#COVID19 NIMR: Tunafanyia utafiti dawa 7 za Kitanzania kama zinatibu Covid 19, chanjo za Magharibi bado hazijathibitika kukinga

#COVID19 NIMR: Tunafanyia utafiti dawa 7 za Kitanzania kama zinatibu Covid 19, chanjo za Magharibi bado hazijathibitika kukinga

Mnazidi kuithibitishia Dunia kuwa mnauwezo mdogo wa kufikiri
Hivi mkuu, tokea vifo vifululize hapa inapita wiki kama tatu sasa na, Ni lini tena Chadema wazee wa kuripoti habari za misiba wamefanya hivyo??

Kaa kimya tuionyeshe Dunia namna Bora ya kushughurikia milipuko ya magonjwa
 
Hizi spices nyingi asilia yake ni Asia watu huko wamekufa huku wakiwa na glasi za tangawizi mikononi na sasa wanalilia chanjo sasa nyinyi maprofesa uchwara na makada wa CCM mtatuua mpaka lini.
Inategemea unakunywa wakati gani ,waswahili tuna hili kambale mkunje angali mbichi. usingojee mpaka umekakamaa ndio unatafuta malimao na tangawizi,kama ulikuwa mtu wa kahawa na chai sasa ni chai ya tangawizi kwa limao unaongeza na karafuu za pemba tatu au zaidi ili kuongeza uhalisia badara ya sukari ya mabeberu tumia asali mwitu kwa maana usitumie zile asalai zilizosafishwa na kuchakachuliwa.
 
We professa acha kujiaibisha mbele ya mataifa...njaa zako zifiche !!

Wewe ni msomi usiongee kama darasa la saba!!
 
Wanaoipigania chanjo wangeweza kupata nafasi ya ushawishi kwa jamii lakini ubaya na wao hata chanjo yenyewe hawaijui wala hawana uthibitisho wa ubora wake.

Wacha niendelee kusimama na serikali yangu, huku nikichukua tahadhari na kumwomba Mungu muumba wa kila kitu na mwenye mamlaka juu ya kila kitu.
 
Mkuu kama ndio hivyo ni kwa nini tumekua tukitumia mabilioni kila mwaka kuagiza madawa ya mafua, upumuaji, athma na magonjwa ya mfumo wa hewa badala ya kutumia tangawizi na limao?...
Tulikuwa hatujajitambua hasa watu wa mjini nenda maeneo ya vijijini uone kama utakuta dawa ya kizungu ya mafua.

Sasa kaa na wenyeji waulize wakipata mafua wanatumia dawa gani. Nenda umasaini ndani ndani ukafanye utafiti lakini usiwabeze utatoka kapa.

Miti shamba ndiyo dawa halisi tuliyopewa na Mwenyezi Mungu. Wazungu walikuja na madawa ya kemikali kwa kuwa kwao hawana miti yq asili bali wana miti iliyokuzwa kwa GMOs haina uasilia wa Mwenyezi Mungu.

Wachina na Wahindi wameshaligundua hilo sasa wanakuja Afrika na kuchukua miti yetu ya asili na kwenda kutengeneza dawa na kuziweka kwenye vidonge na kuja kutuuzia tena sisi hapa Afrika. Waafrika tunahitaji kujitambua.

Tunamshukuru Mwenyezi Mungu tumempata Rais Magufuli ambaye anatufundisha kujitambua ili tuwe wabunifu kuliko kuwasubiri Wazungu tu kwa kila kitu.
 
Sisi Watanzania hatutaki kabisa kuziona hizo chanjo zao za majaribio.
Sio majaribio yametekelezwa? Mamilioni walipata chanjo nchini Israeli. Vifo vya Covid vya wazee vimepungua sana (kabla ya chanjo walijaa hospitali). mamilioni wengine wamepata chanjo Ulaya na marekani.

Kila sehemu tunasikia matokeo ya kawaida ya chanjo: Idadi ya maambukizi zinashuka, watu wachache sana wanpata madhara (jinsi ilivyo kila chanjo).
 
