Nimpeleke mtoto shule ya milioni 1.5 au hela nimuwekezee UTT au hisa?

Mkuu Ugumu wa Maisha usifanye mjifiche kwenye kichaka cha kuwa rudisha watoto nyuma.

Pambaneni wamalize msingi EMS
You are talking about yourself wewe ndo kwako maisha ni magumu
 
For Average Person Mwenye Mzunguko wa not more than 2M kwa Mwezi

Panga hivi elimu ya Mwanao

1. Nursery & Primary Government
2. Secondary Private Tena nzuri za kikatoliki(NB Hapa ndo pana shule 50% ya watoto huko kayumba wanachemka)
3. Advance Government
4. Chuo mlipie Ada

Sielewei ni kwann mzazi anapambana kumsomesha mwanae kwa gharama la kwanza mpaka la 7 private, Halafu ashindwe kulipa Ada ya 1.3M kwa mwaka chuo.

Mwishowe unamwachia mwanao na deni la mil30 maskini
 
😹😹😹 ujue kuna vitu waungwana mnachekesha sana.!!

Sikia usitafute visingizio km huwezi kumudu acha wala hakuna wa kukuchapa..!!
Ushawai kutana na mtu anasema kumiliki iphone ni ushamba? Ndo mtoa maada 😂
 
Afu mnakaa na kuanza sema wahindi wezi
 
Mnunulire ardhi kwa wingi wahenga walisema mali utaipata shambani
 
Ndio mazingira magumu hutoa watu wagumu, lakini mazingira laini huzalisha vilaza wengi wasiojitambua.
 
yaani 1.5 ni ghali kwa mtoto ninaye mpenda??, Kama mdogo angu nime lipa 3m

mwanangu nita mfanyia nini, hahaha .
Kulipa hio 1.5 au 3 sio issue, issue nikua unakuta unalipa ada zote hizo lakini mtoto ukimlinganisha na watoto wa Kayumba unakuta wanazidiwa uwezo wa kufikili katika mazingira halisi.
 
Kulipa hio 1.5 au 3 sio issue, issue nikua unakuta unalipa ada zote hizo lakini mtoto ukimlinganisha na watoto wa Kayumba unakuta wanazidiwa uwezo wa kufikili katika mazingira halisi.
yuko vizuri, kingine ninacho fanya ni kumpa udhamini wa mazingira Bora.

hiyo hoja ya kuzidiana Akili, bado maana wote Wana kariri tu.
wachache Kwa umri huo, Wana fikiri hoja
 
Vilaza ni wengi mkuu, hawawezi kukuelewa, mtu anajitambua anajitambua tu haijalishi kasomea mazingira gani. Hata ukiangalia viongozi wengi wa sasa na watu wenye uwezo mzuri wa kufikili wengi wao wamesoma government. Sema wanachokosa wengi wao ni maadili yakutokupenda rushwa na ufisadi.
 

Shida ya Kuwa na watoto bila Elimu, na Kama una Elimu, basi una Elimika; Mama yake ana akili kuliko wewe, urithi wa mtoto ni Elimu, bora, full stop!
 
yuko vizuri, kingine ninacho fanya ni kumpa udhamini wa mazingira Bora.

hiyo hoja ya kuzidiana Akili, bado maana wote Wana kariri tu.
wachache Kwa umri huo, Wana fikiri hoja
Hoja nayoizungumzia ni utambuzi wa mambo tu madogo madogo. Hata namna yakiitambua akili ya mtoto kua huyu yuko vizuri unamuelewa mapema tu.
 
Duh chekechea analipa ada sawa na mwanafunzi wa chuo au zaidi duh , udaktari ada 1.8M engineer ada 1.7M
 
Shida ya Kuwa na watoto bila Elimu, na Kama una Elimu, basi una Elimika; Mama yake ana akili kuliko wewe, urithi wa mtoto ni Elimu, bora, full stop!
Elimu bora unaipima vipi?. Kama unampeleka mtoto elimu ya michezo au kipaji maalumu kamlipie ela yeyote. Lakini kama ni elimu hii ya BODMAS acha kupoteza pesa zako.
 
Kwahiyo ada Kila muhula utakuwa unalipa 375000

Mwache mtoto asome hapo hiyo pesa hata usilipo lipa ada itaenda katika mambo mengine
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…