Nina milioni tano, naweza pata kiwanja upande huu wa Dar es Salaam?

Nina milioni tano, naweza pata kiwanja upande huu wa Dar es Salaam?

Unapata nenda madale ndani ndani unapata 20 kwa 25 kwa 3m ila uwah kukijengea ukuta kuna wavamizi kibao utakuta kimeuziwa mwingine au kimechukuliwa

Nimenunua hapo ekari moja kwa bei chee sana
Mbopo ???
 
Unanunua kiwanja una mil 5, utajenga na nn au utaweka tent uishi humo?
Hatua moja huanzisha nyingine....me pia nimenunua viwanja na mashamba maeneo mbali mbali na bado sijaanza kujenga ila nimepanda miti na huwa nna kawaida ya kufanya site visit kila baada ya mwezi au miezi miwili na kila nlipo chukua kiwanja au shamba kuna wenyeji wangu wanaokua wananisaidia kufanya usaf na kunyeshea ...

So hata km huna hela ya kuanza kujenga isikuzuie ukashindwa kununua kiwanja ...kumbuka ardhi inapanda thamani kila siku

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa dar es salaam ...Maeneo yaliyobakia ambayo unaweza pata kiwanja kwa bei nzuri ni
Kigamboni
Chanika ndanindani
Mbande ndanindani

Ndo maana makampuni mengi ya Real Estate yamekimbilia Kigamboni ....Naitabiria kigamboni after 5years kuna uwezekano viwanja vikawa vinauzwa kwa bei ghali sana km ilivo Goba sahv


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Heka? Au unamaanisha ekari? Maana hilo neno kwenye vipimo vya hesabu haliko kabisa! Labda kama unamaanisha hekta ambayo ni sawa na ekari mbili na nusu!
Wengi wakisema Heka wanamaanisha Acres ambayo ndo hzo 4000+ sq wengi hawajui kuna ukubwa ambao ni Hecta ambao ni 10000sq

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mipeko ninachofikiria futi 40 kwa 100 tambarare mbele Kuna nguzo ya umeme na mpira wa kuunga maji call 0653057919
 
Mfukoni (actually ni kwenye account ya TigoPesa) nina milioni tano taslimu.

Natafuta kiwanja upande wa kuanzia Ubungo kwenda Goba, Salasala, Tegeta, Madale, hadi Bunju.

Lakin pia Ubungo kwenda Kimara pande zote, Mbezi huko msakuzi, hadi kibamba, Kiluvya.

Kifupi tu nalenga maeneo ambayo ni rahisi kuja na kurudi Ubungo.

Naweza kupata wakuu, kwa bajeti yangu na maeneo nilotaja?
Boko Magereza kumekucha huko utapata, ukisogea Kinondo kwa Ridhiwani pale unang'oa eneo kubwa tu
 
Back
Top Bottom