Nina Mgogoro kwenye ndoa, kila pesa anayopata Mke wangu anaenda kujenga kwao. Naomba msaada

Mshike vizuri tumebaki mimi yeye na wengine 7 nchi nzima🤩🤩
Hua akiingia Jf akasoma matukio basi mwisho wa siku ananisimulia kama hadithi, na kwapamoja tunamshukuru Mungu.
 
Kama umeshasema kakuzidi kipato hayo mbona yanatarajiwa.

Katika mambo ya kuombea yasitokee kwenye ndoa ni Mke kuzidi kipato, kama bado unaitaka ndoa kuwa mpole.
 
Hua akiingia Jf akasoma matukio basi mwisho wa siku ananisimulia kama hadithi, na kwapamoja tunamshukuru Mungu.
Hawakukosea waliosema ukipata mke au mume aliye sahihi basi umepata pepo,, mwenzetu uko peponi unaenjoy tu
 
Kwa sababu wewe unaona ambacho yeye haoni...wewe tulia Tu ...subiri mda ufike ajifunze mwenyewe.

Nenda nae taratibu...ukifika wakati anagombea nyumba na ndugu zake ndo umwambie nilikuonya Sana unaona?

Kwa sasa subiri Tu mda utatoa majibu
Naunga mkono hoja hii
 
Mmmmh
 
Wakuu, mmeoa wanawake wa hovyo sana, hilo tu.
 
Hii ndio shida ya wanandoa kutokuwa watu wa kushauriana kabla ya kufanya maamuzi yenu.

Hapo ni hasira tu najua mtapatana na hizi hasira ulizonazo zitaisha ila tegemea hii kuwa tabia yake endelevu.

Hamjachelewa kikubwa jifunzeni kuwa watu wa kushauriana.
 
Tafuta hela.
We unaumia na 20M aliyokopa serikalini, si na wewe ukakope benki au kwingineko ili kuwatengezea future watoto wenu?
Kumbuka, pesa zake ni zake. Pesa zako ni zenu.
Hiyo kichwa yako imejaa maji ya mvua mkuu, fanya upasuaji
 
Hivi? Hajui ile nyumba hawataishi watoto wake? Hivi hajui ile nyumba watagombea vidume?

Ndani ni kuchuniana. Najuta sana kuoa mwanamke huyu.

Niko puzzled. Epuka kusomesha mchumba.

Mkuu mwanamke akiolewa sio kwamba ndio anakata mahusiano na familia yake...

Kama Mungu kamuinua kifedha, mwache arekebishe hali ngumu ya makazi ambayo mama yake ameipitia miaka na miaka...

Unachopaswa wewe ni kumshauri kwa busara na hekima na sio hasira, mwisho wa siku utajikuta unazua ugomvi kwa vitu vidogo tu mlivyopaswa kuelewana...

Wewe sasa pambania familia yako nayo iwe na mji, usijeukawa kama baba mkwe ambaye 'alipofariki' alimuacha mama mkwe pasipo mahali paziri pa kuishi...
 
Una uhakika ujenzi hautaisha Kwa huyo mkewe??,,sababu amekopa??au ni fikra,,Maono,,na mitazamo yako ya kwamba kila anae kopa kwa ajili ya kujenga hamalizi kujenga??
Mkuu hujasoma ukamaliza? Amekopa mara ya kwanza ujenzi haukuisha mume akamwambia mke ujenzi ni polepole ikabidi mke akope tena M20 akapeleka kumalizia.

Sasa huoni tayari hapo ni liability kubwa (mke na mikopo) na ndio chanzo cha ugomvi
 
Nyumba anayojenga ni yake yeye, hayo maneno ulioambiwa ni ujanja tu wa kuweka uhalali kinachofanyika.

Wanawake si watu wa kutegemea, mara zote hufikiria kuwa na maisha mengine nje ya maisha ya ndoa
 
Kwa sababu wewe unaona ambacho yeye haoni...wewe tulia Tu ...subiri mda ufike ajifunze mwenyewe.

Nenda nae taratibu...ukifika wakati anagombea nyumba na ndugu zake ndo umwambie nilikuonya Sana unaona?

Kwa sasa subiri Tu mda utatoa majibu
Aendelee kusubiria ilihali hali anayopitia haihimiliki hata kwa sekunde tu, au unataka alazimishe furaha hatimaye afe kwa BP, Kisukari, Vidonda vya tumbo na Stroke tokana na excessive family stress?

Sent from my CPH2387 using JamiiForums mobile app
 
Kama anajenga kwa pesa yake ni sawa,huo mkopo atalipa yeye..wewe pesa yako jenga hiyo yako,ingekua ni mimi ningemwacha ajenge kiroho safi
Tatizo alimsomesha Mchumba (Ke) kwa mategemeo makubwa ya "kusaidiana kifamilia".

USHAURI KWA ME:

1. Ke hata akiwa anapata M 10 mshahara na Me M 2, eleweni M 2 ndiyo itayotumika kwa kila hitaji la kifamilia.

2. Me ndiye kichwa cha familia ila Ke ni msaidizi tu(90% matumizi ya fedha ni Me na 10% ni Ke na ni hiyari ya Ke, sana sana Ke ni kuzaa Watoto na kuwalea kwa maadili mema tu).

3. Tumieni kanuni no. 1 ikiwa no. 2 hamjaeilewa katika maisha ya ndoa.



Sent from my CPH2387 using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…