Pole sana mkuu.
Huko kwenye uvuvi ni kipato gani hicho kidogo kisichotosheleza??
Kwanini usijibane hukohuko utoke na mtaji, kwa dunia ya sasa usijipush mwenyewe kujikwamua basi usitegemee kuna mtu atakuwazia hata ndguzo/wazazi ukifika umri fulani unaachwa ujitegemee.
Mtu hakushiki mkono kama hanufaiki na wewe. Jibane uanze biashara.
Humu jf kuna nyuzi nyingi mno za biashara mbalimbali hata za hiyo laki moja unayoidharau.
Kikubwa ni taarifa sahihi, huo ndo mtaji wako. Tumia smartphone yako kutafuta taarifa sahihi.