Ninachoona kwenye Parade ya China Aisee! Kama taifa na bara tupo nyuma sana

Ninachoona kwenye Parade ya China Aisee! Kama taifa na bara tupo nyuma sana

Hawa wanaiba teknolojia za marekani hawana lolote.
 
Jeshi kutokuwa battle tested inaleta athari miezi michache ya mwanzo, baada ya hapo mtakipata cha mtema kuni.

Jeshi la North Korea lilipoingia vita ya Ukraine lilikuwa na performance mbovu miezi kama mitatu tu, baada ya hapo likafanya vizuri. Urusi ilianza vita kwa kukurupuka, miezi michache baadae ikaleta Wagner na wafungwa na mobilization na kuchukua silaha Iran na North Korea. After some time likawa stable.
Ukraine ilianza na casualties nyingi, na ukosefu wa silaha ikapata misaada, training na ikabadili mbinu na sasa iko stable.

Sasa China anaweza zalisha silaha hata 5 times ya Urusi, population anamzidi mbali, uchumi anamzidi mbali. Sasa huo uzoefu wa Urusi utaisaidia nini ukizingatia Ukraine sio hata robo ya uwezo wa China.
Unatolea mfano wa Ukraine inayosaidia kila kitu hadi mafunzo?
😂😂😂😂😂😂😂
 
Kupitia maonesho ya hii parade ya wachina kutimiza miaka 80 toka vita vya pili vya dunia baada ya kumnyuka Japan.

Kama taifa la Tanzania na bara zima la Afrika tujitafakari kidogo kwa kweli tupo nyuma kiulinzi.

Kwa hizi silaha wachina walizo amua kutuonesha japo nina mashaka kama wameonesha zote kabisa walizo nazo tupo nyuma sana ndugu zangu.


Tusijiongopee wakuu tumeachwa mbali sana hizi silaha tulizo nazo kwetu sijui hawa mabwana wameziacha store maana hapa sioni huu uchafu wetu naona vitu vizito vizito mpaka inatisha siku tukianzisha ka vita ka kirafiki sisi na wao maana kamanda wetu mmoja wa JW alisema sisi ni jeshi la sita kwa ubora😁

Ukitazama kwenye documentaries silaha walizokuwa wakitumia wachina wakati wanapambana na Japan na vita vya wenyewe kwa wenyewe ni magobore ya ajabu ajabu hata airforce walikuwa hawana wala jeshi la wana maji linalo jitambua ila leo wanaonesha vyuma vizito hapa.



Sisi bado tumejaza magobore
 
China akuna demokrasia wanapataje maendeleo kwa kasi wakati tunaambiwa demokrasia ndio maendeleo yanapopatikana?
 
Mkuu 'Mi mi', mimi nina machache tu ya kuchangia kwenye mada yako hii.
Kwanza nikuulize; umewasiliana na watu muhimu katika taifa letu hili kama akina David Kafulila, akina kitila Mukumbo wakueleze maono yao ya kihistoria kuhusu mwelekeo wa taifa hili?

Ungekuwa umefanya hivyo, ungetambua kuwa Tanzania inaandaliwa tu kuwa ni nchi ya watwana. Hili kamwe haliwezi kuwa taifa lenye ndoto kama hizo unazo zinshangila kwa wachina.

Ninayo mengi sana ya kukueleza kuhusu mada yako hii, lakini ngoja nikuache tu utafakari hayo machache niliyo dokeza. Natumaini utanielewa vizuri. nisisitize tu kwa mara nyingine: Usitegemee hata mara moja kwa taifa hili kupiga hatua ya kuelekea huko unakokuona kwa kutegemea uongozi mbovu kabisa kama huu tulio nao sasa hivi ndani ya taifa letu.
Na mbaya zaidi, hawataki tuwaondoe madarakani!

Lakini
Moja ya comment bora sana ndani ya huu Uzi..


(Asomaye na afahamu)
 
Moja ya comment bora sana ndani ya huu Uzi..


(Asomaye na afahamu)
Inaumiza moyo sana mkuu kuona taifa letu hili lenye kila kitu kuwa taifa la kuheshimika duniani; lakini tunaburuzwa kwenye matope na hawa watu wasiokuwa na uzalendo wowote ndani ya DNA zao!

SitaKI tuige kila jambo kwa mifano ya nchi ambazo tunaona zimepiga hatua.
Kwa mfano hakuna njia tunayoweza kuwa Marekani, China, Urusi; na hata viinchi vilivyo wahi kututawala.

Lakini nataka kutolea mfano ambao najuwa propaganda nyingi za magharibi zinapotosha kila kitu juu ya ki-nchi hako; au basi niseme vi-nchi hivyo vyote viwili kwa pamoja kuonyesha kuwa Tanzania inaweza sana kuwa juu kabisa.
Mfano wasioutaka waTanzania wengi ni hii Korea Kaskazini. Mfano wanoo utaka karibu wote wenye kuitakia mema Tanzania ni Korea Kusini.

Jiulize, Tanzania haiwezi kweli kuwa bora zaidi ya hizi nchi mbili; tunapochukua mazuri kila upande wa nchi hizo?

Raslimali watu tunao wa kutosha; raslimali ambayo viongozi wetu wanaididimiza kabisa kwa kuiendeleza na kuitumia vibaya.
raslimali mali hizo nchi mbili zinatuzidi nini?

Tahadhali: Kama huijui Korea Kaskazini; jaribu kuisoma nje ya propaganda za Magharibi au washindani wao wa Korea Kusini. Si muhimu tuige baadhi ya mtindo wa utawala wao; lakini kama nch wapo juu kuliko tulivyo sisi pamoja na vikwazo vingi walivyo wekewa na wakubwa duniani.
 
Mkuu mbona wewe na majirani zako mmetofautiana uchumi kwenye maisha ya kawaida? Na ndiomana umeme ukikatika ndani kwako unatoka nje kuhakikisha hiyo ni dalili ya umasikini na roho mbaya! Muhim tujitahid kupigania ugari wetu
 
Weka hiyo clip Jeshi la Marekani haliwezi fanya Military parade kwa amri ya raisi hadi bunge la congress liithinishe hiyo itakuwa sio mikitary parade itakuwa ya jeshi la mgambo

Trump hana mamlaka yeyote ya kuamuru jeshi chochote iwe mikitary parade au kutaka Jeshi liingie vitani bila kibali cha bunge la Marekani yaani Congress

Ubavu huo hana

Onyesha na kibali cha Congress kilichoruhusu Military parade jeshi la Marekani lifanye
Inaonekana bado umelala usingizi mzito sana
 
Hata kama mbona wahindi wana idadi kubwa hawajaendelea kama wachina...
Wahindi walikuwa mbele ya China baada ya uhuru.Lakini India iliendekeza Uingereza kuitwa Sir,MBE,na utamaduni wa siasa za Magharibi. Vipaji hadimu vya kihindi vikakimbilia Canada,Uingereza, Marekani n.k.Kibaya zaidi wakaendekeza ubaguzi wa dini,koo n.k
Wamekumbuka shuka asubuhi,wanashangaa speed ya maendeleo ya China,kawapita kwa mbali sana wamebakia kutingisha kichwa.
 
Back
Top Bottom