Kupitia maonesho ya hii parade ya wachina kutimiza miaka 80 toka vita vya pili vya dunia baada ya kumnyuka Japan.
Kama taifa la Tanzania na bara zima la Afrika tujitafakari kidogo kwa kweli tupo nyuma kiulinzi.
Kwa hizi silaha wachina walizo amua kutuonesha japo nina mashaka kama wameonesha zote kabisa walizo nazo tupo nyuma sana ndugu zangu.
Tusijiongopee wakuu tumeachwa mbali sana hizi silaha tulizo nazo kwetu sijui hawa mabwana wameziacha store maana hapa sioni huu uchafu wetu naona vitu vizito vizito mpaka inatisha siku tukianzisha ka vita ka kirafiki sisi na wao maana kamanda wetu mmoja wa JW alisema sisi ni jeshi la sita kwa ubora😁
Ukitazama kwenye documentaries silaha walizokuwa wakitumia wachina wakati wanapambana na Japan na vita vya wenyewe kwa wenyewe ni magobore ya ajabu ajabu hata airforce walikuwa hawana wala jeshi la wana maji linalo jitambua ila leo wanaonesha vyuma vizito hapa.
Sisi bado tumejaza magobore