Kwanza nikupe hongera mkuu kwa kuweza kukusanya mtaji, Mimi nitakushauri mambo machache ya kufanya
1. Kwa kuwa hujawahi kufanya biashara yoyote ile , Ili kuepuka kupoteza mtaji fanya biashara ambayo haita risk mtaji wako kwa kipindi Cha miezi isiyopungua 6 Ili kupata uzoefu wa hesabu za mapato na matumizi yatokanayo na biashara, mfano anzisha tu kagoli ka tigopesa au uwakala wa bank ( kuwa makini na eneo utakalochagua) hapa test tu na mtaji wa 4m lengo ni kuzoea biashara na namna hesabu zinavoenda huku mtaji wako ukiwa salama
2. Option nyingine wekeza kwenye real estate ( tafuta maeneo yenye potential kwa baadae mfano maeneo ambayo lami itapita siku za usoni tafuta hata heka kadhaa za karibu na barabara kisha tulia zako ( kuwa makini na road reserve), lami ikipita hayo maeneo yatapanda almost mara 4 au tano ya bei uliyonunulia, Kuna maeneo jamaa alinunua eka kwa 250k saivi wadau wanapataka kwa milion 8 na jamaa hataki kuuza
3. Usiingie kwenye kilimo,ufugaji, uchimbaji, au ujenzi huko utapoteza pesa (kama interest yako Ipo kwenye kilimo, au ufugaji hakikisha unatumia faida itakayopatikana ) hivi vitu hupotezaga pesa ndani ya sekunde
4. Kuna nyuzi zangu mbili niliziandika siku za nyuma nikitaka partner mwenye mtaji wa around 3m to 6m na ni 0 risk ukiwa tayari zipitie tunaweza fanya kitu kwa mtaji wa million 6 tu
Hongera