Nina nia ya kuwa Rais wa Tanzania

Uraisi hautaki hizo agenda zako tu mkuu, urais sifa yake nyingine ni KUJULIKANA.

Anza sasa kufanya vituko vituko vyenye akili na vyenye kujenga heshima yako, sio ufanye vituko vya kina Mwijaku.

Tofauti na hapo,anzia uwenyekiti wa mtaa kwanza safari ya kuwa rais sio haba tena kwa Tanzania ndio kimbembe.

CCM wana list ya rais hadi wa mwaka 2060 majina wameyapanga tu. Ni wewe uwashawishi wamtoe nani wakueke wewe ila Rais tayari wanae.
 
Lofa mfanyabiashara ndogo machinga eti utajenga viwanda laki moja

Una Hela za kujenga wewe

Hata ulichosoma hukuelewa hujui hata anayejenga viwanda nani ? Hata ukiwa Raisi

Hapo unaaibisha hicho kidigrii chako Koko kina jina refu lakini hamna kitu
Mimi nimemshangaa kweli yaani anavyotiririka kutaja idadi ya viwanda utadhani kujenga kiwanda ni sawa na kununua baiskeli au bodaboda.
Huyu dogo hata shule yake alienda kuhudhuria tu ili kuongeza miaka ya ukuaji.
 
Duniani kote viwanda ndo mkombozi wa watu ambao hawajasoma blue collar job
Viwandani machine operator ndo wanatakiwa kusomea ku-operate machine

Kama umeshawahi kufanya kazi kiwandani utanielewa
Wewe unaongelea wale vibarua wa kiwandani wanaolipwa mshahara wa elfu 5 kwa siku.
Sasa kwa akili yako wewe kibarua wa kiwandani na mmachinga wa kariakoo ni yupi anapata hela nyingi zaidi?
 
Acha ujinga mzee hujui hata Sheria zakua raisi halafu unataka uraisi boya wewe nyie ndio mnakuwaga mafisadi mkishaingia kwenye vyeo mwanzo mnajifanya mtasaidia wananchi raisi wa kweli kama magu alikua Hana mambo mengi anasema sitawaangusa tu basi Sasa wewe porojo nyingi hata form hujapewa kiufupi wewe tapeli kama wajinga wenzio wa ccm
 
Hakika, nakuunga mkono. Ni kweli u-machinga na bodaboda siyo ajira mujarabu!
 
Mkuu tangu uhuru viwanda vidogo na vikubwa jumla ni 98,678 so ww utawezaje kujenga laki moja kwa miaka 10 au unaota
 
Nilivyoona umesoma uchumi nikajua fika concept ya demand and supply unaifahamu vilivyo.
1. Tuambie hivyo viwanda ni vya nini?.
2. Wateja wa bidhaa zitakazo zalishwa na hivyo viwanda ni kina nani?.
3. Nguvu ya ununuzi (Purchasing power) ya hao wateja wako ikoje?
4. Unafahamu maana ya viwanda 100K???????

Haiwezekani kwa uwezo wa uchumi wa Nchi yetu kujenga viwanda (VIWANDA) 100K kwa miaka 10 tu. andiko lako ni MYTH
 
Kwako haiwezekani ila kwangu mimi inawezekana
 
🤣🤣🤣 Naona umeshindwa kabla ya kuanza
 
Ukitaka kuwa Rais wa JMT, usikipinge kwanza chama kilichoko madarakani kwa sababu baadhi ya watu waliomo kwenye chama hicho ndiyo wanaoweza kukuingiza kwenye Urais. Unatakiwa uchukue madaraka kwanza halafu baada ya hapo ndiyo uanze kusema mapungufu yake kwa kutumia SIASA; usikipinge
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…