Nina tatizo kubwa la upungufu wa nguvu za kiume

Nina tatizo kubwa la upungufu wa nguvu za kiume

Habari wote, mimi ni kijana nasumbukiwa na upungufu wa nguvu za kiume tena sana mpaka nakata tamaa ya maisha, nikiwa na mwanamke bao la kwanza namwaga ndani ya dakika moja na baada ya hapo sipati tena hamu mpaka baada ya masaa kama sita.

Nimeenda hospitalini ni kaonekana na kiwango Cha 0.69 Cha testerone ajabu nikaambiwa niwe nakula vizuri ila ukweli nakula vizuri tu, nilienda mpaka kwa waganga wa kienyeji ila sijaona mabadiliko.

Kuna kipindi nikiwa na mwanamke sipati kabisa hisia na nimeachwa na wanawake wengi.

Naombeni msaada.
Hapo tatizo lako sio nguvu za kiume. Kuna tatizo ambalo ndo linapelekea hiyo. Kama hauna maradhi mengine yanayowezapelekea hilo, basi ni ishu za kisaikolojia tu.

Kama ni ishu za psychology rekebisha life style yako; vyakula unavyokula, fanya mazoezi haswa ya kegeli, acha kujichua kama unafanya hivyo, dhibiti msongo wa mawazo, wasiwasi, au hofu. Ongeza kujiamini. KULA MAISHA
 
Unawasikiliza wahuni wale aisee mtu kakomaa kama anakula mawe anashauri watu wasile kabisa kwa sababu yeye anashinda kwenye kiyoyozi na Land Cruiser.
Na KAZI zetu hizi za zege usile kushiba si unatafuta kuzimia 🤣🤣🤣, atoke ushauri kutokana na aina za KAZI we mbeba zege unamwambia ale chakula SAA SITA mpaka kesho tena si kuuana huko
 
Ukikojoa ndani ya hiyo dakika 1 unasikia utamu au hausikii?
 
Back
Top Bottom