Nina mtaji wa laki nne na nusu, naombeni ushauri nifaye nini?

Acha uoga kijana laki nne na nusu ni nyingi mno .watu tumeanza na mavuzi tu
 
Kwahiyo ndugu Hawa jamaa wanaochoma mahindi huku mtaani mitaji yao ilianzia milioni ?
 
Naomba nimfundishe dada yangu jamani
 
Mdogo wangu yaani Achana na laki nne na nusu laki mbili Tu hapo anatoboa
 
Nunua na kuuza nguo za ndani za kinamama, ongeza taiti na sidiria.

Nunua mashine ya kukamulia miwa, uza juisi ya miwa.

Nunua na uuze yeboyebo HASA za watoto.

Fungua mgahawa(baba lishe) na usimamie ww mwnyw, biashara ya chakula inalipa Sana

Au nenda mahali penye soko lililochangamka, tafuta meza na uuze mifuko tu
 
Tengeneza mkokoteni wenye jiko , balance itumie 300,000/= (laki 3 )na kabati lake.
Nunua kg 2 za nyama , tengeneza mshikaki anza kutembeza.
Jifunze jinsi ya kutengeneza mishkaki vizuri.
Kuwa msafi (smart sana).
Unaweza pata 10,000-- 20,000 kila siku.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…