Ninachoona kwenye Parade ya China Aisee! Kama taifa na bara tupo nyuma sana

Sisi askari wetu wanatumika kwenda kujaza mikutano ya kampeni za Samia.
 
Kupitia maonesho ya hii parade ya wachina kutimiza miaka 80 toka vita vya pili vya dunia baada ya kumnyuka Japan.

Kama taifa la Tanzania na bara zima la Afrika tujitafakari kidogo kwa kweli tupo nyuma kiulinzi.

Kwa hizi silaha wachina walizo amua kutuonesha japo nina mashaka kama wameonesha zote kabisa walizo nazo tupo nyuma sana ndugu zangu.

Tusijiongopee wakuu tumeachwa mbali sana hizi silaha tulizo nazo kwetu sijui hawa mabwana wameziacha store maana hapa sioni huu uchafu wetu naona vitu vizito vizito mpaka inatisha siku tukianzisha ka vita ka kirafiki sisi na wao maana kamanda wetu mmoja wa JW alisema sisi ni jeshi la sita kwa ubora😁

Ukitazama kwenye documentaries silaha walizokuwa wakitumia wachina wakati wanapambana na Japan na vita vya wenyewe kwa wenyewe ni magobore ya ajabu ajabu hata airforce walikuwa hawana wala jeshi la wana maji linalo jitambua ila leo wanaonesha vyuma vizito hapa.

Sisi bado tumejaza magobore
Hawo hawana chochote Wenda wanaweza kucheza pornography ngozi nyeusi ni Bora sana katika uwanja wa vita
 
Nimeona Hadi mbwa wakiroboti.
Ila china bhana nasikia Gwanzuu ilikuwa kama DSM tu miaka ya 90 kurudi nyuma.

Haya maendeleo yameanza sisi tukiwa tayari tunauhuru.
Sisi tumeamua kuwekeza kwenye siasa na propaganda za hovyo hovyo
 
Tumeacha wanasiasa waendeshe kila kitu badala ya kuthamini sayansi na tafiti
Wanasiasa wenyewe ni Musukuma Kasheku, Lusinde, Baba Revo, Mbowe,....yes nimesema Mbowe Aikaeli😎
 
Tumeacha wanasiasa waendeshe kila kitu badala ya kuthamini sayansi na tafiti
Umesema kwa uchungu sana, hatuna mpango mkakata wa nchi ila tuna mipango mkakati wa kukaa madarakani kwa kipindi tunachokihitaji kwa manufaa binafsi. Hatuna mpango kama Nchi nini kifanyike na kiwe na faida hata kwakizazi kijacho tunajifikiri kushiba kwetu tu. Hatukubali kuanza kwa mpangilio na makubaliano tunakwenda kwa matakwa ya mtawala.
 
Kupitia maonesho ya hii parade ya wachina kutimiza miaka 80 toka vita vya pili vya dunia baada ya kumnyuka Japan.

Kama taifa la Tanzania na bara zima la Afrika tujitafakari kidogo kwa kweli tupo nyuma kiulinzi.

Kwa hizi silaha wachina walizo amua kutuonesha japo nina mashaka kama wameonesha zote kabisa walizo nazo tupo nyuma sana ndugu zangu.

Tusijiongopee wakuu tumeachwa mbali sana hizi silaha tulizo nazo kwetu sijui hawa mabwana wameziacha store maana hapa sioni huu uchafu wetu naona vitu vizito vizito mpaka inatisha siku tukianzisha ka vita ka kirafiki sisi na wao maana kamanda wetu mmoja wa JW alisema sisi ni jeshi la sita kwa ubora😁

Ukitazama kwenye documentaries silaha walizokuwa wakitumia wachina wakati wanapambana na Japan na vita vya wenyewe kwa wenyewe ni magobore ya ajabu ajabu hata airforce walikuwa hawana wala jeshi la wana maji linalo jitambua ila leo wanaonesha vyuma vizito hapa.

Sisi bado tumejaza magobore
Kumiliki masilaha meeengi, makorokoro kibao na idadi kubwa ya askari ni jambo moja. Kazi inakuwa ipo kwenye swali la je, unavitumia kwa weledi wa kiwango gani??? Tazama Mrusi anavyohenyeshwa na kanchi kadogo Ukraine au Mataifa ya wale Kobaaz wanavyo chezea kichapo cha IDF.
 
Umesema kwa uchungu sana, hatuna mpango mkakata wa nchi ila tuna mipango mkakati wa kukaa madarakani kwa kipindi tunachokihitaji kwa manufaa binafsi. Hatuna mpango kama Nchi nini kifanyike na kiwe na faida hata kwakizazi kijacho tunajifikiri kushiba kwetu tu. Hatukubali kuanza kwa mpangilio na makubaliano tunakwenda kwa matakwa ya mtawala.
OK. Hilo ndilo linalosomeka hadharani machoni petu lakini ujue mambo mengine hususan ya Kijeshi huwa ni SIRI sio ya kuanika hadharani. Uwezo wa Jeshi hujulikana zaidi pale Adui Mchokozi anaposhikishwa Adabu tena adabu ya kudumu e.g. ilivyotokea kwa Iddi Amini Dadaa au wale jamaa wa Kibiti n.k..
Sio jambo jema sana kujilimbikizia masilaha ambayo kesho tu yameshapitwa na wakati na unarudi au utarudikununua mengine tena nayo yanakuwa vivyo hivyo. Unless ww uwe ni mtu wa vita-vita siku zote. Ni hayo tu.
 
Dunia iko kazi sana. Kwenye vita ya iraq tulikuwa tunashangaa drones za marekani na mandege tu. Sasa mpaka iran na uturuki wanayafyatua tu. Ukraine vile vidogo vinaundwa hadi home
Ni suala la Taifa kujiwekea Vipaumbele katika kila Sekta na muda wa Utekelezaji na Tathmini ya Viashiria vinavyopimika.
Vipaumbele vya Tz kwa sasa kwenye Maendeleo yetu sio lazima vifanane na vya nchi nyingine. au kwa lugha nyepesi Vipaumbele vya Familia yako sio Vipaumbele kwa Familia yangu na wala hatushindani vipaumbele vya kwangu na vile vya kwako.
 
Hakuna sehemu niliposema vipaumbele vyetu vifanane na vy nchi nyingine. Nnilichosema ni kwamba dunia iko kasi sana.
 
Hata kama mbona wahindi wana idadi kubwa hawajaendelea kama wachina...
Una uhakika? Unaijua India au unaandika tu ukiwa zako Kingugi? India ina teknolojia ambayo hakuna nchi ya Afrika inayo
 
Kama unailinganisha na Afrika sawa ila kama unailinganisha na mataifa yenye teknnolojia bado. Japo pia ina GDP kubwa sana, ila bado pia raia wake wengi wanaogelea kwenye lindi la umasikini, miundombinu mibovu, miji michafu n.k.
Ukitaka linganisha vitu linganisha vilivyonona.
 
Back
Top Bottom