Ninahisi nimepata gonjwa la zinaa ila dawa zote zimedunda

Ninahisi nimepata gonjwa la zinaa ila dawa zote zimedunda

Wingi huo wa dawa ulizopewa unaonesha gonjwa lenyewe halisikii dawa limekuwa sugu. Aliyekupa hizo dawa anabahatisha tu hana uhakika. Je umefanya "culture and sensitivity" kuona dawa ipi sahihi kwa tatizo lako? Vinginevyo endelea kutwanga maji kwenye kinu utapata unga safi mwishoni!
Nimefanya hyo culture hata kwenye list ya vipimo hapo nimeiweka lakini haikuonyesha chochote
 
Daktari alishawai niambia kua huyu Hana tatizo lakin ni mchafu haogi tu...
Nilipigwa nabutwaa siogi kivipi wakt nidesturi yangu kuoga KUMBE hakumaanisha hivyo aisee
Sometime nicode tu yaupande wapil
Maana yake ni usafi kwa mwanamke sio
 
images (4).jpeg
 
sio candidiasis kweli hiyo? kachome penadu chupa 5 ,kila baada ya wiki chupa 1 afu utumie azuma na ampiclox, NB HAKIKISHA MKE WAKO NA MICHEPUKO YAKO INATIBIWA.kuna jamaa nilimtibu kwa dawa hizi nayee ute ute ulikuwa unatoka na kichwa cha uume kuwasha washa
 
sio candidiasis kweli hiyo? kachome penadu chupa 5 ,kila baada ya wiki chupa 1 afu utumie azuma na ampiclox, NB HAKIKISHA MKE WAKO NA MICHEPUKO YAKO INATIBIWA.kuna jamaa nilimtibu kwa dawa hizi nayee ute ute ulikuwa unatoka na kichwa cha uume kuwasha washa
Sawa mkuu, tatizo madokta wanatofautiana ukienda anakutibia tofauti labda uwe recommend kutoka hospital inayojulikana
 
Kwa kweli nikiona tundu linalotoaa harufu siielewi kwa kweli hua navaa boxer yangu na mchezo unaishia hapo,
 
Nimefanya hyo culture hata kwenye list ya vipimo hapo nimeiweka lakini haikuonyesha chochote
Ulichofanyiwa ni urine culture. Iwapo waliifanyia sensitivity test kuona mchanganyiko upi wa dawa unafaa basi utakuwa una tatizo la usugu wa dawa. Je unatibiwa wewe tu au pamoja na mwenzi wako? Nyote wawili lazima mpate matibabu ili kuzuia msiambukizane. Kujitibu peke yako bila kuwa na mwenzio yaweza kuendeleza tatizo hili.
 
Ulichofanyiwa ni urine culture. Iwapo waliifanyia sensitivity test kuona mchanganyiko upi wa dawa unafaa basi utakuwa una tatizo la usugu wa dawa. Je unatibiwa wewe tu au pamoja na mwenzi wako? Nyote wawili lazima mpate matibabu ili kuzuia msiambukizane. Kujitibu peke yako bila kuwa na mwenzio yaweza kuendeleza tatizo hili.
Mwenzangu tumetibiwa wote kwa awamu mbili. Dozi ya siku kumi ikadunda na sindano za siku 5 pia hazikuleta matokeo. Dawa zote zinakupa nafuu Ila hauponi
 
Wakuu habari ya leo, kwa miezi kadhaa nimehangaika na ugonjwa ambao hapo chini nimeweka dalili ninazozipata, vipimo na dawa nilizotumia lakini bado sijapata suluhisho. Kama kuna mwenye uzoefu naomba msaada.

