Nina safari ya Dar kwenda Kigoma. Madereva nipeni uzoefu!

Hapo ndio mchawi. Ulazima ni mkubwa kiasi kwasababu ya nature ya kazi na vitu tunavyobeba. Unanitisha mkuu.

Huu mwaka longest trip nimeenda ni Dar - Njombe moja na Dar Songea kupitia Lindi moja.
Dar - Songea via lindi, kwa private car, napo jau pia.
 
X5 achana nayo kabisa iwe Option ya mwisho….zibaki Fit na Crown
1. Fit itumie ikiwa budget yako sio rafiki . So best Option hapa ni Crown, kama gari haina changamoto za kiufundi basi ulaji mafuta utakuwa kawaida haswa ukizingatia ni HighWay, No breaks nyingi Why Crown ? i/ Comfortability as ni safari ndefu lazima mtachoka mnahitaji gari yenye uhuru ii/ Capability , kwa safari unayofanya Crown ndio shughuli zake as ni gari yenye Engine kubwa, perfomance nzuri barabarani…wajuzi wa hiyo route wanadai kuna kipande cha Vumbi kifupi hii sio tabu, hapo itavumilia( low speed+ Driving ya umakini)
*Ratiba/Mpango wa Safari :- Toka Dsm mapema sana ikifaa saa mbili asbuh ikikute Morogoro…fanya kazi zako Saba Mchana anza safari ya Dodoma ( Ukifikahapa/Dom utapima hali yako ya uchovu kama bado una-Energy unga kalale Singida ili ukiamka uitafute Tabora, ila kama umechoka lala( vzuri upate muda kupumzika vya kutosha) kisha kesho yake mapema uanze kuzikata Singida na Tabora ) . Utatupa Updates hapa za Safari yako na vituo utavyo weka .Kila kheri
 
Hiyo x5 ni bmw x5 au mazda cx5? Vipi kuhusu ile atenza yako kwa nini usiende nayo
 
Mkuu, shukrani sana naomba nipime haya maelezo vizuri mkuu. Shukrani sana hapo kwenye mpango wa safari.
 
Kama ni bima haifai,, 😂😂Kumbe chuma ulishakunywa kitambo
Hahhaa Diesel SkyActiv D tuwaachie wenyewe si tunaki na Petrol. Ila Atenza ingefurahi sana hii safari.
 
Kwanini aende mpaka Singida?
 
Ondoka Dar saa 9 usiku fika Moro saa 2 asubuhi piga kazi Hadi saa 6 mchana amsha ukalale Kaliua (Tabora) kisha amsha hadi Kigoma. Kama vipi uunge hadi kwenu Bujumbura
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…