Nina shilingi milioni 64, niwekeze kwenye biashara gani kati ya hizi?

Nina shilingi milioni 64, niwekeze kwenye biashara gani kati ya hizi?

Fanya biashara hii hutojutia maisha yako milele Geita MPUNGA vijijini una 70000 junia njoo chukua junia za kutosha subiri a mwezi wa 12 karibu na Christmas mchele Kilo 2500-2800 we kila junia ukipewa 150000 utakuwa na faida ya 80000 kwa kila junia hahahaaaa njoo uone matajiri vijijini japo sio matajiri Sana ila ni matajiri
Kijiji gani hapo Geita mchele umeshuka hivyo? Sengerema nimepata taarifa una Tsh 80K per gunia.
 
Utakuja mnaemshauri hana mia... Kijana mbongo mwajiriwa mwenye Milioni zoteizo anapatawapi adabu ya kutulia kusoma posti na kujibu watu vizuri!! Labda kama anatarajia kuzipata/kuzikopa
 
Habari wakuu.

Natumaini mnaendelea vizuri na maandalizi ya sikukuu.

Bila kuwachosha sana, nimeweza ku save jumla ya shilingi milioni 64 hadi sasa, kiasi hiki nimeweza kukisave kuanzia mwezi April mwaka huu kutoka kwenye mshahara wangu. Nipo mkoa wa Dodoma.

So far, nimefikiria kuwekeza katika mojawapo ya mambo yafuatayo:

  1. Ninunue eneo la shamba kubwa maeneo ya Dodoma nje ya mji au Dodoma vijijini kisha nianzishe kama ranchi hivi ya ufugaji wa mbuzi.

    Nimefikiria mbuzi kwa sababu kwa utafiti wangu wa muda mfupi nimeona kuwa mbuzi hawana complications nyingi kulinganisha na wanyama wengine wa kufuga, na pia kuna fursa zaidi kwa mbuzi nchini, na demand ambayo haijawa satisified.

    Lengo la hii ni baadae niweze kuwa na kiwanda kabisa cha kuchinja na kuprocess nyama ya mbuzi, na kuweza hata kuuza ndani na nje ya nchi products za nyama ya mbuzi.

  2. Nifungue park kwa ajili ya michezo ya watoto kwa Dodoma. Moja ya gaps ambazo nimeziona Dodoma ni kukosekana kwa eneo zuri la maana kwa ajili ya michezo ya watoto na watu kupumzika pia.

    Hapa nafikiria ninunue eneo Dodoma then nilitengeneze vizuri na kuweka michezo ya watoto (indoor na outdoor) ya kutosha, pamoja na kutengeneza garden nzuri ya kuvutia kwa ajili ya watu na familia zao kupumzika na kupigia picha.

    Kwa nje kwenye ukuta nawaza pia kuwe na frame kadhaa ambazo nitakodisha kwa watu waweke maduka ya vyakula, vinywaji, na vitu vya watoto.

  3. Nifungue kiwanda cha maji ya kunywa yale ya kwenye dispenser kwa ajili ya matumizi ya majumbani na maofisini. Nimeona gap pia hapa kwa sababu makampuni yaliyopo hapa Dodoma kwa hii huduma hayatoshelezi mahitaji kwa kiasi kikubwa, mara nyingi sana unakuta yanapotea sokoni kwa muda fulani (no consistency of supply).

  4. Ninunue kiwanja saizi ya kati maeneo ambayo sasa hivi ndo yanajengeka (eg Ilazo, NALA) halafu nipige vyumba vya low-cost (behewa style), niweke hapo vyumba kadhaa, then nipangishe nile kodi kila mwezi hata 50K kwa kila room. Baadae kadri ninavyopata mpunga zaidi, niongeze idadi ya vyumba zaidi na zaidi.

    Wenye uzoefu wa biashara na ideas na mnaoifahamu Dodoma, niambieni hapo nianze na ipi kati ya hizo kwa mtaji huu nilionao (milioni 64), au hata idea nyingine ambayo sijaitaja hapo juu.

