Nina miaka 45, nimeshafungua maduka 11 sasa nimefilisika

Kama ulikuwa auhongi au kutumia pombe lazima ufilisike
 
Kitaalam tunaita portfolio diversification.
 
Yaani makosa ninayoyaona hapo ni mengi mno, yaani natamani nikukalishe chini nikupe somo la biashara. Lakini pole tumia muda huu kutafakari ulipoanguka, fanya hivi
1.chukua kalamu na daftari anza kuandika kila kosa unalofikiri ulilifanya kwenye biashara yako mpaka ukafilisika alafu kwa kila kosa andika suluhisho lake ni lipi.... usijaribu kuanza upya bila kujua ulipokosea na utatuzi wake la sivyo utaanguka tena.
2. Kumbuka mara ya kwanza kabisa ulipoanza biashara ulianza vipi mpaka ukaweza kutoka.
3. Sasa angalia ni biashara gani ukiifanya sasa hivi itakusaidia hata kama ni ya mtaji mdogo. Anza nayo tena.
4. Usihof kuhusu swala la umri miaka 45 ni mdogo sana hasa kwa sisi waafrika. Namfahamu mtu ambaye ana miaka 67 na bado anafungua biashara mpya kila siku.
5. Anza upya ila angalia usirudie makosa
 
Amin
 
Maduka 11 with same line of products? Anyways 2016-2020 wafanyabiashara wengi walipitia changamoto sana. Mabadiliko ya kisiasa, covid, sera za fedha.
 
Awamu ile tulifilisika kwa nguvu, awamu hii ni automatically unajikuta nje ya mfumo, nasubri ushauri na mimi
Awamu ile nilisema ngoja nijaribu biashara. nikafungua duka la kawaida la jumla lilifilisika kabisa na kuniachia baadhi ya madeni.
Baadae niligundua kosa kubwa ilikua sina rekodi nzuri ya mwenendo wa biashara, sina kumbukumbu ya matumizi na mapato, nilikua nachanganya hela yangu na ya biashara, nilikua sifuatilii vizuri benki nimetoa nini na nimebakisha nini na mwisho nilikua na matumizi binafsi yasiozingatia bajeti wala ukubwa wa biashara. kwa ufupi kwa mtazamo wangu nilifilisi biashara yangu kwa (Poor management of my business)
 
Kama ulifilisika 2016 kipindi cha kuanza upya ni sasa...nakushauri yafuatayo....
1.Badili Marafiki kabisa...
2.Usiongee Mambo yako kabisa kwa mtu hata ndugu yako
3.Biashara ya simu imebadilika kidogo tafuta mtaji tafuta simu used za Dubai...uza kwa oda na uzia wateja waKo..
4.Naamini ulikua na asset uza moja iwe mtaji...


Pole ila Pambana mm utawala 2016-2021 march hali ilikua mbaya ila nimekaza kuna hatua nimepiga...
 
mimi naomba kazi ya Shop Manager. Hayo maduka yatainuka tena kwa kasi ya ajabu.
 
Mkuu sikuweza kuweka kumbukumbu izo kipindi hiki cha mwisho wa kufilisika lakin nina historia nzuri tangu nianze biashara mwaka 94 mpaka nilipofilisika mwaka 2016
Ulikuwa unafanya biashara gani kwenye hayo maduka yako na kuanzia 1994 hadi 2016 ulikuwa ukijihusisha na biashara gani na wapi? Kwa kujua hayo machache, naweza kujua wapi nianzie kwa ajili ya kukupa ushauri wangu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…