Nina miaka 45, nimeshafungua maduka 11 sasa nimefilisika

Pole brother muombe sana mungu
 
Ulishawahi kufanya biashara japo yakuuza karanga?Kwa namna ulivyoandika sidhani kama unauzoefu wa biashara yoyote.
Wakati mwingine bora unyamaze ujifunze kwa wengine
 
Ahsante mkuu
Mkuu Pole na napenda nikuambie haya.

Mungu ni mwenye Rehema.
Usijihesabu mkosaji mbele za Mungu ikiwa unatambua makosa uliyotenda na kukiri mbele zake toka moyoni, anasamehe. Umeshasamehewa. Jisamehe mwenyewe pia na usamehe waliokukosea. Usihukumu wengine.

Usihusishe Uchawi kwenye biashara.
Ikiwa ulitumia ushirikina katika biashara zako mafanikio uliyopata yasingekuwa ya kudumu. Shetani hukuvuta akishakumiliki anakupiga. Atakupa mafanikio ya muda kisha anakugeuka. Lakini Mungu ni mwema rejea kwake uanze upya.

Kushindwa usimamizi wa biashara.
Biashara kuwa nyingi hivyo kukosa usimamizi wa mapato na shughuli zako.

Hofu na mashaka.
Hii ni karakana ya shetani inayochakata na kuharibu mambo ya watu wengi. Hofu na mashaka ya mambo usiyoyajua na hayapo. Hapa humtegemei Mungu unategemea akili zako mwenyewe. Hii karakana imeleta majanga na vilio kwa wengi kwani ukishakuwa na hofu tayari umeshafilisika hata kabla ya kufilisika kiuhalisia. Hapa ndipo hasa wewe ndugu ulipoangukia.

Mahusiano mabaya ndani ya ndoa.
Kukosa mahusiano mazuri kwenye ndoa ni janga lingine shetani amewekeza kuharibu maendeleo na ustawi wa kazi zetu. Ukiondoka nyumbani unasononeko na kuwaza naenda kutafuta kwa ajili ya nini sasa hupati na hata ulicho nacho kinaondoka kwani haukihitaji. Hapa kuna siri kubwa shetani kawekeza.

Ni mengi ndugu ila hapo napiga kuzunguka kichaka kama nimekugusa sema hapo hapo. Ila ikiwa tunaongea ana kwa ana kupata mtiririko wewe mwenyewe utajua umeangukia wapi.

Lakini pia ikiwa kuna watu wanaanza kutoka zero na kuwa matajiri, iweje wewe mwenye uzoefu na biashara uanze kujikabidhi kwa shetani katika mfumo wa kufilisika? La! hasha. Ondoa hilo kichwani, hauna cha kupoteza, kataa shetani, chagua mafanikio na Mungu.
 
Mkuu sikuweza kuweka kumbukumbu izo kipindi hiki cha mwisho wa kufilisika lakin nina historia nzuri tangu nianze biashara mwaka 94 mpaka nilipofilisika mwaka 2016
Hili ndio chanzo cha yote yaliokufika...muwe munaendesha biashara kwa kufata principle za biashara kwa kutfuta mtu mwenye elimu ya uhasibu akusaidie.
 
acha kumdanganya mwenzako isee .. biashara ni mipango na kusimamia hiyo mipango kwa umakini kama hakufanya hivyo au ata wewe hautafanya hivyo utafilisika tu.
 
Mi nadhani hata utitiri wa ofisi nyingi umekukwamisha.

Kikawaida ukishaona mambo yameyumba,
Unatakiwa baadhi ya branch uzisimamishe mpka utakapokaa sawa.

Hapo mi nadhan Ni hesabu TU ya mapato vs matumizi ilikuangusha
 
Hukusoma vizuri mwenendo wa biashara yako. ulitakiwa ubadilishe mapema biashara au kuongeza huduma nyingine mfano kutoka kuuza simu na vifaa vyake na utoe huduma za kifedha kupitia simu, uza vocha au utengeneze simu hata kwa kumlipa fundi akae hapo. Inafika wakati kila mmoja anamiliki simu je hapo utafanya kweli biashara?
 
acha kumdanganya mwenzako isee .. biashara ni mipango na kusimamia hiyo mipango kwa umakini kama hakufanya hivyo au ata wewe hautafanya hivyo utafilisika tu.
Na hapo ndo unapozidi kupotea. Unapojifanya ww ni bingwa wa fikra na mipango. Mwisho wa siku unajikuta umepoteza kila kitu. Kwa kosa la kumsahau na kumtanguliza mungu kwanza.... Angalia Marekani pexa yao inaongoza ulimwengu mzima ( Soma meneno yalioandikwa ndani ya us $)
 
Unajua ni Mungu gani wanaye muamini..
Au wewe ukisikia Mungu tu unaweweseka.
-Mungu wao anaruhusu ushoga na usagaji.
-mungu wao anaruhusu mapenzi hadharani na Wala hakuna shida.
-mungu wao anaruhusu uasi na n.k

Siku nyingine dokie kabla ya praise tu..
 
Je kwa upande wako ww binafsi umemuani mungu gani ?
 
Ulishawahi kufanya biashara japo yakuuza karanga?Kwa namna ulivyoandika sidhani kama unauzoefu wa biashara yoyote.
Wakati mwingine bora unyamaze ujifunze kwa wengine
Nilipokua miaka 9 niliuza biashara ya njugu miwa na mahindi mpaka nimefika miaka 15 nikafungua duka
 
Mkuu biashara ya simu mpaka leo inalipa kwa mfano simu jumla 15000 unauza 20000

Simu jumla 150000 unauza 160000

Mtaji wa milioni 10 unaweza kuuza hata pc 10 au 15 kwa siku

Biashara iliopo kariakoo
 
Kwa nilichojifunza kwenye biashara izi kipindi biashara imekunyookea jaribu kuwaza biashara mpya au uwekezaji mpya wengi waljofanya ivyoo wamesavaivu sana pindi biashara zikiyumba au kufilisika mf Una maduka na biashara imechangaya embu wekeza kwenye hisa au mashamba au mifugoo usiwekeze tena kwenye Duka au Una mifugo na Duka embu wekeza tena kwenye nyumba za kupangisha au udalali kubadili uelekeo WA shughuli zako unasaidia sna niliona Kwa mjimba wangu alikuwa na Duka kama 3 apo buguruni za mbao na hardware Ila vilipotea kama utani kilichomsaidia ni mashamba na mifugoo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…