    Mimi maisha yangu yote nimeajiriwa tu hadi sasa (nina umri wa miaka 35). Sijawahi kufanya buashara hata ya kuingiza shs 500. Nimeona ni bora pia niangalie upande huu wa business pia maana siwezi ajiriwa milele, na pia kama mjuavyo hizi ajira zetu, leo ipo kesho haipo hasa huku private sector.

    Natanguliza shukrani.
Nunua vyombo vya music ukodishe,inalipa sana
 
Build a beautiful house and rent it out kama AirBnB.
 
Utakuja mnaemshauri hana mia... Kijana mbongo mwajiriwa mwenye Milioni zoteizo anapatawapi adabu ya kutulia kusoma posti na kujibu watu vizuri!! Labda kama anatarajia kuzipata/kuzikopa
Akili mgando hizi
 
Kuna comments kama ya huyu uliem quote huwa naziona then naamua kuzipotezea tu mkuu. Wangejua bongo hii hii hata katika watu wanaolipwa hela nyingi sipo, pamoja na kulipwa 14+ per month. Kuna watu wanakunja mara mbili ya hiyo.

Umasikini ni mbaya sana, ndo chanzo cha wivu na frustrations za hivi, kwa hiyo mimi huwa naelewa sana watu wa namna hii.

Mimi nimeweka nidhamu kubwa sana pia katika ku save. Na save 2/3 ya net income yangu, I live a very simple life.

Kitu kikubwa kinachoniumiza kichwa ni namna ya kuizalisha hiyo pesa, kama nilivyosema awali sijawahi fanya biashara ya kuzalisha hata 500.

Mkuu, TMO analipwaje per month?

-Kaveli-
 
Kutofanya biashara unafeli. Pamoja na kuwa na chanzo kikubwa cha mtaji halafu haujawahi kufanya biashara hata kidogo? Badilika mwaka huu. Use your savings to start a business.
Kuna comments kama ya huyu uliem quote huwa naziona then naamua kuzipotezea tu mkuu. Wangejua bongo hii hii hata katika watu wanaolipwa hela nyingi sipo, pamoja na kulipwa 14+ per month. Kuna watu wanakunja mara mbili ya hiyo.

Umasikini ni mbaya sana, ndo chanzo cha wivu na frustrations za hivi, kwa hiyo mimi huwa naelewa sana watu wa namna hii.

Mimi nimeweka nidhamu kubwa sana pia katika ku save. Na save 2/3 ya net income yangu, I live a very simple life.

Kitu kikubwa kinachoniumiza kichwa ni namna ya kuizalisha hiyo pesa, kama nilivyosema awali sijawahi fanya biashara ya kuzalisha hata 500.
 
Hii biashara ya lodge ni nzuri sana na inalipa vizuri kweli hata mimi nashauri hili ingawa sina taarifa sahihi ya bei za viwanja huko.

Lakini kwenye hayo maeneo tajwa na mwandishi anaweza kuangalia ni wapi kumechangamka na kuanza na lodge moja kali ya kisasa na ikamlipa vizuri sana kisha baada ya miaka mitatu akafuangua park kali sana hadi ukashangaa..

Biashara ya lodge na hotel need proper management to keep your customer. Ikiwemo ukarabat wa mara kwa mara
 
Hii biashara ya lodge ni nzuri sana na inalipa vizuri kweli hata mimi nashauri hili ingawa sina taarifa sahihi ya bei za viwanja huko.

Lakini kwenye hayo maeneo tajwa na mwandishi anaweza kuangalia ni wapi kumechangamka na kuanza na lodge moja kali ya kisasa na ikamlipa vizuri sana kisha baada ya miaka mitatu akafuangua park kali sana hadi ukashangaa..

