Nina safari ya Dar kwenda Kigoma. Madereva nipeni uzoefu!

Hapo kwenye singida umepotea.
Kutoka Dom ukifika manyoni kuna shortcut ya kwenda Tabora ni km 250. Barabara mpya na haina magari
 
Ondoka Dar saa 9 usiku fika Moro saa 2 asubuhi piga kazi Hadi saa 6 mchana amsha ukalale Kaliua (Tabora) kisha amsha hadi Kigoma. Kama vipi uunge hadi kwenu Bujumbura
Uondoke dar saa 9 usiku alafu moro ufike saa 2? Hiyo gari au Bajaj😅
Ukiondoka saa 9 inapaswa saa 12 na nusu uwe moro
 
Safari njema mkuu...
Tunataka update zote zitumwe huku...

 
Ulale Dom. Ukiwa unaendesha kupumzika ni muhimu sana. Kutoka Dom Jumamosi asubuhi utalala ndani ya mkoa wa Kigoma na jumapili utaingia Kigoma mjini.
 
Naenda na bebe nae ni dereva mzuri tu. Tunataka tuwe na vituo vya kulala viwili hivi ila kurudi hatuna haraka tunaweza lala ata kila mkoa (Tabora, Dom ata Moro).
Mnaenda kuchepuka km si mkeo.
Mi nishaweka Rip. 🙌
 
X5 ingekuwa unyama sana, au ungekuwa na GLE Coupe 😎.. mtoto awe kavaa kimini mapaja meupe kasura innocent.. trafiki akisimamisha anaisoma namba
 
Hapo kwenye singida umepotea.
Kutoka Dom ukifika manyoni kuna shortcut ya kwenda Tabora ni km 250. Barabara mpya na haina magari
Hakuna majambazi huko?
Hapo mbele ya Manyoni kuingia ndani huko tulipigwa tanchi tukatemeshwa kila kitu hadi chupi bus zima.
Si wamama, si watoto woote unavua unaenda kulala chini
 
Hakuna majambazi huko?
Hapo mbele ya Manyoni kuingia ndani huko tulipigwa tanchi tukatemeshwa kila kitu hadi chupi bus zima.
Si wamama, si watoto woote unavua unaenda kulala chini
Hayo mambo sehemu nyingi yalikuwaga zamani, lakini kwa sasa hiyo njia watu wanapita 24/7
 
Per diem utakayolipwa itaishia kwenye mafuta,
 
Gharama ya mafuta ya Km 2500
Gharama ya mafuta km 2500 kwenda na kurudi(5,000 Km) na kula njiani ni kiasi gani?
Air Tanzania go and return kigoma kama laki 7 na vichenjichenji, Precision haifiki huko ila ukienda kupandia Mwanza mpaka dar kwenda na kurudi ni kama laki nne na nusu.
Gari unaacha airport pale.
Au unataka ununue kuku singida,mafuta tabora pale ufike Dodoma ununue wine ufike chalinze ununue nyama choma,mananasi vyungu na miiko.vya kupelekea wenyeji wako dar au vya kurudi navyo nyumbani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…