa wako ni duni mno. Hujui kuwa binadamu tunatofautiana? Kuna wanaosoma special schools na kuna wanaosoma MEMKWA ila wote wanatafuta elimu.
Kumbe unayo akili mno mkuu, yes uelewa ni dunia mno yaani mno kulingana na uelewa wako uliotumika ku asses uelewa wangu. Mana inaonekana wewe ndiye SI unit ya ku asses uelewa wa watu. Keep it up niga
 
Huku chini hawa watoto wanahitaji uangalizi na msingi mzuri sana.Wajue lugha vyema,na uelewa upanuke

Form 1 kayumba sawa
Sikia lugha watt wakiingia from three Ile kayumba na em wanapoteana yaani kayumba na em hawajulikani na nani
 
Kwani shule za government hawezi kusoma?
Shida ya Kuwa na watoto bila Elimu, na Kama una Elimu, basi una Elimika; Mama yake ana akili kuliko wewe, urithi wa mtoto ni Elimu, bora, full stop!
 
Acha Kumsumbua mtoto mwache tu asome kwa raha.
Hivi kwenda shule na fagliò na kudumu unaona kazi ndogo

Mungu akubariki uweke na hisa zake,
Hizo ndo shule sasa. Achana na hizi shule zenu za soft work
 
Kwani shule za government hawezi kusoma?

Anaweza soma kokote ndugu, Hakuna shida, wewe ndo unaamua! Wakati Maisha ya nakuwa magumu msijifurahishe na Sababu zisizo Kuwa na maana, amueni tu kufanya vile uwezo wenu unawataka mfanye!
 
Mke wako kwa point fulani ana idea nzuri. Hii dunia ya sasa kama hujui inglishi vizuri kuna mengi yatakupita. Mpeleke walau primary akajifunze inglishi then olevo mpeleke st kayumba.

NB: hata mimi nilikua na mtazamo kama wako ila nikiangalia inglishi inavyopelekesha watu huku makazini ikabidi niwaze upya msimamo wangu!
Umeshauri vizuri, lakini Bora mtoto umpeleke st Kayumba primary alafu ujikusanye akifika secondary mpeleke shule ya maana hata kama ni mzito sana ataambulia kitu, lakini akienda primary private alafu secondary akaenda kayumba, miezi 3 inamtosha kuwa amesha sahau kila kitu na amefanana na wale waliotoka kayumba msingi
 
usipoteze hela kulipa english medium primary school

HIZO HELA WEKEZA KWENYE HISA,MASHAMBA,VIWANJA PERI URBAN AREAS

📌FOCUS IANZE KWA KUWEKEZA PESA ZA KUJA KUWAPA MITAJI NA URITHI WA MALI KWA HAO AKINA JUNIOR WENU.KUPOTEZA MAMILIONI HUKO EMS KISHA ANAKUJA KUGOMBANIA INTERVIEW ZA TAMISEMI NI "UKICHAA".

MABASI YA NJANO NA TABU ZA TAMISEMI WAPI NA WAPI ACHIENI KAYUMBA HUKO TAMISEMI NDO MAZINGIRA YAO TANGU WADOGO.NYIE WAZUNGU PORI😄😄😄ANZISHENI MIRADI!!!
Hamjui maana ya shule ninyi. Na pia hamjui maana ya mtaji. Kwa kifupi duniani raslimali ya maana kuliko raslimali zote sasa hivi ni elimu (ujuzi).
 
Umeshauri vizuri, lakini Bora mtoto umpeleke st Kayumba primary alafu ujikusanye akifika secondary mpeleke shule ya maana hata kama ni mzito sana ataambulia kitu, lakini akienda primary private alafu secondary akaenda kayumba, miezi 3 inamtosha kuwa amesha sahau kila kitu na amefanana na wale waliotoka kayumba msingi
Fact
 
Usalama wa watoto pia dhidi ya sexual harassment,
Ems ndio hatari Zaidi kuanzia kwenye gari mtoto wako anaweza kubakwa na dereva wakati wa kupelekwa shule alfajiri.

Shuleni wanafunzi wachache ukimya mwingi mtoto anaweza kubakwa chooni au ofisini Kwa teacher big na watu wasijue Kwa sababu hakuna movements nyingi

usafi wa mazingira, idadi ndogo ya wanafunzi ndani ya chumba kimoja cha darasa, n.k..

Children pyschology inasema watoto wana enjoy Zaidi wanapokuwa kwenye kundi la watoto wengi na Sio wachache
 
Wakuu kuna mtoto wangu kaanza shule mwaka huu, chekechea ada yake ni milioni 1.5 ukijumlisha na vikorokoro vingine inaweza fika jumla milioni 1.7

Sio muumini sana wa hizi shule, ila mama yake ndio aling'ang'ania sana tumpeleke huko baada ya kuona rafiki zake nao wamepeleka watoto wao shule za private na wanaongea kiingereza kingi wakiwa na umri mdogo na pia anasema mtoto tukimpeleka shule za serikali atateseka6

Sasa nimefikiria, kumpeleka mtoto hadi amalize shule ya msingi, then sekondari, je hizo pesa za ada badala ya kumlipia shule ya private nikamhamishia serikalini ambako hata hivyo atakua ananuliwa vitabu na materials nyingine , halafu hiyo ada ya private nikawa naiwekeza kwenye mfuko wa UTT au kununua hisa za kampuni inayofanya vizuri tu kila mwaka, au kuiwekeza kwenyw kununua ardhi

Baaadae mtoto akiwa na miaka 20 ama 25 huko atakuwa na mtaji wa kuanzia maisha halafu connection nitampa mimi kwenye biashara zangu

Pia nimefikiria kumpeleka mtoto shule za kawaida kutamjenga awe 'mgumu' awe na kuweza kumudu mazingira halisi ya mtaano baada ya kumaliza masomo, kuliko mazingira ya kupelekwa na kurudishwa na school bus ambayo hayamjengi

Mimi mwenyewe ni msomi mwenye degree, lakini kazi ninyoifanya haihusiani kabisa na elimu yangu, na ilinibidi ni adapt mtaani japo kwa maumivu na hofu yangu ni kuwa mwanangu naweza kumsomesha kwa gharama kubwa halafu elimu isimsaidie kwenye maisha kama mimi, na akawa hana hata skills za kutoboa mtaani, mimi kutokusoma hizo shule za gharama naamimi kumenisaidia kidogo

Dunia inabadilika, wasomi wengi mtaani kazi hakuna na mbaya zaidi kazi nyingi zitaenda kuwa automated miaka ijayo,
Swali hili natamani alijibu Tundu Lisu au pascal Mayala
 
Hii hoja sio kweli.

Watoto walio soma private schools (Sio English medium, elewa tofauti) They are more formal, Kuliko sisi watoto wa kayumba.

Sisi watoto wa kayumba tuna uswahili mno, ambao tumekua trained nao tangu tukiwa shule.
Hiyo kua na uswahili mkuu maana yake ni nini?.
 
Back
Top Bottom