Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kosa la mke wako ni kukwambia matumizi ya pesa yake. Wazazi wake wamemsomesha uliwakopesha? Kwanini na yeye ashindwe kujenga kwao
Ingekuwa heri mwanaume na hasioe!! Lakini kwa ajili ya kuwaka tamaa miili yenu basi mwanaume na aoe mke mmoja! Pigia mstari INGEKUWA HERI ASIOE. Sio maneno yangu ni ya Mtume Paulo kwa Wakolintho.Pole mkuu, nakushauri tu muache mkeo ajenge kwao! Na wewe Jenga kwako! Mwanaume hudumia familia yako kwa kuhakikisha wanaishi pahala pazuri na panapofaa!
Acha na hela ya mkeo maana SIYO YAKO
Mimi nilikopa fedha nikajazia ujenzi wa nyumba anayojenga mume wangu maana ni familia moja, matokeo yake amekuja kunitemgenezea maneno ya kashfa machafu yasiyo faa!
Mkopo ukiisha, nachukua mwingine na NITAJENGA KWETU ili siku tukiachana niende kwetu kwa raha! Wanaume mna matatizo sana ACHA MKEO AJENGE KWAO, wewe Jenga KWAKO.
Sent from my Infinix X683 using JamiiForums mobile app
Sasa hao yatima wako wangapi ukili.ganisha na idadi ya vijana wanaotaka kuoa?Jana mtu kaja na code mpya hapa JF kuwa oweni YATIMA ..mtamshukuru baadae
Duuh aisee ni hatari sanaWewe unaGombana na mkeo kwa jambo la kijinga sana,unataka asijenge kwao!? Ishini na wake zenu kwa akili,mimi mke wangu juzi kakopa milioni 10 akaenda kukarabati nyumbani kwao ilikhali sisi tuko katika nyumba ya kupanga.
Pigia mstari neno ishini nao kwa akili.
Hakuna mwanamke anaweza kopa milioni 47 eti akajengwe kwa wazazi wake, hiyo haipo. Ni nyumba yake hiyoNyumba anayojenga ni yake yeye, hayo maneno ulioambiwa ni ujanja tu wa kuweka uhalali kinachofanyika.
Wanawake si watu wa kutegemea, mara zote hufikiria kuwa na maisha mengine nje ya maisha ya ndoa
Mkuu umeamua umwambie ukweliii mtupuuuHakuna mwanamke anaweza kopa milioni 47 eti akajengwe kwa wazazi wake, hiyo haipo. Ni nyumba yake hiyo
Sio kwa mwanamke tu, kamwe usiwe na expectations kwa binadamu yeyote, utaishia kuwa disappointedNa ukianza kuishi bila ku expect kitu toka kwa mwanamke unaimarika sana
Daa! Pole sana baba ester,,,mama ester anachokifanya sio kizuri ila saiz hapa wameshusha mchanga nahis wanataka kuweka marumaruIko hivi wife na mimi tulifahamiana Kijijini. Nilikuwa F6 yeye akiwa F4 leaver. Nilimsaidia akapata Chuo cha Takwimu akaenda akafanya akapata cheti. Wakati akiwa chuo tulioana, mimi nilikuwa nafanya kazi. Miaka mitatu baadae tulijaaliwa watoto wazuri.
Maisha yaliendelea nikiwa kazini na yeye akiwa ofisi moja masuala ya takwimu nchini. Mambo ya ndoa yalikuwa safi sana nili enjoy ndoa labda kwa sababu ilikuwa ya kusafiria. Maana yeye mkoa mimi mkoani. Nilifanikiwa kumuhamishia mkoani kwangu yeye na watoto. Tuliishi vizuri kwa wastani wa miaka 5.
Baadae Mama yake akapitia wakati mgumu, tukashauriana tumjengee kibanda. Kwa kuwa wapo watoto wakubwa wakaona washirikiane wote. Kwa kuwa wife ndiye mwenye kipato kizuri akakopa Benki Milioni 27 lakini nyumba haikuisha.
Kero ikaanza sasa. Kila wakati anataka pesa ya Ujenzi kwa Mama Mkwe. Majuzi alipata bingo Ofisini kwao (Milioni 20) ni pesa ya offer ya Serikali yenye riba kidogo. Lahaulaaa!! Si akaipeleka yote kwenye ule ujenzi.
Wana JF wenzangu, kumbuka si kwamba sisi na Watoto wetu hatuna mahitaji, hapa ada, nyumba haijaisha asilimia Mia. Why apeleke Milioni 20 kwao? Hivi? Hajui ile nyumba hawataishi watoto wake? Ndani ni kuchuniana.
