Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Nyumba utaijenga kwa Tshs 70Mil, na kupangisha kwa labda Tshs laki 7 kwa mwezi. So itachukua miezi (Tshs 70Mil/Laki 7) = Miezi 100 (miaka 8) kurudisha hela.Ekeza katika kununua nyumba na uzipangishe
Ni lazima itakuhusisha usafiri nchi za wengine hasa asia fika kwenye viwanja vya ndege na ukiwa na hati ya kusafiria ya TZ acha utakavyo ambiwa vua nguo zote na kubinuliwa kila upande hayo ndio matatiozo yake makubwa.Mkuu biashara ya sembe inatatizo gani?
Nyumba utaijenga kwa Tshs 70Mil, na kupangisha kwa labda Tshs laki 7 kwa mwezi. So itachukua miezi (Tshs 70Mil/Laki 7) = Miezi 100 (miaka 8) kurudisha hela.
We bana ingia kwenye Kilimo kama vipi. Nunua mashamba au hata kodisha mashamba na ulime. mazao kama Mpunga na Ufuta yanalipa sana. Ufuta ukiuzia shambani ni Tshs 2,500/= kwa Kilo, na ukiuzia kwa wachina au wahindi wa kurasini ni Tshs 4,000/= kwa kg. Heka moja yaweza kutoa mpaka magunia 8 au 10, so utakua na hela yako ndefu tu.
Halafu hela kama hizo usizifanyie pupa. Kama ni hela "umepiga" mahali (sorry kama sio) hua zinakuaga na mzuka sana, but kama umezichanga kidogo kidogo utakua umezizoea, so zisikupe presha sana. Ukitulia unaweza ukazizalisha sana.
Otherwise angalia pia na sisi wanaume, wengine ukitupata tuta-act kama "mario", then hela zikaisha.
Ni hayo tu.
Mbona unajicontradict, Si umesema hujui kufanya biashara?
Swali lako liko kinadharia zaidi kwa sababu jibu lake ni rahisi tu: fanya vilevile ulivyofanya ukapata hizo mil. 270,just do it again and again, it seems to be working quite well...
Unaweza kufungua kituo cha mafuta,Tank 3 kama 150m, moja ya diesel, nyingine ya mafuta ya taa na nyingine ya petrol.
pump 3 kama 18m. Jenga Jengo dogo la kiushikaji kama ofisi, nunua sehemu kando ya barabara unaweza tumia kama 20M na 30m kujenga jengo dogo la kiushikaji kwa ajili ya ofisi.Kopa kama 200m nyingine anzia hapo.
Ni lazima itakuhusisha usafiri nchi za wengine hasa asia fika kwenye viwanja vya ndege na ukiwa na hati ya kusafiria ya TZ acha utakavyo ambiwa vua nguo zote na kubinuliwa kila upande hayo ndio matatiozo yake makubwa.
kaka vp? Yaan milioni 270 tu unauliza kua nimezipataje?....hahaha kwel Tz bado saana,,...mbona pesa ya kawaida sana? Na wenye kumiliki Mabilioni nao watasemaje?..,,,au huo ndo urithi wa mawazo uloachiwa na babu yako Nyerere?? ok nna nyumba kadhaa nimerent wazungu kwa dollars maeneo ya mbez na msasan,,...na mbal na hapo nna v mpesa,,...tigopesa na maduka kadhaa mjini,,...ni ayo tu kwa ufupi hope umenielewa
Huku tuendaka hatutaki biashara wala mambo kufanywa kiushikaji! Madhara yatokanayo na mambo kufanywa kiushikaji na bila kuzingatia safety issues yametosha sasa. Kama mtu unataka kufanya biashara au shughuli yoyote ni lazima uzingatie kanuni na sheria zilizopo ikiwa ni pamoja nakutokuleta madhara kwa watumiaji au mazingira yanayokuzunguka.
Mpe ushauri utakaozingatia haya!
thinka,,....ahsante kwa mawazo yako
Japokuwa umeonyesha chembe ya dhihaka lakini sitosita kukushauri,
Kulingana na maelezo yako ya awali yanaonyesha wazi kuwa pesa hiyo kwako ndio pesa nyingi zaidi uliyowahi kuishika na mazingira ya upataji yalitia shaka kidogo uwezo wakowakuimiliki,
Vema, ushauri wangu nikuwa, endelea kuwekeza hapo kwenye biashara ya nyumba na upangishaji, vilevile biashara ya M-Pesa nk,
Ukitoka nje ya hapo siamini kama utafanikiwa,
Kwa mtanzania wa kawaida milioni 270 ni pesa nyingi sana, usishangae ndugu!
Mungu akutangulie,
umetoa ushauri mzuri sana, haki tena hata mm ningemshauri ivyo.biashara ni kutoka moyoni,wala cyo kushauliwa.big up kwa ushauri wako mzuri.wengi huwa hata Mimi wananiuliza swali km hilo.na jibu langu ni km ulo mpa huyo Dada.w/end njema.Quick and simple advice mdogo wangu, chukua pesa yako kafungue fixed account endelea kupiga kazi mpaka pale utakapokuwa tayari kufanya biashara. Au kanunue fixed asset kama nyumba tena nakusistizia siyo kiwanja. Nasema hivyo sababu ya hizi sentensi zako mbili "Binafsi ambayo nafikiria nii ingize kwenye Biashara huku nikiwa naendelea kupiga kazi kama kawaida,,...!!
Sasa naombeni mnishauri nifanye biashara gani ambayo itamudu kiasi icho cha pesa na kunii ingizia faida"
Lakini pia kumbuka biashara inahitaji hashiki, shauku na matamanio ya kile kitu unachokwenda kufanya ili hata pale utakapoangua hivi vitu vitatu vitakushawishi uamke na ujipanguse na kuanza tena vita upya. Pia inataka kujitoa lakini usipokuwa makini hiyo 270 milioni utazitia mtaroni mdogo wangu halafu utajuta. Mwisho, huu ushauri wangu utakuwa hauna maana kwenye biashara yoyote ile kama wewe mwenyewe hauna shauku navyo hivyo vitu vine nilivyosisitizia hapo juu. Mshauri wa biashara atakushauri jinsi ya kufanya biashara lakini si aina gani ya kuafanya hii yote sababu biashara inaanzia moyoni mdogo wangu.