Mimi Sisyphus leo, nimeliona joto la jiwe ... mtu nilimuamini ameanza rasmi kuonyesha MAKUCHA yake ... ni miaka minne sasa niko na huyo mwanamke, ni muda mrefu sasa mwenzangu alikua anaomba ndoa mara nyingi sana..nimejaribu kumuelewesha asubiri tujipange kwanza (na najipanga kweli sio uhuni) .. maana tushamleta na mtu duniani, naona sasa muda wa uvimilivu wake umaenza kufika kikomo ....
Story inaanzia kati, leo alienda kutafuta chumba mana kuna short course alikua anataka kusomea kwahiyi ikambidi akatafute chumba sasa amefika dalali akamwambia asubiri mama mwenye nyumba arudi kwahiyo itambidi akae masaa matatu kumsubiri... akanipa taarifa mimi nikaona hakuna logic ya kumsubirisha mana anakoishi(siishinae) amecha mtoto ( 1.9 year) basi bwana nikampigia dalali , dalali akaanza kuropoka “ ooh bro msiondoke mana mkiondoka hiki chumba mtakikosa” ... la haula ikabidi ni muulize nisiondoke na nani, akajibu “ we si yule jamaa mumewe ambae uko nae” bila kufikiri mara mbili nikajibu hapana mimi ni mumewe ila sipo huko.
Dalali akaanza kuuma uma maneno mwisho akasema aaah basi ngoja kidogo nitaku-check ... nikamuambia embu subiri nipe maelezo kidogo huyo mwanamama amekuja na nani? ... kwa sababu alishaanza ikabidi aseme amekuja na jamaa akamtambulisha ni mumewe ( mimi nilipo ikabidi nikae chini kwanza ) ... lakini dalali akaendelea itakua basi boda... nikamwambia sawa fatilia hilo swala la mama mwenye nyumba kwanza.
Nikatulia kwanza alafu nikamtafuta vipi mwenzangu leo umeenda na nani? Mara ooh sijaenda na mtu mara oohh ni boda ndiye niliyemtambulisha mume wangu ... kwa kifupi taarifa aliyonipa dalali ni kwamba walienda wawili na aliwaacha wawili ukiacha boda.
Ikanibidi nimuulize vizuri boda ndio unamtambulisha mumeo ,? ( ...ghafla akaanza ule mchezo wao anakurudishia maswali kwani wewe huniamiani blah blah).
Baada ya haya ikabidi nianze ku-analyse wapi nilikosa umakini mpka nikashindwa kuona hili kwa hupitia uwezo wa roho mt. nikaanza kuona vingi nilivyokua sitilii maananini kwanza AMEACHA KUSISITIZIA NDOA , pili amepunguza wivu na anakaribia kuacha kabisa , tatu amekua na majibu ya mkato na kujifanya anajiamini( now days ana-vihela mana kuna-business nilimpa akaweza ku-make kwa kipindi kifupi).
Nne .. kuna mambo anayafanya mwenyewe mwenyewe na hua tunashirikishana kila kitu ila nimeanza kuona gap upande wa pili
NB: huyu mwana-mama nimefanya nae vitu vingi sana hata kipindi na mpiga tarehe anafaham hasa nini nilikua nafanya, nilivyofanya na naendelea kufanya . MAAZIMIO shetani amenijia na ujumbe wa kumpiga chini mapema maana nilivyokua nafanya nafanya kwa ajili yetu sote isingekua hivyo mi ningeenda zangu SHULE KITAAMBO nikabukue zangu masters ya masimulizi...
WAJAMENI ...nipeni ushauri mana shetani ananizonga na mawazo yake... ni chukue hatua gani easy way , hard way Au mixing