Nina 5,000,000 tu. Naweza kununua gari ipi ikiwa na hali nzuri?


Ukweli mtupu KANYEGELO
 
Hizo gari tajwa ni za vijana wasio na vision?
 
Acha kutisha watu. Hujui hata atakuwa analitumiaje ushaanza mkwara. Jua kwanza matumizi yake ya gari ndio ujue ushauri mzuri / mbaya
 
Waungwana nimechoka kutembea kwa mguu, Nina ka milioni 5 nilitaka nitafute ka miguu minne nipumzike shida kutembea, ila sina uzoefu na mambo ya magari ni aina zipi za magari naweza kununua ikiwa na hali nzuri kwa hiyo bei?
Kwa hizo hela mkuu njoo hapa maskani tuongee, nina kabajaji used nitakupunguzia 2,000 tu ili upate nauli ya kurudia home.
 
Kama fungu linatoka ofisini kwa ajili ya wese hata ukimiliki 5.7L V8 haina shida
 
nakushauri ni bora weka fixed account mpaka kuwa sawa.

ilishanitokea na nilijuta mpaka kuliuza kwa hasara
Tatizo ni kuwa mnakurupukaga yani! Huna uzoefu wa gari tafta mtu anayezijua gari ndio uende nae kununua gari! Gari ya kitonga hakikisha ni ya Toyota na anayeiuza hio gari anashida ya hela tu sio wale ambao hana hela gari imemshinda ndio anauza huwa gari zao zinakuwaga vimeo sana!

Nina best yangu juzi kanunua Mini Cooper ya mkononi ile gari kauziwa 4.5M ila iko na vipengele vya kutosha😅 yani kabla hata ya diagnosis kufanyika. Hakuomba ushauri wala nini na yeye sio mzoefu wa magari kabisa ila kwa kuwa mini cooper imekaa kibishoo yeye kaona freshi tu na vile namba ni DK.

Aliniomba nimsaidie kuiendesha toka gereji mpaka kwake maana hata leseni hana. Kilichotokea kwanza steering ni ngumu kuliko fiat mbaula 😅 yani kufika mtaani ilibidi niagize ugali mkubwa. Pia gari inasita sita ikiwa kwenye gear ya kwanza ila ikichanganya inatulia. Side mirror ya kushoto mbovu. Mguu wa nyuma unagonga yani gari iko na stiff suspension utafikiri haina shock absobers yani kama gari iliofungwa matairi kwenye chassis! Taa baadhi haziwaki yani na dashboard lights ya tire pressure sensor iko on, ya alama ya radi ipo on yani kwa navyojua BMW zilivyo pale ikipigwa diagnosis mkeka wake hautapungua 3M kuiweka gari sawa.
 

Sikurupuki labda kama unataka kumuingiza kingi huyo mwenye kutaka gari.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…