Nina mtaji wa laki nne na nusu, naombeni ushauri nifaye nini?

Daaah nyie watu nyie....
Kipindi unaanza biashara ulikua unakaa wapi mkuu..?
 
Nimecheka sana eti wanaviita vibolo😂😂😂😂 vitakuwa vya Bata
 
Nikitulia naweka kisa changu hapa hiyo laki nne na nusu ni hela kubwa sana.

Kuna kipindi nilipata kazi ya mkataba wa miezi 6 nikawa nalipwa vizuri kama elfu 45 kwa siku pamoja na hela ya usafiri basi nikajisahau nikidhani kazi itadumu aisee nilikuwa mtu wa kujipongeza na hela za posho kuja kushituka mkataba unaelekea kuisha na sina savings yoyote ya maana na madeni juu. 😂😂

Nilisota kama mwezi mmoja hivi sina kazi akiba yangu ilikuwa haizidi laki 3🤣🤣 kwakuwa nilikuwa na mke na mtoto nikampa laki 2 ya matumizi mimi nikabaki na laki 1 tu huyo nikatokomea kujitafuta upya! 😁

Haya maisha yaacheni tu!
 
Karibu mkuu
Wapewe hawa watoto uzoefu
Mtu anadharau laki 4
 
Ingekua rahis hivyo walimu si wangeshatoboa maisha mana ndo biashara yao
 
Mleta mada soma vizuri ujumbe huu utakusaidia...

Usiwaze sana biashara gani bali ni kazi gani utaifanya kwa ujuzi ili iwe biashara yako hapo itakubidi uumize kichwa kidogo!
 
Karibu mkuu
Wapewe hawa watoto uzoefu
Mtu anadharau laki 4
Tatizo wanadhani kila biashara lazima uanze na mamilioni.

Nakumbuka nilikuwa na laki hapo sijajua cha kufanya nilimfata rafiki yangu niliyesomaga nae yeye alikuwa ana ofisi kubwa katika kupiga nae story alinipa wazo konki ambalo mpaka leo limenipa hela nyingi.

Iko hivi hakuweza kunikopesha hela ila alinijua kuwa nina bidii ya kujituma kwenye kazi, basi akinielekeza kwa boss wake(anayemuuzia bidhaa kwa jumla). Nikaenda na laki 1 yangu lakini nilipewa jumla mzigo wa laki 3 yeye ndo akawa mdhamini wangu.

Nilichukua hizo bidhaa za Urembo nikaingia nazo maeneo ya machimbo huko mkoa x.. Niliuza bidhaa zote ndani ya siku 5 zikaisha nikawa na kama laki 5 na elfu 60 nikarudi town kufunga mzigo mwingne, waliowahi kuuza urembo wamenielewa hiyo faida ni kawaida maeneo ya mgodini...

Nilizidi kukomaa hivyohivyo mpaka kuwa na goli la 5m+,akaniongezea na ujuzi ambao mpaka sasa hvi ndo unaniweka mjini kama nikihitaji pesa za kula napata vizuri nimefungua ofisi 2 zinazotoa hizo huduma na wateja nawapangisha tu foleni.

Wanaosema mtaji hautoshi ni watu ambao hawajawahi kuishiwa au kuanzia chini kabisa.
Nawasilisha! 🙏
 
Hongera mkuu.ila duniani nimegundua tunatofautiana Sana..kwangu laki nne na nusu ni hela nyingi Sana tena kwa.kijana mwenye nguvu na miguu
 
Hebu acha kuandika vitu visivyo na uhalisia wewe motivation speaker
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…