Nina Mgogoro kwenye ndoa, kila pesa anayopata Mke wangu anaenda kujenga kwao. Naomba msaada

Nina Mgogoro kwenye ndoa, kila pesa anayopata Mke wangu anaenda kujenga kwao. Naomba msaada

Mshike vizuri tumebaki mimi yeye na wengine 7 nchi nzima🤩🤩
Hua akiingia Jf akasoma matukio basi mwisho wa siku ananisimulia kama hadithi, na kwapamoja tunamshukuru Mungu.
 
Kama umeshasema kakuzidi kipato hayo mbona yanatarajiwa.

Katika mambo ya kuombea yasitokee kwenye ndoa ni Mke kuzidi kipato, kama bado unaitaka ndoa kuwa mpole.
 
Hua akiingia Jf akasoma matukio basi mwisho wa siku ananisimulia kama hadithi, na kwapamoja tunamshukuru Mungu.
Hawakukosea waliosema ukipata mke au mume aliye sahihi basi umepata pepo,, mwenzetu uko peponi unaenjoy tu
 
Kwa sababu wewe unaona ambacho yeye haoni...wewe tulia Tu ...subiri mda ufike ajifunze mwenyewe.

Nenda nae taratibu...ukifika wakati anagombea nyumba na ndugu zake ndo umwambie nilikuonya Sana unaona?

Kwa sasa subiri Tu mda utatoa majibu
Naunga mkono hoja hii
 
Let me put my advice in english may be you will understand
She simply does not care about you. I have more than ten years experience, so i know whereof i speak.You need to save yourself from yourself

Life is too short, there is no reason for you to be unhappy with a partner that doesn't want to cooperate when there a hundreds of women that will appreciate and cooperate with you on your goals. Dump her ASAP[emoji23]
Mmmmh
 
Hii ndio shida ya wanandoa kutokuwa watu wa kushauriana kabla ya kufanya maamuzi yenu.

Hapo ni hasira tu najua mtapatana na hizi hasira ulizonazo zitaisha ila tegemea hii kuwa tabia yake endelevu.

Hamjachelewa kikubwa jifunzeni kuwa watu wa kushauriana.
 
Tafuta hela.
We unaumia na 20M aliyokopa serikalini, si na wewe ukakope benki au kwingineko ili kuwatengezea future watoto wenu?
Kumbuka, pesa zake ni zake. Pesa zako ni zenu.
Hiyo kichwa yako imejaa maji ya mvua mkuu, fanya upasuaji
 
Hivi? Hajui ile nyumba hawataishi watoto wake? Hivi hajui ile nyumba watagombea vidume?

Ndani ni kuchuniana. Najuta sana kuoa mwanamke huyu.

Niko puzzled. Epuka kusomesha mchumba.

Mkuu mwanamke akiolewa sio kwamba ndio anakata mahusiano na familia yake...

Kama Mungu kamuinua kifedha, mwache arekebishe hali ngumu ya makazi ambayo mama yake ameipitia miaka na miaka...

Unachopaswa wewe ni kumshauri kwa busara na hekima na sio hasira, mwisho wa siku utajikuta unazua ugomvi kwa vitu vidogo tu mlivyopaswa kuelewana...

Wewe sasa pambania familia yako nayo iwe na mji, usijeukawa kama baba mkwe ambaye 'alipofariki' alimuacha mama mkwe pasipo mahali paziri pa kuishi...
 
Una uhakika ujenzi hautaisha Kwa huyo mkewe??,,sababu amekopa??au ni fikra,,Maono,,na mitazamo yako ya kwamba kila anae kopa kwa ajili ya kujenga hamalizi kujenga??
Mkuu hujasoma ukamaliza? Amekopa mara ya kwanza ujenzi haukuisha mume akamwambia mke ujenzi ni polepole ikabidi mke akope tena M20 akapeleka kumalizia.

Sasa huoni tayari hapo ni liability kubwa (mke na mikopo) na ndio chanzo cha ugomvi
 
Nipo kwenye ndoa nimekuwa nikisoma tu lakini naona na mimi limenikuta.

