Nina nia ya kuwa Rais wa Tanzania

Huwezi kuwa Rais kwasababu uandishi wako unakusaliti. Unachanganya lugha kama mwehu. Halafu unazijua MW 300,000 za umeme au umekurupuka tu? Bwawa la Nyerere linalotutoa jasho ni MW 2100. Viwanda laki 1 ukivijengea ndotoni ni sahihi. Kwa katiba ya TZ huwezi kuwa Rais bila chama cha siasa. Na hadi uwe Rais lazima uwe umepita kwenye nyadhifa mbalimbali.. wewe hata uenyekiti wa mtaa haupo.
 
Na sio megawatts 300,000 nilikosea ni 1,000,000 (gigawatts 1000)
Ahsante kwa kushiriki na lazima niwe Rais
 
Usirudie kuandika maandishi yenye rangi rangi ni Uxee….
Kwanza huwezi kua rais uanekuandikia vitu vya marangi rangi kama kindergaten

Ebu endelea kukua akili yako bado ww pamoja na hawa waliokupa like
Ahsante kwa kushiriki
We tukana matusi yote kamwe huwezi badilisha nia yangu
 
Ni vzr kuwa na maono makubwa, lakini ungeanza kutuambia mpaka hapo ulipo, umeishafsnya nini? Au unatafuta tu ajira ya mshahara mnono?mbele ya kitita anacholipwa raisi, hata kila za anaweza SEMA, mkinichagua, nitaifanya TZ iwe kama America, UK, au, Canada! Wakati hata ghetto analoishi halina hata AC!
Yaani, hujawahi kujenga chochote, lakini unataka tukupe nchi uijenge! Seriously!
Vijana kama, Mero,au Fernandez wa Nala, au Gibson kawago, au Mond, wakisema tuwape nchi sawa, maana kwa nguvu zao tu wameweza kutengeneza biashara kubwa zinazotoa ajira, lakini hawa wengine, wana elimu tu, hawajawahi hata kutengeneza, andiko kusaidia kijiji au kata, au, mtaa, hawajawahi, hata kuwa viongozi wa kata na mtaa, au, ksmpuni kubwa, ila wanataka tuwaaamini watafanya maajabu wakiingia ikulu! Kama ni hivyo kila MTU anaweza kuifsnya bongo itiririke maziwa na asali!
 
Ahsante kwa kushiriki kamwe hakuna mtu atakayenirudisha nyuma ongea mpaka kilugha chako ponda unavyojua, tukana unavyoweza ila kamwe siwezi acha adhma yangu

Kwani hao wakina fernandez, mond wamekatazwa kutangaza nia waambie watangaze
 
Changamoto kubwa inayoikumba Tanzania na nchi nyingi za Afrika ni kama zifuatazo;-
i) Uwepo wa walipa kodi wachache sababu watu wengi wanajihusisha na informal sekta kwa hiyo wengi hawalipi income tax na kodi nyingine.

ii) Kwa sababu kuna walipakodi wachache imepelekea nchi nyingi kuongeza kodi kwenye vyanzo vilevile na hii imepelekea kuumiza wananchi wengi.

iii) Kiwango cha kodi kinachoongezeka hakiendani na ongezeko kubwa la watu na mahitaji yao hivyo kuwepo kwa deficit kwenye budget.

iv) Kwa sababu wigo wa kodi ni mdogo imezilazimu nchi nyingi za africa ikiwemo Tanzania kukopa ili waweze ku-finance budget zao na kuleta changamoto nyingine ya madeni.
 
Hana akili ya kujibu hoja yoyote huyu
 
Kila unachokiona hapo chini kina mpango mkakati wake;
i) kupima nchi nzima na kuzalisha umeme megawats 300,000 (gigawatts 300)
ii) kuanzisha viwanda zaidi ya laki 1
Nmemaanisha fuata alichokushauri mdau hapo juu, Anzia huku chini ( kwenye jamii )

Huo ndio mchakato wa kukufikisha unapoptaka.
 
Nmemaanisha fuata alichokushauri mdau hapo juu, Anzia huku chini ( kwenye jamii )

Huo ndio mchakato wa kukufikisha unapoptaka.
Ushauri wa kukatisha tamaa kamwe siwezi uchukua
Wananchi wanataka umaskin uondoke na sio kitu kingine
 
Ushauri wa kukatisha tamaa kamwe siwezi uchukua
Wananchi wanataka umaskin uondoke na sio kitu kingine
Doh! Kuanza kuchukua hatua ni kukatishwa tamaa ?

Nadhani kuna tatizo sehemu hasa kwenye uelewa wako, Sasa ndugu unakatishwaje tamaa kirahisi namna hii utaweza kusimama kweli kuwa raisi ?
 
Hongera kwa nia nzuri.

Maswali yangu kwako kupima uwezo wako!

1. Utafanikishaje ujenzi wa viwanda laki 1 ndani ya miaka 10 tu?

2. Utafanikishaje sekta zisizo rasmi kuajiliwa kwenye viwanda wakati hawana ujuzi wa kufanya kazi kwenye viwanda?
Kasema Karibu tujenge historia ya nchi yetu! Nadhani unatakiwa utoe majibu mwenyewe ya Maswali haya kuonyesha kweli una Nia ya kushiriki kujenga historia ya nchi na si kumkatisha tamaa mleta mada.
 
Huo umeme wa GW 1000 ndio umeme ambao US anazalisha sasa Kwa mwaka, Tanzania hatuna hata GW 2 kwenye gridi ya Taifa,Kwa nchi kama TZ siku ukisikia tuna GW 10 kwenye gridi ya Taifa ujue tumetoka kundi la third word countries, hauko serious wewe
 
Unafikiri kuwa rais ni sawa na kubeti, rais huandaliwa. Lakini pia kitrndo cha kuja kucomet jf nia yako ya kuwa rais kinakuondolea kabia sifa za rais unaonekana bado una waza kitotototo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…