Ukitaka kujua 64 M ni hela ndogo

Ngoja aingize kwenye biashara

Ukiona mtu katoboa kwenye business muheshimu

Reality on the ground huwa nitofauti na expectations
 
Kwanza nikupe hongera mkuu kwa kuweza kukusanya mtaji, Mimi nitakushauri mambo machache ya kufanya

1. Kwa kuwa hujawahi kufanya biashara yoyote ile , Ili kuepuka kupoteza mtaji fanya biashara ambayo haita risk mtaji wako kwa kipindi Cha miezi isiyopungua 6 Ili kupata uzoefu wa hesabu za mapato na matumizi yatokanayo na biashara, mfano anzisha tu kagoli ka tigopesa au uwakala wa bank ( kuwa makini na eneo utakalochagua) hapa test tu na mtaji wa 4m lengo ni kuzoea biashara na namna hesabu zinavoenda huku mtaji wako ukiwa salama



2. Option nyingine wekeza kwenye real estate ( tafuta maeneo yenye potential kwa baadae mfano maeneo ambayo lami itapita siku za usoni tafuta hata heka kadhaa za karibu na barabara kisha tulia zako ( kuwa makini na road reserve), lami ikipita hayo maeneo yatapanda almost mara 4 au tano ya bei uliyonunulia, Kuna maeneo jamaa alinunua eka kwa 250k saivi wadau wanapataka kwa milion 8 na jamaa hataki kuuza


3. Usiingie kwenye kilimo,ufugaji, uchimbaji, au ujenzi huko utapoteza pesa (kama interest yako Ipo kwenye kilimo, au ufugaji hakikisha unatumia faida itakayopatikana ) hivi vitu hupotezaga pesa ndani ya sekunde

4. Kuna nyuzi zangu mbili niliziandika siku za nyuma nikitaka partner mwenye mtaji wa around 3m to 6m na ni 0 risk ukiwa tayari zipitie tunaweza fanya kitu kwa mtaji wa million 6 tu

Hongera

Real estate kwa mil 64, ???guys hizo ni dola 25K tu
 
Umesevu Mil 64 kwa miezi nane kutoka kwenye mshahara. Hii ina maana kama umeweza save million 8 kila mwezi kutoka kwenye mshahara, na uko Dodoma, najiuliza mshahara wako kiasi gani kwa mwezi? Maana mahesabu kawaida unaweza kusave maximum 30% ya mshahara wako kwa mwezi wakati pesa zingine zina matumizi mbali mbali. Unless pia una biasara nje ya mshahara ya kuingiza kipato na hutegemei mshahara kwa kila kitu. Kama umeweza save hiyo pesa kwa muda mfupi, hiyo ni biashara tosha. Anyways, watu tumepishana sana kimapato. Hongera
 
Hongera sana kwanza kwa kukusanya hiyo 65m. Ushauri wangu kwanza achana na wazo la ku invest Dodoma.

Nenda Dar chukua viwanja viwili maeneo ya Goba au madale jenga apartment zako mbili hata za vyumba vitatu vitatu. Trust me unakula hela ukiwa umekaa.

Shida ya hizi investment zingine inabidi ukimbizane sana lkn investment ya nyumba ukishamaliza ujenzi hela inakukuta umekaa.

Wazo zuri, hela haitoshi kununua kiwanja goba na kujenga nyumba za ukubwa huo tena standard. Anunue kiwanja kwanza labda, aanze kupandisha mdo mdo...ujenzi wa mbali hatari lakini
 
Kwavile una changamoto ya muda (umeajiriwa na kazi nzuri sharti itunze), usiwaze faida ya haraka ila waza usalama wa pesa na uhakika wa faida, hapo baadae.

Pata kiwanja mjini mjini hapo dodoma, say 10m

Jenga studios (chumba, sebule yenye open kitchen na bafu). Uzuri wa hizi unaweza kusoma hela inaendaje na ukafanya finishing kwa mbili au tatu etc

Kwa 50 million, finishing kali sana ya AC, water heaters, alluminium windows etc... (Japo sijui gharama za ujenzi za dodoma), utatumia si chini ya 35m kwa moja

Ukafanya finishing ya hali ya kati, unaweza kujenga mbili na ukakamilisha hadi komeo na watu wakaingia.
Hata kama kodi utaanza na ndogo, walau hela yako unaiona!
 
Namba 1 au jenga nyumba uweke wapangaji
Faida itayopatikana weka ujenge park ya michezo

Kama umeoa mshirikishe mkeo achague pia
64 m unajenga Nyumba gani na hiyo Hela Kwa rentinya laki 3inarudi lini we kale Bata Mungu anajua destiny yako
 
Back
Top Bottom