Nina shilingi milioni 64, niwekeze kwenye biashara gani kati ya hizi?

Nina shilingi milioni 64, niwekeze kwenye biashara gani kati ya hizi?

Tatizo la nyumba unazika pesa na faida inakuja kuonekana baada ya miaka mpka 7,8 na kuendelea mbele hapo unadhani kibongobongo hiyo ni hasara chukulia nyumba ya M50 kali unapangisha 500k kwa mwenzi hapo Ela inarudi baada ya miaka 9 hapo ikiwa imepangishwa non stop na kitu ambacho hakiwezekani pia kodi nimechukulia kodi ya 500k ambayo ni kubwa ila kikawaida ni 200k mpka 300k.
Zipo sehemu Kigamboni watu wanalipa rent 500k per month...
 
Fanya biashara ya agricultural finished products kama mafuta ya alizeti na unga wa mahindi

Kodi Jengo au jenga jengo dogo weka mashine ya kusaga na kupack unga. Uza hapohapo Dodoma

Kuhusu mafuta ya alizeti nunua tu Kibaigwa harafu uza hapo Dodoma .utapata hata tenda vyuoni kwenye ma cafe

Angalizo:biashara yoyote usiiianze na more than 50% of your capital
 
Usijaribu biashara hii kichaa, utamnufaisha dereva.
Wekeza UTT mfuko wa wekeza maisha kwa miaka kumi. Kila mwaka utapata interest ya 30% ukiwa umekaa bila kufanya kazi. UTT hautojuta.
UTT kuna plan ambayo ina interest ya 30% mkuu? Are you sure?
 
Biashara ni desire,passion,vision,mission na ambition.Kwa hiyo huwezi kuchaguliwa hivi vitu na mtu
Nakubali mkuu, ila hivyo vyote vinaweza kuwa developed. Au haiwezekani? Maana si naweza nikashauriwa idea, nikaichukua na kuifanyia research na kudevelop passion na desire along the way... Then nikatengeneza mission na vision before entering into that business...
Au haiwezekani?
 
Nunua eneo kubwa nje ya mji kama Nala au michese....chimba kisima...M15 inakutosha kabisa na apo umenunua na jenereta incase umeme ukikatika......haya chimba bwawa la samaki(mawili ili ufuge samaki aina mbili na kambale wakiwemo)....weka drip irrigation...jenga kijumba kidogo cha msimamizi..hapo roughly itafika M30....chukua M8 nenda kwa doctor bajaji hapo chukua TVS mpya ...hii itakusaidia kama passive income ili usilie lie njaa..na pia usiguse kiasi kilichobaki kwenye m64 ....kumbuka utakua umebaki na M16, imetulia..hii mpaka ifike miez ,6 utakua umepata akili ya wapi uiwekeze
NB: kwakua umekiri wazi hujawah fanya biashara..wewe huhitaji biashara za kuumiza kichwa kwakua pia usimamizi wako utakua mdogo...
Ukipata hela yeyote kwenye sources zako anza biashara ya kujenga Nyumba za kupangisha au nunua government bonds
Asante sana mkuu
 
UTT kuna plan ambayo ina interest ya 30% mkuu? Are you sure?
Yaani uweke 2,000,000/= UTT na mwisho wa mwaka upate faida ya 600,000/= kwa riba ya 30% hamna hiyo aisee yaani kwa mwezi faida ya 50,000/= UTT hawajawai kuwa na ukarimu huo.

Watu wangeamisha hela zao benki waweke UTT wapate hizo faida huku wamekaa nyumbani, yaani 10,000,000/= upewe faida ya 3,000,000/= kutoka UTT hamna hiyo
 
Back
Top Bottom