Yes, mkuu ndio tumepatiwa hayo majibu hospital na imebidi tulipe gharama Bima ikawekwa pembeni, sasa nauliza kwanini?
kama ni Hospitali wamekiuka Masharti ya mkataba wa Bima ya Taifa ya afya NHIF..
kwa sababu;-
1. kwa Swala la kwanza: Kusubiri Wiki 2 au Mwezi (Waiting Period)
Ni kweli bima iliweka utaratibu ambao unajulikana kama
"Frequency Control." na lengo sio kumzuia mgonjwa lengo lilkuwa ni
Kuzuia Udanganyifu (Fraud Control) kuna kipindi kulikuwa na mchezo wa watu kuazimana kadi. Mtu mmoja anatumia kadi asubuhi, kisha anampa ndugu yake aitumie mchana kwa ugonjwa mwingine. Kuweka ukomo wa muda kunasaidia kuzuia kadi moja kutumika na watu wengi kwa wakati mmoja.,...
kwahiyo ndo likatambulishwa swala la 72 hours consultation period yaani ukipata
"Authorization" ya kutibiwa inadumu kwa siku tatu kwahyo kwenye kipindi chote hicho huwezi kupata new attendance unless its a
Re-attendance na mara nyingi mtu anakuja kwa ajili ya tatizo lile lile na consultation fees hugawanywa kuwa nusu..
lets say 50,000/= ndo pesa ya consultation (kumuona Daktari) ukija ndani ya masaa 72 ,italipwa 25k na uwe na sababu maalumu ya kurudi......Na hapa ndo hufanya hospitali nyingine kuwakataa wagonjwa.....
ila Pia waginjwa tukubali kukamilisha dozi kabla hujaenda kutibiwa tena we umepewa antibiotic leo Hospitalini umetumia siku ya kwanza siku ya pili au ya tatu umeenda unasema bado hujapona tunashindwa kuelewa kuwa daktari anapokupa dawa leo, anategemea uone mabadiliko baada ya muda fulani (mara nyingi siku 7 mpaka 14). Bima inaamini kuwa ndani ya wiki mbili unapaswa kuwa bado unatumia dawa ulizopewa..
kwahyo huwezi ukaandikiwa umetibiwa UTI au ugonjwa wowote leo na ukategemea kesho au kesho kutwa utapimwa vipimo vile vile na upewe dawa zile zile na utibiwe vile vile hiyo BIma wataiona kama ni udanganyifu wa matibabu kwahyo watakata folio nzima so ilikuepuka Hilo Hospitali nyingi huktaa wateja wanaorudi kwa shida hiyo hiyo mpaka wamalize dozi ya dawa walizopangiwa unless uende una tatizo jingine..
2. Swala la pili Kuonana na Daktari Mmoja kwa Siku (Single Consultation)
Claim yako kuwa Zamani ilikuwa rahisi "kuzunguka" kliniki zote, lakini sasa hivi haiwezekani..
kila kitu kina mpangilio mkuu, Yaani huwezi ukataka kuonana na madaktari 6 kwa siku moja na wote wakiwa na level sawa ya proffesional ukumbuke pia na wao wanalipwa consultation fees sasa wote 6 wakilipwa wamekutibu mtu mmoja huoni kutakuwa na treatment confusion?
lakini pia Bima zinajaribu kupunguza gharama hizi ili mfuko usifulie (bankruptcy).
lakini pia Kidaktari, si vizuri mgonjwa mmoja kupata dawa kutoka kwa madaktari watano tofauti kwa siku moja bila wao kuratibu. Kuna hatari ya dawa kuingiliana (
Drug Interaction) na kumdhuru mgonjwa, zamani daktari alikuwa anamtibu mgonjwa mmoja mpaka apone na alikuwa anaambiwa mgonjwa wako fulani kaja..hiyo inatoa picha kuwa hata mgonjwa akipata changamoto yoyote unajua sehemu gani ya kuanzia..
siku hizi ukitumia dawa asubuhi ukiona haijakupa matokeo unavyotaka mchana umeenda kwa mwingine kakupa dawa na usiku kakupa pia dawa sio sahihi...
unapaswa kwenda kwa daktari mmoja na kama daktari huyo akiona vipi yeye ndo ataamua matibabu yako..
yaani Ukweli ni kwamba unaweza kuonana na madaktari zaidi ya mmoja kwa siku, lakini
lazima kuwe na mtiririko wa kitaalamu wa rufaaa (Referral Flow), kama endapo utahitajika kwenda kwa daktari bingwa au bingwa mbobezi zaidi ya aliyekutibu, Ila huwezi kutoka kwa GP/MD na ukataka uende tena kwa GP taratibu za kimatibabau haziruhusu ,Taratibu zinataka uonane na daktari wa awali (General Practitioner), ambaye yeye ndiye atakayeamua kama unahitaji kuonana na daktari bingwa (Specialist). Ukihitaji kuonana na wabingwa wengi, daktari mratibu anapaswa kuandika maelezo maalum....na inaruhusiwa vinginevyo BIMA inaona kama ni njama ya kutaka kufanya POLY claim ili kujipatia kipato na inakata form zote ...na hospitali haziko radhi kupoteza mapato na ndo maana hupinga kumpokea mgonjwa mwenye kutaka dizaini hii ya matiabu