Nina miaka 32, elimu bachelor of science economics population and development chuo mzumbe, kazi nayojishughulisha kwa sasa mfanyabiashara
Kama kisemavyo kichwa cha habari nina nia ya kuwa Rais wa Tanzania, kwanini nimeonyesha nia ni kupitia sababu zifuatazo;-
i) kwa miaka 10 ntajenga viwanda zaidi ya laki 1 ndio laki moja
ii) kwa mda wa miaka 10 ntaongeza pato jipya lenye thamani ya usd billion 100 na zaidi fahamu hiki ni chanzo kipya
Kutakua na zone saba nchi nzima ambazo zitakua ni kitovu cha viwanda ili kupeleka maendeleo kila mahali ni kama zifuatazo;-
a-Wilaya ya mpanda na uvinza viwanda zaidi ya 20,000
b-Wilaya ya muleba na karagwe viwanda zaidi ya 20,000
c-Wilaya ya kishapu na shinyanga vijijini viwanda zaidi ya 20,000
d-Wilaya ya itigi na manyoni viwanda zaidi ya 20,000
e-Wilaya ya ruangwa na lindi vijijini viwanda zaidi ya 20,000
f-Wilaya ya mwanga na moshi vijijini viwanda zaidi ya 20,000
g-Wilya ya kibaha, chalinze, bagamoyo na mkurunga viwanda zaidi ya 30,000
Kutakua na factories ambazo zinazalisha bidhaa from scratch na sio assembly na vitakuwa ni vya ku-export kwenye soko la dunia
Primary industries
- Steel
- Aluminium
- Leather
- Plastic
- Glass
- Copper cable
- Battery
Secondary industries
- Automobile
- Chipset
- Home appliances
- Smartphones
- Clothes and apparel
- Aeroplane
- Pharmaceutical
Minimum wages itakua sh 10,000 kwa mwezi
FAIDA ZA VIWANDA LAKI MOJA KWA NCHI YA TANZANIA
a) Serekali itakuwa na uwezo wa kukusanya moja kwa moja usd billion 100 (Tsh trillion 250,000,000,000,000) kutoka kwenye viwanda tu; hapo sijaongelea sektor nyingine ambazo zitaguswa na viwanda indirect na zitaongeza pato la nchi
b) Viwanda Vitakuwa vinamilikiwa na familia tofauti tofauti za wazawa (watanzania), kwa gharama kubwa sana serekali itawapigania kwa nguvu zote wazawa kumiliki viwanda lengo ni uchumi kumilikiwa na wazawa na sio wageni
c) Viwanda vitaondoa sekta ambazo sio rasmi (informal sector)kama wamachinga, wauza mitumba bodaboda n.k sababu wataajiriwa kwenye hivyo viwanda zaidi ya laki 1
Njia ya kuwaondoa wamachinga ni kujenga viwanda vingi ili waajiriwe na wawe na uhakika wa pension wanapofikia miaka 60 na zaidi
Sasa hivi wamachinga hawana pension au akiba yeyote itakayowasaidia pale watakapokua wazee
d) Nchi ikiwa na viwanda zaidi ya laki 1 hizi squatters na slum zitaondoka tu automatical sababu kutakua na hela ya kuziondoa na watu watakua na kazi za uhakika na hii itaenda sambamba na kupanga kisasa nchi nzima kisasa na nyumba na majengo yatakua na mfumo unao-fanana ili miji yetu ipendeze sio kila mtu anajenga jenga namna anavyotaka
"Hakuna jiwe litakakuwa juu ya jiwe lingine; jiunge turudishe madaraka kwa wananchi"