Nina milioni 25, naweza kuwekeza kwenye nini ili nipate pesa nzuri kwa muda mfupi?

Nina milioni 25, naweza kuwekeza kwenye nini ili nipate pesa nzuri kwa muda mfupi?

Chukua milioni tano au kumi, kwa milioni kumi unapata eka 50 kwa kila eka laki mbili mbili.

Kila eka utatumia 30 au 50 kulima.
tafuta mbegu nzuri ya mihogo, uzuri wa kilimo cha mihogo mizizi ikishashika tu basi ata Kama kuna uhaba wa mvua itastahimili.

Kuvuna ukiuzia shambani kila eka haukosi milioni moja na laki tatu, apo unakua umemuuzia dalali shambani, ukiwa na soko lako faida kubwa zaidi.

Ukivuna Mara moja tu ela yako itakua imerudi, na faida kubwa umepata, Shamba ni lako kila mwaka utaendelea kulima.utanishukuru badae
n.b ukiitaji Shamba nicheki 0693786080
 
Kama huna wazo la biashara na ungependa hela yako iku3 fanya biashara ya kukopesha kwa riba, Kwa mtaji huo 25M utakua unakusanya 5K kwa siku, hivyo kwa mwezi moja unaingia 15M na mtaji wako uko vil3 vil3, Cha msingi ufuate taratibu za kufanya biashara ya fedha.
 
What i can say ni kwamba, Pesa nzuri hutaipata kwa muda mfupi, otherwise ufanye biashara Haramu...

Pesa nzuri zinahitaji mipangilio mizuri, kutokata tamaa, uvumilivu na kujipanga sio shortcut za chapchap.
The best advice

Nimewahi kupoteza 17 Million kwenye kilimo kwa sababu ya kukurupuka - niliambiwa ufuta na mpunga vinalipa sana basi nikasema ngoja nitumie principle of diversification 8.5M niweke kwenye mpunga na 8.5M nyingine niweke kwenye ufuta Kondoa kilichotokea pesa iliyorudi kutoka kwenye mauzo hata milioni tano haikuzidi kwa vyote (mpunga + ufuta) ni mambo ya ajabu sana yanaendelea kama hutafuatilia miradi yako wewe mwenyewe tena kwa ukaribu na unaweza ukawa unafuatilia kwa ukaribu lakini kama huna utaalamu basic wa kitu pia nirahisi sana kupoteza pesa yote - kumbuka ufuta nililima ekari 50 na mpunga ekari 25 na nilienda kukagua mimi mwenyewe lakini matokeo yalikuwa kama hivyo maana najua ntaambiwa kilikuwa ni kilimo cha whatsapp

So kwa mleta mada milioni 25 ni pesa inayoweza kukufanya ukapiga hatua lakini pia kupotea ni dakika mbili tu inabidi uwe makini sana

Ushauri wangu

Katika pita pita zangu nimegundua kama vijana mkiungana especially wenye maono yanayofanana mnaweza kufika mbali kama utakuwa na rafiki mzuri ( wa kibishara maana uwana nao ukizidi hakuna kitakachoendelea) mnaweza kuingia ubia na kufungua microfinance mnaisajili vizuri na kufuata taratibu zote za ki mamlaka mnaweka zenu 10 Milioni na yeye anaweka mnakuwa na 20 Milioni yenu mnaanza kuizungusha kwa riba nafuu bila kuwa na tamaa na kuhujumu au kuonea watu....Milioni 15 nyingine unajiwekea akiba maana hakuna guarantee pia kwamba lazima upate faida kwenye microfinance ila with proper nurturing ni business inayolipa sana ..na wateja mnaweza anza na watu hata watano au kumi mnao waamini (wapo mtaani) japo pia wapigaji ni wengi sana...ila baada ya miaka mitatu kama mnaenda na principle zenu nzuri za kibiashara na kibenki ...utarudi hapa kunipa mrejesho

Ukiweza pia kufanya peke ako Microfinance ni wewe tu ila fuata taratibu na ukubali kukua kidogo kidogo

Uwe na siku njema
 
Wekeza kwenye spare za magari. Anza na zile ndogondogo zinazohitajika wakati wa service za magari....sparkplugs, air and oil filters, oils, coolant....mdogo mdogo utaanza kuongeza heavy spare parts.....oil filter kwa mfano ya toyota maduka ya jumla utanunua kwa bei isiyozidi sh 4000. Rejareja utauza kwa sh 10,000
Mkuu wawezA nipa mchanganuo ama ukawà mshauri kwa biashara hii mkuu.inaonekana kama una wazo
 
Nina milioni 25, naweza wekeza kwenye nini ili nipate pesa nzuri kwa muda mfupi?

Wadau mawazo yenu Tafadhali.

Mchango wa mdau


Pia soma: Biashara gani zinazoingiza mamilioni kwa muda mfupi?
Njoo tufanye biashara ya pamoja, nafaka na Dagaa,...wewe usihangaike na usimamizi...wewe leta pesa yako tu Mimi nitafanya kila kitu,...,nitakuwa nakupa 7% kila mwezi,kama faida ya mtaji utakaoweka kwenye biashara.Iwe hiyo million 25, mill 10,au zaidi...yaan kiasi chochote cha mtaji utakaoweka ,nitakupa hiyo faida kwa mwezi.

Tunafata taratibu zote za kulinda pesa yako isipotee...,kama kuandikishana mikataba ya kisheria ili kila mtu awe na uhakika na pesa yake.

Zaidi sana biashara inahitaji uthubutu,uzoefu,maarifa, kujitoa,uvumilivu na uaminifu Wa kiwango cha PhD.,njoo inbox au tuwasiliane +255716060677.
 
Ndugu yangu aliuza nyumba ya urithi Mikocheni, akaenda kununua nyumba Sinza, akafungua studio ya kurekodi muziki, Hadi leo sijawahi kusikia redioni wimbo kutoka studio yake, sijui zinapigwa kwenye space station anga za mbali?!?!¿‽‽🤔🤔🤔
Nyimbo zake ziko Netflix huko, siyo huko mikito na modundo.com😀😀
 
Wekeza kidogo (sio mzigo wote) kwenye biashara ya magari (kulenga)!

Ni fani imevamiwa sana ila ukimpata mzoefu, maisha yatasonga!
 
Chukua 10 zungusha 15 kanunue bond ama fixed account itakulipa. Hiyo kumi fanya biashara ya kuuza nafaka. Ukicheza na 25 ambayo naamini ni ya mirathi ya mzee wako laana itakuwa katika paji la uso wako.

Hiyo pesa mmeuza nyumba mpo wanne mmekula 25 each. Ndugu kama unaweza wekeza kwenye real estate ya Chamazi 15M unajenga nyumba unauza 55M. Zaidi ya hapo italia ni pesa ndogo sana hiyo.
Mtu mwenye uwezo wa kuw ana milioni 25 hawezi kusema hana namna ya kuitumia. Unless kauza mashamba ya babu huko Segera tanga.
 
Kama huna wazo la biashara na ungependa hela yako iku3 fanya biashara ya kukopesha kwa riba, Kwa mtaji huo 25M utakua unakusanya 5K kwa siku, hivyo kwa mwezi moja unaingia 15M na mtaji wako uko vil3 vil3, Cha msingi ufuate taratibu za kufanya biashara ya fedha.

Hebu elezea hii Mkuu kwa kirefu nikuelewe, mimi nafanya kwa mwezi Mungu ni mwema si haba inalipa ila nataka nijitanue zaidi.
 
Back
Top Bottom