Magical power
JF-Expert Member
- Sep 27, 2022
- 2,158
- 5,626
Nina wanaume wawili na wote wanataka kunioa. Labda nikufafanulie kidogo, kaka. Niko kwenye mahusiano na wanaume wawili: mmoja ni kijana kama mimi, ana miaka 27, na mimi nina miaka 24. Anaishi kwao, na baba yake ni mtu mwenye pesa sana, hivyo anampa kila kitu. Hata kufanya kazi hataki, kwani ameshapewa nyumba na mama yake na mama yake anataka sana niolewe na kijana wake.
Ameniahidi kuwa nikiolewa naye atanipa mtaji na kunifungulia biashara ili niisimamie. Huyu kaka sina mahusiano naye sana — ni mama yake tu aliyenipenda sana na akasema anataka niolewe na kijana wake. Alituunganisha na mwanaume huyu, naye alivutiwa na mimi, akaahidi kunipa kila kitu.
Mwanaume wa pili ni mtu mzima kidogo, ana miaka 34. Yeye ni mfanyakazi wa serikalini, na kipato chake ni cha kawaida tu. Anaishi maisha ya kawaida, hana nyumba ya kwake; amepanga, lakini anaishi vizuri. Tumekuwa kwenye mahusiano kwa miaka 3, na sasa anataka kuja kwetu kunioa.
Shida ni kwamba ndugu zangu hawataki kumsikia kabisa. Wanasema kuwa nikiolewa naye, watanitenga, yaani ni kama wanataka niokoe familia. Nampenda huyu mtu wangu, lakini nikifikiria maisha yake na mshahara wa laki 8, naona kama hatutaishi vizuri. Naomba unisaidie, kaka, nisije kufanya uamuzi mbaya!