Najuta sana kuoa mwanamke huyu.
Si bora huyo anajenga kwao! Kuna mwenzake huku anakopa benki anaporomosha mahekalu huko alikoolewa kwenye uiwanja vya mume wake. Watu washaongea wamechoka yeye anajitetea eti anajenga kwa ajili ya watoto.
Inafika muda akipokea mshahara unakaa siku 10 hana mia. Ashukuru kazini anaenda kwa mguu tu sio mbali na anakaa kwenye nyumba za sirikali.
Nilidhani ulisema mliamua kumjengea mama mkwe kibanda? Kibanda gani hicho kilichogharimu mil 27 na hakijakamilika na kinahitaji another 20 mil? Na kama mkeo alikopa mil 27 hao ndugu zake wamechangia kiasi gani? Una hakika wanajenga kibanda kweli?Iko hivi wife na mimi tulifahamiana Kijijini. Nilikuwa F6 yeye akiwa F4 leaver. Nilimsaidia akapata Chuo cha Takwimu akaenda akafanya akapata cheti. Wakati akiwa chuo tulioana, mimi nilikuwa nafanya kazi. Miaka mitatu baadae tulijaaliwa watoto wazuri.
Maisha yaliendelea nikiwa kazini na yeye akiwa ofisi moja masuala ya takwimu nchini. Mambo ya ndoa yalikuwa safi sana nili enjoy ndoa labda kwa sababu ilikuwa ya kusafiria. Maana yeye mkoa mimi mkoani. Nilifanikiwa kumuhamishia mkoani kwangu yeye na watoto. Tuliishi vizuri kwa wastani wa miaka 5.
Baadae Mama yake akapitia wakati mgumu, tukashauriana tumjengee kibanda. Kwa kuwa wapo watoto wakubwa wakaona washirikiane wote. Kwa kuwa wife ndiye mwenye kipato kizuri akakopa Benki Milioni 27 lakini nyumba haikuisha.
Kero ikaanza sasa. Kila wakati anataka pesa ya Ujenzi kwa Mama Mkwe. Majuzi alipata bingo Ofisini kwao (Milioni 20) ni pesa ya offer ya Serikali yenye riba kidogo. Lahaulaaa!! Si akaipeleka yote kwenye ule ujenzi.
Wana JF wenzangu, kumbuka si kwamba sisi na Watoto wetu hatuna mahitaji, hapa ada, nyumba haijaisha asilimia Mia. Why apeleke Milioni 20 kwao? Hivi? Hajui ile nyumba hawataishi watoto wake? Ndani ni kuchuniana.
Najuta sana kuoa mwanamke huyu.
Mwache mkeo aheshimishe kwao. Kwasababu hata wewe mwanaume lazima ujenge kwenu. Utazikwa wapi? Na yeye asipoendeleza kwao familia yake itamwonaje. Msingi ni kwamba asiiosahau familia yake ya sasa.Mkuu kwa point hii, basi kila mtu aliepo kwenye ndoa ajenge kwao na hizo mali zisihesabiwe kma za familia (ndoa), basi kulikuwa hakuna maana ya ndoa maana hapo ndoa ipo kwaajili ya kuzalishana au kufanya mapenzi tu. Na mbaya sheria ya ndoa uwa vyote vilivyovunwa ndani ya ndoa ni vyenu wote hata kma ni mwanaume ulifanya hvyo. It’s not fair, hata mm nilisomeshwa na wazazi kama yy alivyosomeshwa.
OkayWewe unaGombana na mkeo kwa jambo la kijinga sana,unataka asijenge kwao!? Ishini na wake zenu kwa akili,mimi mke wangu juzi kakopa milioni 10 akaenda kukarabati nyumbani kwao ilikhali sisi tuko katika nyumba ya kupanga.
Pigia mstari neno ishini nao kwa akili.
Mwanaume ndiyo anatakiwa kuendeleza kwao na siyo mwanamke, Kaka zake ndiyo wanatakiwa kuendeleza kwao , yeye anatakiwa kuwatunza wazazi wake, Mtoto wa kike akiolewa anaondoka kwao na kujiunga kwenye familia ya Mwanaume we kwa akili yako huyo mke wake alifariki leo unafikiri watoto wake wata rithi sehemu ya mali za Mama yao alizo wekeza kwao?Mwache mkeo aheshimishe kwao. Kwasababu hata wewe mwanaume lazima ujenge kwenu. Utazikwa wapi? Na yeye asipoendeleza kwao familia yake itamwonaje. Msingi ni kwamba asiiosahau familia yake ya sasa.