Nina Mgogoro kwenye ndoa, kila pesa anayopata Mke wangu anaenda kujenga kwao. Naomba msaada

Nina Mgogoro kwenye ndoa, kila pesa anayopata Mke wangu anaenda kujenga kwao. Naomba msaada

Not easy as you suggested! Divorce is something very complex, it has some ambiguities that no one want it
It's not too hard, the divorce can go as smoothly or as roughly as you want. The choice is yours
 
Umeona ee kama pesa ni yake amwache ajenge tu
Mtu anajenga kwao kuwasitiri wazazi ni jambo zuri,mana hata wanao wakiende kusalimia watalala hapo...ndio ndoa zetu zilivyo,mimi hata angesema anakopa IMF ni sawa si mkopo analipa yeye
 
Ila nyie wanaume hamueleweki, wakati ule nikipata kale ka mshahara ka miaka ile nilikuwa naweka mezani hela inapangiwa bajeti,

Kuja kushtuka mtaa wa tatu keshazaa watoto wawili.

Sometimes mnaboa
Pole best....mimi sijui hata mia yake mana natoa matumizi ya wiki,ada zote nalipa kwahiyo pesa yake yeye atajua anafanyia nini,ada za watoto anakusanya yeye bt zinatoka kwenye apartment zangu
 
Pesa yake? Unamaanisha nini?
Hiyo mikopo ya Milioni 27 & milioni 20 mumewe anahusika moja kwa moja hivyo ni lazima ashirikishwe.
Kimsingi hiyo hela lazima wakubaliane kabla ya kukopa na matumizi yake.....
Ngoja mkeo ashindwe kulipa hiyo mikopo ndio utajua hujui....
Ukijifanya mpuuzi wa kutofuatilia mienendo ya mikopo ya mkeo, jua tu huna tofauti na Mangungo wa Msovero aliyeuziwa mbuzi kwenye gunia....
Mwaka jana tu jirani yangu karibia afe kwa presha; Katoka zake kwenye mihangaiko kakutana na bango kubwa nje ya nyumbani yake; Nyumba hii inauzwa!!! kumbe mkewe alikopa....NMB walitaka kufanya yao
Toka lini hata ukaweka nyumbani kwa hawa wanawake zetu wenye vikoba 10...kwa maelezo yke mke kakopa kma yeye labda kupitia kazi yake.istoshe huyo jirani yako hiyo kesi nyepesi sana.
Unakopeshaje hati ya nyumba bila mwenye jina kusign
 
Ni kweli anajenga kwa pesa yake. Lakini mwenzetu ndiye anayeiangalia familia kwani mama pesa yake inalipia madeni aliyokopa. Mzigo umemzidi uzito.
Hakuna namna mwanaume tunakula kwa jasho ...pesa ya mke hata bure siitaki afanye maendeleo yake
 
Mkeo mama huruma

Huu uzi nimeuelewa na nimeshamfahamu mke wako, tupo ofisi moja, na hizo bingo wengi wamepewa hapa ofisini. Ni kweli alikuwa anatueleza kuwa hiyo hela ataipeleka kumalizia nyumba ya mzazi wake hadi wengine tukashituka ingawa mimi sipo kwenye waliopewa huo mkopo.
 
Wewe unaGombana na mkeo kwa jambo la kijinga sana,unataka asijenge kwao!? Ishini na wake zenu kwa akili,mimi mke wangu juzi kakopa milioni 10 akaenda kukarabati nyumbani kwao ilikhali sisi tuko katika nyumba ya kupanga.
Pigia mstari neno ishini nao kwa akili.
Kwaio unaona mkeo ana akili timamu kweli? Na wewe ukamshauri hivyo
 
sijaona unacho lalamika, kwanza mkeo anakupenda ndiyo mana amekushirikisha kuna wengine wanakopa kimya kimya na wanawapa wanawowafanyia masagi kimya kimya!
Kama huu ndio upendo bora[emoji23][emoji23][emoji23], basi nimeamini ndoa kwamiaka tuliyofikia sasa hatuziitaji. Boss unajua kujitoa kumjenga mtu maana mimi ilinitokea na tuliachana. Basi heri nusu shari kulilo shari kamili. Wanawake waache kulazimisha ndoa maana majukumu hawayawezi. Kwakuwa sitaki kuumia hivyo sitaki kuumizwa basi ndoa sijawabu sahihi kwakijana wakizazi cha sasa.
 
Si bora huyo anajenga kwao! Kuna mwenzake huku anakopa benki anaporomosha mahekalu huko alikoolewa kwenye uiwanja vya mume wake. Watu washaongea wamechoka yeye anajitetea eti anajenga kwa ajili ya watoto.

Inafika muda akipokea mshahara unakaa siku 10 hana mia. Ashukuru kazini anaenda kwa mguu tu sio mbali na anakaa kwenye nyumba za sirikali.
 
Mbona mm sijaona tatizo jamani. Kwa maelezo yake nadhan mkewe anatumia pesa yake ama
 
Mwache ajenge kwao wanawake wapo hivyo hela yake ni yake yako ni yake!
 
Back
Top Bottom