Nimwombe Rais Samia awaondoe haraka wanajeshi wetu kule DRC Congo. Mnapigana na nchi ya EAC

Lakini nae inasemwa kuwa aliibiwa madini sana na PK kwenye ukuta aliojenga Mererani
 
Biashara yetu na Kenya ni kubwa kwa sababu Kenya ni tajiri wa kipato kuliko sisi na ina uchumi mkubwa, suala la amani ni nyongeza tu, unaweza kuwa na amani na ukawa masikini.
 
Mabadiliko ya tawala kutoka kiimla mpaka kidemokrasia huko Kampala na Kigali ndio mwanzo wa kurejea kwa amani na utulivu huko Drc mashariki
 
Kuuawa askari imetokea tu kama Bahati mbaya,unajua vita vya DRC ni kama mradi?
Inasemekana baadhi ya askari wetu wanaotoa hadi hongo,waende huko, kwasababu pesa wanazolipwa ni nyingi sana,ndo ambazo wakitoka huko wakifika huku wanaanza kujenga majumba na starehe mbalimbali.
Imetokea tu.
 
Biashara yetu na Kenya ni kubwa kwa sababu Kenya ni tajiri wa kipato kuliko sisi na ina uchumi mkubwa, suala la amani ni nyongeza tu, unaweza kuwa na amani na ukawa masikini.

..mahali penye vita ni vigumu wananchi wake kufanya shughuli za uzalishaji mali na matokeo yake ni umasikini.
 
Mabadiliko ya tawala kutoka kiimla mpaka kidemokrasia huko Kampala na Kigali ndio mwanzo wa kurejea kwa amani na utulivu huko Drc mashariki

..ni vigumu sana watawala wa Rwanda na Uganda kuruhusu demokrasia.

..Si umeona Museveni amemteua mwanae kuwa Mkuu wa majeshi?

..kuna kipindi huko nyuma Museveni alimteua mdogo wake kuwa Mkuu wa majeshi.
 
Hizo tawala Zina mwisho mkuu
 
Na Kagame siyo wa mchezo mchezo. Ni Putin wa Afrika huyu, akiamua kumung'oa mama jua halizami.

PK aliwahi kumwambia JK, I will hit you!. JK hakutia neno.
Awachezee hao hao kongo lakini sio TZ.
Amuulize Iddi Amin Dada alifanywa nini na TZ
 
Utulivu uliokuwepo wakati wa Mobotu ilikuwa ni kwa sababu ya msaada wa USA kwa sababu Mobotu alikuwa adui wa Ukomunisti, baada ya Ukomunisti kuanguka na vita baridi kuisha Mobutu alikosa umuhimu kwa US akapoteza uungwaji mkono, maovu yake waliyokuwa wanayafumbia macho muda mrefu yakaanza kupewa uzito ndipo hapo na waasi na wapinzani wakarejea ulingoni Congo kwa nguvu kubwa sana. Mojawapo ya hao waasi ni Laurent Kabila ambaye alipata msaada na ushirikiano mkubwa kutoka kwa Kagame, Museveni na hata Tanzania.

Tangu wakati huo vurugu na maasi zimekuwa na muendelezo DRC kwa sababu Laurent Kabila hakuweza kutawala au kuidhibiti DRC vizuri na zaidi sana aligombana na kutofautiana na warlords wenzake, Kagame na Museveni walioshiriki kumuweka madarakani.
 
Huo wimbo wa mabeberu umepitwa na wakati, China ndio mvunaji mkubwa wa madini na mbao huko DRC kwa sasa kwa njia halali na haramu.
 
Mabadiliko ya tawala kutoka kiimla mpaka kidemokrasia huko Kampala na Kigali ndio mwanzo wa kurejea kwa amani na utulivu huko Drc mashariki
Hakuna dalili demokrasia itapata nafasi Kampala au Kigali kwa miaka mingi ijayo, lakini pia DRC imekuwa ikitawaliwa kiimla tena na madikteta wajinga kwa muda mrefu sana, hata Tshisekedi aliporewa ushindi na Kabila kutoka kwa Fayulu ili awe kibara wake na amlinde.
 
Mwombe kagame aondoe majeshi yake Congo anapigana na nchi za EAC.
 
Na Kagame siyo wa mchezo mchezo. Ni Putin wa Afrika huyu, akiamua kumung'oa mama jua halizami.

PK aliwahi kumwambia JK, I will hit you!. JK hakutia neno.
Story za vijiweni hizi na ovyo kabisa! Mheshimu Amiri Jeshi Mkuu wetu na nchi. Hao M23 ulisahau walivyochapwa enzi za Mwakibola? Muhimu tuiombee DRC amani, wahuni waondoke na askari wetu waendelee kuwa salama. πŸ™πŸ™πŸ™
 
Na Kagame siyo wa mchezo mchezo. Ni Putin wa Afrika huyu, akiamua kumung'oa mama jua halizami.

PK aliwahi kumwambia JK, I will hit you!. JK hakutia neno.
Alisikika mlevi mmoja akiwa mitaa ya Manzese Mtaa wa Fisi πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Kagame ni Putin wa Africa. Usiwe mbishi dogo. Kagame akikutaka wewe hakukosi
 
The thing is, tukiwaacha Congo, siku M23 wakishinda vita next stop ni kwetu..
Kuliko kupigana vita kwenye ardhi yetu ni bora tutume vikosi nje hata miaka 100 kama vitasaidia vita isije kwetu.

Hio ndio sababu tunaendelea kutuma vikosi, bila kutuma watu Congo mpaka leo ile vita ingekua imehamia Kigoma, na tusingekua tunaingelea wanajeshi watatu kufa, tungekua tunaongelea wananchi 70 na wanajeshi 10+ kufa..
 
Tofauti yetu na east Congo ni kwamba Nyerere alitumia jitihada nyingi sana kwenye nationalism.

Tanzania sijui sehemu nyingine zaidi ya Ngara (I’m open for education) na tena kabilla la wahangaza tu wanaongea Kinyarwanda tena as a second language, lakini Kiswahili ndio lugha kuu.

Na wahangaza ninao wajua mimi walio kulia Dar ni waswahili pengine wazaramo na wandengereko kunishinda (mind you upande wa mams yangu ni wandengereko huo uswahili kwetu ni wakunitisha).

Isitoshe asilimia kubwa ya hayo makabila ya mpakani wanajitambua kama watanzania kuliko hizo lebel za uasi mnazotaka kuwapa. Hata huko vijijini ambapo wapo watu wa makabila ya mpakani wanaokaribisha raia wa nchi jirani. Ni watu wanaoishi huko huko wenye kuongea lugha moja na hao wageni ndio wanao report uingiaji wa waamiaji haramu (ndio tuelewe umuhimu wa natiolism propaganda na kazi kubwa aliyofanya JKN) sio rahisi kama tunsvyodhani wengi wetu.

Hiyo inakwambia muhimu ni nationalism efforts ya mipaka yetu kuliko kutaka kuwapa watu wa mipakani labels za hovyo and mistrust kisa wanaongea lugha moja na watu wa nchi jirani.

Sisi wenyewe ndio tunaotaka kuchochea huo mgawanyiko kwetu ambao aupo; be careful na wachangiaji wa JF kuna mijitu ina agenda zao. Unakuta jitu kila siku yeye ni mada za ugomvi wa kidini tu we vipi.
 
Matatizo ya vita ya Congo ni jeshi la Congo kuwa very corrupted !
Congo sio wa kuwaamini kushirikiana nao kwenye vita !
Kuna uwezekano baadhi ya wanajeshi wa Congo wako upande wa M23 na upande wa nchi Yao wanacheza kote kote Shauri ya biashara ya dhahabu .
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…