Nina haja ya dhati Lamomy wa JF kwenye maisha na huduma yangu daima

Oohh hallelujah Jehovah Jyire,

Mungu ni Mwema wapendwa....

Asante Yesu kwa kibali chako wasaa huu muhimu tena jioni ya leo...
Baraka na Neema zako zikaambatane nasi sote katika mazungumzo, majadiliano, mafunzo, masemezano na maelekezano. Roho Mtakatifu naomba Muongozo wako mwema kwa niaba ya watumishi wako wote humu jukwaani..

Mtumishi Lamomy na mwenzi wako wa pekee Countrywide. Mwenyezi Mungu awabariki sana na awalinde daima.
Mahusiano na pengine ndoa yenu ikawe daima ya furaha, amani na upendo wa kiMungu.
Daima uaminifu, msamaha na kuelekezana kwa upole na upendo vikatamalaki ndani ya mioyo yenu na nyumba yenu yote. Mungu anawapenda sana kwa hakika.

Imeandikwa,
Mke wako atakua kama mzabibu, wenye kuzaa matunda yaliyo mema ndani ya nyumba yako..
Mungu wa Mbinguni awajaalie kuzaa matunda yaliyo mema na yenye furaha ndani ya nyumba yenu.

Baada ya kusoma majibu ya waraka wako wa kichingaji dhidi yangu, mtumishi Lamomy niliingia kwenye maombi makali kidogo kuomba na kuskiliza malekezo ya Roho Mtakatifu, kabla sijaja kuupokea ukweli ambao kwa hakika umeniweka huru.
Mungu amenibariki na amekubariki sana, sana,sanaaaa..

Roho mtakatifu amenielekeza kwa ujasiri na upendo mkuu, kuupokea ukweli wako kwangu kwa mikono miwili na kuutii kikamilifu kwa heshima, sifa na utukufu wa jina lake mwenyewe.

Amenihakikishia kwamba siko pekeyangu ktkt hili, sijapotea, sintapotea, ananilinda na ananichunga vema kimwili na kiroho, na hivyo nisiogope wala kutetereka. Siko pekeyangu, niko salama na Mungu Mwenye.

Na kwakweli kupitia kwako mtumishi Lamomy, yawezekana ndipo lipo daraja la mimi mtumishi nisie stahili kuvuka na hatimae kufika ninapostahili kuwa...

Naendelea kumuomba Roho Mtakatifu kila wakati, ili hatimae lile ambalo limeandaliwa kwajili yangu mimi mtumishi nisie stahili kustahilishwa kwa wakati wa Mungu.

Nimefurahi sana, na nimashukuru Mungu kwa yote....

Ninawaombea baraka na Neema wale wote walionitakia mema kwa sadaka na maombi ya kufanikiwa katika hili.
Mungu awabariki sana, bado tunayo nafasi kutoka hapo tulipoishia na Roho Mtakatifu anataka tusonge mbele bila kukata tamaa kwa upendo, amani shangwe na vigeleveli katika utukufu wa Mungu...
Aimen.....
Kwakwo mtumishi Lamomy
 
Kwa nn unaandika comment ndefu sana? Una muda mwingi sana?
 
Unaandika sana bwana....we sema tu umeelewa inatosha🀣🀣🀣🀣🀣
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…