Nina nia ya kuwa Rais wa Tanzania

Watanzania wengi tumejawa na kukatishana tamaa negativity mtu katoa malengo yake na mbona binafsi ninaona ana hoja!!!

Ko suluhisho letu ni kuendelea kukaa huku hatufanyi chochote huku tukitegemea muujiza au?? Ni nafikiri tunahitaji mtu mwenye uthubutu na nia ya kuimprove na kuitoa Tanzania kutoka kutegemea kodi tu na misaada kutoka nje na tujitegemee sisi wenyewe kwa kua na teknolojia na viwanda vyetu wenyewe

Mi binafsi naona yuko sahihi kwasababu mwisho wa siku kila kitu kinaanza na nia na baada ya hapo ndo inafuata namna ya utekelezaji wa hiyo nia

Mwisho Nina swali kwa mtoa mada unafikiria kuja na mkakati gani wa kutengeneza Tanzania ya viwanda ili vidumu make kujenga viwanda sio mwisho tu suluhisho unahitaji soko,mtaji n.k na vingine vingi make hata hapo nyuma viwanda vilikuwepo vingi lakini mpaka sasa havifanyi kazi kwa asilimia kubwa.
 
Shida hapa sii kukatishana tamaa,je kwanza tunajua shida yetu ni nini? Binafsi nimechukulia mawazo yake positive ila pia mengi kati ya maswali yangu hajajibu hata swali la kipimo cha umadhubuti wa kukabilia na hoja kinzani,na jinsi ya kuichukulia mitazamo tofauti.
 
Shida hapa sii kukatishana tamaa,je kwanza tunajua shida yetu ni nini? Binafsi nimechukulia mawazo yake positive ila pia mengi kati ya maswali yangu hajajibu hata swali la kipimo cha umadhubuti wa kukabilia na hoja kinzani,na jinsi ya kuichukulia mitazamo tofauti kwa umakini.
 
Approach yangu haiwezi kuwa approach yako kila mtu ana-approach yake hata nchi zilizoendelea zimetumia approach tofauti tofauti
 
Uongo wamapema asubuhi kabla hapajakucha,ila hujasema kama mabomba yatatoa maziwa🤣
Changamoto kubwa uliyonayo ni ushamba na hujatembea kuna miji ukienda ya ulaya na asia kwa nchi kama japan au korea huwezi kuta mjini una vumbi au matope ni pavement au lami sehemu zote za mjini

Ukienda miji kama london, tokyo, melbourne, toronto n.k seolu ni ngumu sana kukutana na mavumbi kama ilivyo miji yetu kama wao wameweza kwanini sisi tushindwe kuifanya miji yetu isiwe na mavumbi kama ilivyo sasa

Changamoto kubwa ya afrika watu wana exposure ndogo sana
 
Katika vitu ambavyo haviwezi nizuia ni hii negative ya watanzania nawajua vizuri sana mfano nimesema baadae baada ya kuboresha shule na hospital serekali itajitahidi sana kuweka pavement kwenye maeneo ya mjini ili kusiwe na vumbi mtu anakukebehi anasahau ukienda ulaya au nchi za asia kama south na japan miji yao haina vumbi sasa kama wao wameweza kwanini sis tushindwe

Kuhusu viwanda kutakau na government agency itakayovipambania viwanda kwa njia zifuatazo
  • Kuhakikisha viwanda vinapata raw material
  • Kuhakikisha viwanda vinapata machine zinazotumika viwandani
  • Kuhakikisha viwanda vinapata skilled labour
  • Kuhakikisha bidhaa zinazozalishwa Tanzania zinakua na bei ndogo kwenyw soko la dunia ili ziuzike
  • Kuhakikisha bidhaa zinazozalishwa Tanzania zinakua na ubora ili ziuzike kwenye soko la dunia
 
Poa ulaya umefika wewe tu na unahitaji kuja kuwakamata masikio mbumbumbu wa bongo,hadi hapo ndio maana ulikimbia kujibu maswali yangu,inatosha sihitaji hata kusumbuka na wewe.
 
Kupitia mikopo siyo au kodi za vichwa
 
Hongera mdogo wangu ,ukiwa raisi anzisha wizara ya kilevi na ulevi staarabika niko hapa kuwa waziri chini ya uongozi wako mkuu
 
Poa ulaya umefika wewe tu na unahitaji kuja kuwakamata masikio mbumbumbu wa bongo,hadi hapo ndio maana ulikimbia kujibu maswali yangu,inatosha sihitaji hata kusumbuka na wewe.
Kama unashangaa mji mzima kupigwa pavement hilo sio kosa langu ni lako

Nikusaidie florence walipiga pavement mji wao mzima mwaka 1339 kama unashangaa leo hii 2024 mji mzima kupigwa pavement pole
 
Nakupongeza kwa nia uliyonayo,
Lakini inapaswa ujue kila ndoto inahitaji mchakato/hatua ili kuikamilisha.

Ndoto ili itimie ni step, Start moving now.
Kila unachokiona hapo chini kina mpango mkakati wake;
i) kupima nchi nzima na kuzalisha umeme megawats 300,000 (gigawatts 300)
ii) kuanzisha viwanda zaidi ya laki 1
 
Ahsante kwa maoni yako
Lengo la kuleta huu uzi umu ni lipi kana hutaki kujadiliana na watu masuala ya msingi kama.

Utakuwaje Rais bila kuwa vyama vya siasa na hapo juu umesema ni kupitia movement za wananchi ambazo nadhani namaanisha power of influence, sawa hao wananchi wanakufahamu wewe kama nani kwasasa na huo ushawishi utatoa wapi.? utajibu short.

Umeulizwa hio hela ya kujenga viwanda laki moja hujibu , kwanini usingeishi nayo tu hii nia yako kama hutaki majadiliano
 
Sidhani kama ni kosa kukuambia ahsante kwa maoni yako
 
Hata hao walijuja na point hizihizi... Sahivi Tunabuluzika

Lakini pambania ndoto, Inawezekana Tu
 
Usirudie kuandika maandishi yenye rangi rangi ni Uxee….
Kwanza huwezi kua rais uanekuandikia vitu vya marangi rangi kama kindergaten

Ebu endelea kukua akili yako bado ww pamoja na hawa waliokupa like
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…