Ninachoona kwenye Parade ya China Aisee! Kama taifa na bara tupo nyuma sana

Ninachoona kwenye Parade ya China Aisee! Kama taifa na bara tupo nyuma sana

anafananisha na nchi ambayo ukiamka maneno mawili tu ndio yanatrend "Mama" na "kizimkazi" wakati China trending words ni AI na Machine learning. Huku kila kitu kizuri kafanya mama, kule mifumo mizuri ndio inafanya vizuri..... Aisee hatari sana mkuu...
Xi Jinping kafanikisha mitano tena oktoba kwa Xi tunatiki😀
 
Brother ulikuwa ujui hayo kwamba tuko nyuma sana sana. Afrika kuna kitu ambacho hatukielewi. Tumekaa kama watu wsiojielewa vile. Lakini ninaona shida kubwa sana kwetu ni elimu. Hatuna elimu ya kutuwezesha kujikomboa na zaidi sana tumekuwa na viongozi wabovu sana.
Hakika mkuu
 
Ukitazama Ile event simchezo midege inaelea angani kama kunguru midege kibao

Nikawa Nina jisemea kimoyo moyo kwahayq anayo yqfanya china na sisi tunayo yqfanya katika siku ya uhuru hakika tunayo yqfanya inatosha kuwa comedy Huko Duniani 🤣🤣
Tundege twetu sijatuona leo sijui vipo store vinapigwa na vumbi huko kwenye makambi ya wachina maana hapa naona mandege mazito tu
 
Wakuu tupo nyuma sana kuna vyuma unaviona hapa unasema hawa jamaa wakiamua kuwa serious kimabavu sisi tuwe makoloni yao hakuna wa kuzuia
Hakuna kipya hapo. Sisi bado tunamsifia fisadi kama Rostam eti ni ''business magnate'' kwa nini tubaki nyuma? China huyu angeshauawa siku nyingi. Usione vyaelea... watu wanafanya kazi. Kwetu tunakimbilia kuvaa saa za gharama na kununua Rolls Royce.
 
wachina wamewaonesha ulaya na marekani silaha zao,,,wamezitengeneza wenyewe kwahiyo siri ya ufanisi wa hizo silaha wanazijua wenyewe😀
 
Bado miezi 3 tu tukashuhudie la kwetu la Kuvunja Matofali na kushuka kwa miavuli,9 dec.2025!
Kila mwaka linafanyika kutishia vyama Upinzania.
Kwamba jeshi letu lipo mahususi kupambana na Chadema kuliko kulinda nchi aisee kazi ipo
 
Hakuna kipya hapo. Sisi bado tunamsifia fisadi kama Rostam eti ni ''business magnate'' kwa nini tubaki nyuma? China huyu angeshauawa siku nyingi. Usione vyaelea... watu wanafanya kazi. Kwetu tunakimbilia kuvaa saa za gharama na kununua Rolls Royce.
Kazi ipo
 
Mkuu usitishwe kabisa na hayo manyanga field ni something extra mkuu muulize urusi wiki mbili ZIMEKUA miaka mingapi?


Fullstop, kwishaaa
 
Kama taifa la Tanzania na bara zima la Afrika tujitafakari kidogo kwa kweli tupo nyuma kiulinzi.
Si sawa hata kujilinganisha nao, wa ni nchi ya viwanda ikiwepo silaha, sisi walaji tu. Tutajivunia kuwa na silaha kali toka kwao.
 
Wameamua kuweka watu sahihi mahali wanapostahili,Sasa hivi ulendeleo wa kijinga umetuzidi waafrica ,kama watoto wenye vipaji na akili wapo ila hatutaki kuwaendeleza badala yake ni rushwq na upendeleo vimetamalaki
 
Mkuu 'Mi mi', mimi nina machache tu ya kuchangia kwenye mada yako hii.
Kwanza nikuulize; umewasiliana na watu muhimu katika taifa letu hili kama akina David Kafulila, akina kitila Mukumbo wakueleze maono yao ya kihistoria kuhusu mwelekeo wa taifa hili?

Ungekuwa umefanya hivyo, ungetambua kuwa Tanzania inaandaliwa tu kuwa ni nchi ya watwana. Hili kamwe haliwezi kuwa taifa lenye ndoto kama hizo unazo zinshangila kwa wachina.

Ninayo mengi sana ya kukueleza kuhusu mada yako hii, lakini ngoja nikuache tu utafakari hayo machache niliyo dokeza. Natumaini utanielewa vizuri. nisisitize tu kwa mara nyingine: Usitegemee hata mara moja kwa taifa hili kupiga hatua ya kuelekea huko unakokuona kwa kutegemea uongozi mbovu kabisa kama huu tulio nao sasa hivi ndani ya taifa letu.
Na mbaya zaidi, hawataki tuwaondoe madarakani!

Lakini
 
Mzee sio poa wale Jamaa wapo well trained
 
Back
Top Bottom