Waajiriwa wa serikali wote sasa msimamo wao ni ule wa boss wao ... hakuna kingine
 
Inategemea unakunywa wakati gani ,waswahili tuna hili kambale mkunje angali mbichi. usingojee mpaka umekakamaa ndio unatafuta malimao na tangawizi,kama ulikuwa mtu wa kahawa na chai sasa ni chai ya tangawizi kwa limao unaongeza na karafuu za pemba tatu au zaidi ili kuongeza uhalisia badara ya sukari ya mabeberu tumia asali mwitu kwa maana usitumie zile asalai zilizosafishwa na kuchakachuliwa.
Rais wa Zanzibar ameeleza kuwa hali ni mbaya kule wanakabiliwa na Corona karafuu mbona wanazo nyingi hazijasaidia mkuu hata limao na tangawizi zipo nyingi. Mimi naona tusiingize ushabiki kwenye maisha ya watu
 
Hujui kuwa Tangawizi na Limao imekuwa ikitumika miaka mingi kuponyesha mafua na magonjwa yanayohusiana na upumuaji?? Waulize wazee wako bahati mbaya umekalia kugoogle tu! Watumie wazee watakupa maarifa mengi sana.
Wew utakuwa na matatizo ya ubongo siyo.

Uliwa kusoma wapi viral effection diseases, ina kuwa treated na limao na tangawizi asee.
 
Wala usishangae, hata CV yake na thesis ya PHD unaona unaona ali based sana kwenye coral reef fisheries biology...sasa mambo ya dawa za chanjo atueleze kitu gani kipya. Yeye angekuja tu akatupa mrejesho wa dawa yetu ya Madagascar uchunguzi umefikia wapi, haya ya chanjo naona yako juu ya uelewa wake!
Yaani prof mzima anaongea utopolo namna hii? Huyu si alikuwa taaluma UDSM?
 
Prof. Yunus Mgaya hana uzoefu wowote ule wa kile anachoongelea.

Cheki alichosoma:
Yunus Mgaya is Tanzanian, born in 1957. He studied at the University of Dar es Salaam, the University of British Columbia and the University College Galway in Ireland. His research has focused mainly on coral reef fisheries, biology and management of invertebrate fisheries as well as aquaculture of different species.

Hivyo basi pale NIMR yeye ni administrator tu , hana utaalam wowote juu ya viruses.
 
Mkuu kama ndio hivyo ni kwa nini tumekua tukitumia mabilioni kila mwaka kuagiza madawa ya mafua, upumuaji, athma na magonjwa ya mfumo wa hewa badala ya kutumia tangawizi na limao?

Kwa nini serikali imekua ikitumia hela zote hizo huku dawa ya hayo magonjwa inajulikana miaka mingi?

Wakikujibu niite hao wafia tumbo!
 
Sawa tuwaambie wahisani waache kutusumbua na mavidonge yao ya ARV ili tujishughulikie kwa nyungu malimao na Tangawizi au sio Ndugu?
Mkuu Imhotep, mpaka sasa ni mtu mmoja tu tena Mwafrica kama wewe, ambaye amewahi kutibu wagonjwa wa Ukimwi Ila hao unaowapenda Sana walimnyonga, na ndiyo Maana inatubidi turudue akili zetu waafrica,

Ndiyo yaweza kuwa tuko nyuma Sana Ki teknorojia lakini hata akili ya kuhoji kipi ni kipi tusiwe nayo?

Si tutakuwa wapumbavu kama ilivyo Chadema na wapambe wake
 
Ni mtu mmoja tu tena Mwafrica kama wewe, ambaye amewahi kutibu wagonjwa wa Ukimwi Ila hao unaowapenda Sana walimnyonga, na ndiyo Maana inatubidi turudue akili zetu waafrica...
Usiwe mjinga.

Suala la Public Health unaanza kuingiza sentiments za siasa, ati CHADEMA.

Hivi una akili weye?

Ndiyo mnakipa jina baya chama chetu CCM.
 
Back
Top Bottom