Iko hivi wife na mimi tulifahamiana kijijini. Nilikuwa f6 yeye akiwa f4 leaver. Nilimsaidia akapata chuo cha takwimu akaenda akafanya akapata cheti. Wakati akiwa chuo nliamua kudate nae tukaoana (marriage) nikiwa nafanya kazi na yeye akiwa chuo.

Miaka mitatu baadae tulijaaliwa watoto wazuri. Maisha yaliendelea nikiwa kazini na yeye akiwa ofisi moja masuala ya takwimu nchini.

Mambo ya ndoa yalikuwa safi sana nilii injoi ndoa labda kwa sababu ilikuwa ya kusafiria. Maana yeye mkoa mimi mkoani.

Nilifanikiwa kumuhamishia mkoani kwangu yeye na watoto. Tuliishi vizuri kwa wastani wa miaka 5. Baadae mzazi wake yaani mkwe aka experience wakati mgumu (code). Tukashauriana tumjengee kibanda. Kwa kuwa wapo watoto wakubwa wakaona washirikiane wote. Kwa kuwa wife nde mwenye kipato kizuri akakopa banki 27M lakini nyumba haijaisha.

Kero ikaanza sasa. Kila wakati anataka pesa ya ujenzi kwa mama mkwe. Kumbuka yule ni mzee ile nyumba watakuja kugombana watoto nikamwambia ujenzi hauishi siku moja. Buy time.

Majuzi alipata bingo ofisini kwao 20 Mil ni pesa ya offer ya Serikali yenye riba kidogo.

Lahaulaaa si akaipeleka yote kwenye ule ujenzi.

Wana JF wenzangu, kumbuka si kwamba sisi na watoto wetu hatuna mahitaji, hapa ada, nyumba haijaisha asilimia Mia. Why apeleke 20 kwao? Mwanamke kiumbe wa ajabu sana.

Hivi? Hajui ile nyumba hawataishi watoto wake? Hivi hajui ile nyumba watagombea vidume?

Ndani ni kuchuniana. Najuta sana kuoa mwanamke huyu.

Niko puzzled. Epuka kusomesha mchumba.
Nyumba anayojenga ni yake yeye, hayo maneno ulioambiwa ni ujanja tu wa kuweka uhalali kinachofanyika.

Wanawake si watu wa kutegemea, mara zote hufikiria kuwa na maisha mengine nje ya maisha ya ndoa
 
Kwa sababu wewe unaona ambacho yeye haoni...wewe tulia Tu ...subiri mda ufike ajifunze mwenyewe.

Nenda nae taratibu...ukifika wakati anagombea nyumba na ndugu zake ndo umwambie nilikuonya Sana unaona?

Kwa sasa subiri Tu mda utatoa majibu
Aendelee kusubiria ilihali hali anayopitia haihimiliki hata kwa sekunde tu, au unataka alazimishe furaha hatimaye afe kwa BP, Kisukari, Vidonda vya tumbo na Stroke tokana na excessive family stress?

Sent from my CPH2387 using JamiiForums mobile app
 
Kama anajenga kwa pesa yake ni sawa,huo mkopo atalipa yeye..wewe pesa yako jenga hiyo yako,ingekua ni mimi ningemwacha ajenge kiroho safi
Tatizo alimsomesha Mchumba (Ke) kwa mategemeo makubwa ya "kusaidiana kifamilia".

USHAURI KWA ME:

1. Ke hata akiwa anapata M 10 mshahara na Me M 2, eleweni M 2 ndiyo itayotumika kwa kila hitaji la kifamilia.

2. Me ndiye kichwa cha familia ila Ke ni msaidizi tu(90% matumizi ya fedha ni Me na 10% ni Ke na ni hiyari ya Ke, sana sana Ke ni kuzaa Watoto na kuwalea kwa maadili mema tu).

3. Tumieni kanuni no. 1 ikiwa no. 2 hamjaeilewa katika maisha ya ndoa.



Sent from my CPH2387 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom