Nina msongo wa mawazo, maisha hayana maana kwangu, msaada wa mawazo

Wakiitwa walio gizani wewe haumo. Acha kudanganya watu hapa.
Una kazi, una mke hadi ulishawahi kuwa na gari??? Huyo mungu ni wakwako peke yako?

Kama nakupata hivi.

Kuna siku nilisema.
Tushukuru kwa Mungu wetu. Sio kwa sababu ya leo. Ila kwasababu ya jana yetu, Mungu alitupa chakula maji nguvu na uhai. tumekosa leo ila tushukuru kwa jana. Na kutegemea kuwa kesho tutakuwa na Neema zaid ya leo.

Amein.
 
Kutoa sadaka ni jambo jema lakini kuna hatari ya kutoa sadaka kama hongo.
Huyo jamaa alipokuambia kwamba aliinenea sadaka ungemuuliza imeandikwa wapi kwamba unapotoa sadaka unatakiwa uinenee? Yesu anasema "yoyote mtakayoyaomba katika sala mkiamini, mtapokea."(Mathayo 21:21-22). Hajasema yoyote mtakayonena wakati wa kutoa sadaka mtapewa. Kama huyo alitoa akafanikiwa huo sio ushahidi kwamba ukiinenea sadaka unapata unachokitaka. Mungu huwanyeshea mvua wema na waovu. Be careful, hizi ni nyakati za mwisho. Kuna mafundisho ya mashetani(1 Timotheo 4:1) na pia kuna manabii wa uongo wanaofanya ishara za kuwapoteza yamkini hata wateule(Mathayo 24:24).
Hilo wanao fanya kunenea kwenye sadaka ni ushirikina hamna Umuungu ndani yake.....African yuna shida kubwa.
 
Amina Mtumishi wa Mungu Setfree ,

naambiwa kuna roho za uharibifu zinatakiwa kuvunjwa, kw madhabahu yenye nguvu
 
Siku hizi naona unaitangaza injili bwashee🤣

W nakujibu Honest kabis kwasababu ni ndugi yangu.
Sijielewi aisee.
Ila Najikuta tu huku kwa Dini. Labda sababu nina 35+ , na sina shauku kwenye mapenzi, na pia sina hamasa kwenye Siasa. Na Niko kwenye kazi na ujasiriamali.
Sasa naona bora nitoe niliyonayo kuhusu Dini na habar nyingne mchanganyiko.

Ukitoa Siasa. Mada nying naona ni za Vijana zaid. Ila ambazo nikiona naweza toa mawazo yangu. Nina chop in.
 
Ni mwaka wa tatu sasa tangu niamue kabisa kuacha uzinzi na pombe na kuamua kutulia na mke wangu tu.

wakati wote nimejitahidi kuishi kwa kufuata neno la Mungu pamoja na kusali sana.

Nimezingatia kufunga, kutoa sadaka, zaka na michango mbalimbali.

Mwaka jana mwezi Agosti niliweza kununua tena kausafiri kazuri ka kutembelea,

sambamba na kuanzisha mradi wa kilimo cha bustAni kubwa.

mwezi wa pili mwaka huu, Mrs alipata changamoto kazini, iliyopelekea kuhamishwa kituo, hivyo nilijikuta nauza gari ili kulipa madeni ambayo tulikuwa tumejikopesha.

nimeendelea na kilimo lkn hadi sasa mtaji umeisha, sina namna ya kuweza kuendelea na mradi.

hivyo nimepoteza Gari yangu na mtaji wa mradi ambavyo nilifanikiwa kuvipata baada ta maisha ya wokovu wangu,

ikumbukwe huko nyuma nishaanzisha miradi mingi na ikafa,

Mbali na hayo mimi ni mwajiriwa, lkn nimekwama kbs kiutumishi,

nina miaka 14 tangu nihitimu shahada lkn sijafanikiw kupanda cheo kazini.

Kama mwaka na nusu umepita Kuna jamaangu nilimshauri kuhusu madhara ya uzinzi, akazingatia,

juzi nimekutana naye akiwa na furaha kuu kwa mafanikio aliyoyapata baada ya kuzingatia ushauri niliyompatia,

yeye anasema alituma kwa mchungaji mchango wa SH. elfu 20 tu, baada ya kuinenea.

tangia hapo alifunguliwa na neema zinamfata mpaka sasa,

ikumbukwe wakati namshauri anasema alikuwa amekata kbs tamAa ya maisha,
miradi yake ilikuwa imekufaa, madeni kila kona, mshahara unapitiliza tu bila kununua hata shati,

sawa na hali ambayo naipitia mimi.

pmj na mambo mengi tuliyoongea,

amenishauri nihudhurie kanisani kwao kwa ajili ya maombi ya kufunga na kukesha,
kwamba RC ninakosali hakuna nguvu za kiroho,

npo njia panda sielewi kinachoniangusha na wapi ntApata msaada.

- kumradhi kwa uandishi na mpangilio mbovu,
penye utata uliza ntafafanua vzr

- Matusi na lugha za kejeli naomba sana viepukwe.
Wewe unaijua mahakama ya Mungu inavyofanya kazi, Rudi mahakamani mwombe Mungu faili lako. Akikupa muulize why unaruhusu, nifanyeje niondoke kwenye hii kadhia. Atakupa Cha kufanya. Hujafungiwa kwenye sadaka, Kuna mkataba upo unazuia hatua zako. Pia omba toba kama mkosaji halisi. Tusitumie kigezo nafanya,.may be Huwa hufanyi istahilivyo. Rudi na neno alilosema njoo tuhojiane, upate kupewa haki yako. Kahoji!
 
Tuliza kichwa tu mkuu ,hamna cha mchungaji Wa kweli wala Nini!
Maombi yanaanza na Wewe,Muombe Mungu Kwa Imani,afanye asifanye we shukuru tu,Amini wakati wako WA kufanikiwa U karibu!then weka mipango yako Sawa!
 
W nakujibu Honest kabis kwasababu ni ndugi yangu.
Sijielewi aisee.
Ila Najikuta tu huku kwa Dini. Labda sababu nina 35+ , na sina shauku kwenye mapenzi, na pia sina hamasa kwenye Siasa. Na Niko kwenye kazi na ujasiriamali.
Sasa naona bora nitoe niliyonayo kuhusu Dini na habar nyingne mchanganyiko.

Ukitoa Siasa. Mada nying naona ni za Vijana zaid. Ila ambazo nikiona naweza toa mawazo yangu. Nina chop in.
Safi sana mkuu , mimi nasoma tu bwashee 😅
 
Ni mwaka wa tatu sasa tangu niamue kabisa kuacha uzinzi na pombe na kuamua kutulia na mke wangu tu.

wakati wote nimejitahidi kuishi kwa kufuata neno la Mungu pamoja na kusali sana.

Nimezingatia kufunga, kutoa sadaka, zaka na michango mbalimbali.

Mwaka jana mwezi Agosti niliweza kununua tena kausafiri kazuri ka kutembelea,

sambamba na kuanzisha mradi wa kilimo cha bustAni kubwa.

mwezi wa pili mwaka huu, Mrs alipata changamoto kazini, iliyopelekea kuhamishwa kituo, hivyo nilijikuta nauza gari ili kulipa madeni ambayo tulikuwa tumejikopesha.

nimeendelea na kilimo lkn hadi sasa mtaji umeisha, sina namna ya kuweza kuendelea na mradi.

hivyo nimepoteza Gari yangu na mtaji wa mradi ambavyo nilifanikiwa kuvipata baada ta maisha ya wokovu wangu,

ikumbukwe huko nyuma nishaanzisha miradi mingi na ikafa,

Mbali na hayo mimi ni mwajiriwa, lkn nimekwama kbs kiutumishi,

nina miaka 14 tangu nihitimu shahada lkn sijafanikiw kupanda cheo kazini.

Kama mwaka na nusu umepita Kuna jamaangu nilimshauri kuhusu madhara ya uzinzi, akazingatia,

juzi nimekutana naye akiwa na furaha kuu kwa mafanikio aliyoyapata baada ya kuzingatia ushauri niliyompatia,

yeye anasema alituma kwa mchungaji mchango wa SH. elfu 20 tu, baada ya kuinenea.

tangia hapo alifunguliwa na neema zinamfata mpaka sasa,

ikumbukwe wakati namshauri anasema alikuwa amekata kbs tamAa ya maisha,
miradi yake ilikuwa imekufaa, madeni kila kona, mshahara unapitiliza tu bila kununua hata shati,

sawa na hali ambayo naipitia mimi.

pmj na mambo mengi tuliyoongea,

amenishauri nihudhurie kanisani kwao kwa ajili ya maombi ya kufunga na kukesha,
kwamba RC ninakosali hakuna nguvu za kiroho,

npo njia panda sielewi kinachoniangusha na wapi ntApata msaada.

- kumradhi kwa uandishi na mpangilio mbovu,
penye utata uliza ntafafanua vzr

- Matusi na lugha za kejeli naomba sana viepukwe.
Du unatuma 20000 kwa Mchungaji unabarikiwa saidia wenye mahitaji ndugu + watoto yatima kula nawo na kunywa ndani ya siku 7 utaona mabadiliko
 
Hilo wanao fanya kunenea kwenye sadaka ni ushirikina hamna Umuungu ndani yake.....African yuna shida kubwa.
Hakuna mahali katika Biblia palipoandikwa kuwa sadaka ni “fomula” ya kumlazimisha Mungu akupatie kitu fulani. Tatizo watu ni wavivu wa kusoma Maandiko.
 
Shida ni akili yako badili mtazamo wako wa kufikiri na maisha yako yatabadilika tu
 
Back
Top Bottom