Dalili.
1.Maumivu kwenye mrija wa mkojo karibu na kwenye kichwa cha uume(hii ni kawaida bila kukojoa). wakati wa kukojoa mkojo unagawanyika na kutoka kama njia mbili na sisikii maumivu Ila mkojo wa mwisho ukiisha ndo unasikia maumivu yanaendelea na unakuwa Kama umechochea
2 .Maumivu ya korodani, na mishipa yake pamoja na ile inayoenda chini karibia na sehemu ya haja kubwa
3. Maumivu ya nyonga
4.maumivu ya kiuno(mara chache sana)
5. kutoka ute ute mweupe kwenye uume wakati wa haja kubwa
6. Unaamka asubuhi unakuta boxer imelowa kana kwamba uliota unafanya sex then uka ejaculate vitu Kama sperm lakini sio vipo kama kamasi fulani hivi na vinateleza. lakini katika hali ya kawaida sioni hvyo vitu vikitoka.

VIPIMO vyote nilivyopima vinaonyesha hamna chochote na dawa zote huwa zinanipa nafuu na wife pia ametumia. huwa nikipata nafuu nakaa Kama wiki hv Ila nikikutana na mwenzangu hali inarudi tena sasa sijajua tatizo n nn au dawa ninazopewa sio. kuna docta aliwahi niambia nimepata klamidia japo hakunipima na akanipa dawa lakini bado haikusaidia.

VIPIMO
1.Urinalysis
2.Ultrasound(kibofu,tezi dume,kongosho,figo,ini)
3.Urine Culture
4.Ultrasound (korodani)
5.VDRL
6.Full blood picture
7. Urinalysis + VDRL(twice)
8. Urinalysis+ Ultrasound (tezi dume&figo)


DAWA
1. Cipro+PCM siku 5
2. Amoxclav siku 5
3. Azithromycin siku 6
4. Gentamycin 160mg siku 5
5. Doxycycline+metrodinazole siku10,
cefixine kidonge kimoja tu
6. Ceftriaxone siku 5
7. Azithromycin siku 3
8. Ceftriaxone+getamycin (80mg) mara mbili kwa siku, kwa siku 4(sindano 16)
9. Tribulent PCM, siku 5
10. Ceftriaxone 2g+getamycin (once)+Cipro (7 days)+ ibuprofen
Kapime HIV acha ujinga ,utakufa
 
buda17 ushauri wangu: Nenda kwa YESU!! Yeye ni mponyaji wakati wengine wote hutibu tu!! Focus yako iwe kwa YESU na si kwa WAOMBEAJI!! Anzas hivi: 1. Fanya toba ya dhati, mwombe Mungu akusamehe dhambi zako zote unazozikumbuka na ambazo huzikumbuki. Fanya toba kwa kinywa chako ukiwa unamaanisha na ukiwa na dhamira ya kutokuzirudia tena!! kusudia hivyo kwa dhati katika moyo wako!! Katika toba hii kwa kinywa chako na sauti yako MKARIBISHE YESU katika moyo wako awe BWANA na MWAKOZI wa maisha yako. Mwombe YESU akutie nguvu za kushinda dhambi, na akaushe tamaa yote ya dhambi katika maisha yako. Kama ukifanya toba hii kwa dhati ukiwa peke yako katika mazingira ya utulivu, YESU Kristo ataingia katika moyo wako, atakusamehe dhambi zako, utajua moyoni kuwa umesamehewa dhambi zako na utapata furaha na amani ya kweli, na utakuwa UMEOKOKA. 2. Kwa kinywa chako na sauti yako mwombe YESU uliyempokea na ambaye sasa yuko moyoni mwako, akuponye magonjwa yako yote unayoyafahamu na usiyoyafahamu huku ukiwa umeweka mikono yako sehemu unayoumwa. 3. Baada ya maombi haya amini kwa moyo wako wote kuwa YESU AMEKUPONYA, hata kama dalili za ugonjwa bado unazo!! Ujue kuwa ugonjwa ni roho!! ndiyo iliyokuwa inautia nguvu ugonjwa. roho ya ugonjwa imeondoka wakati huo huo ulipoomba. Kwa kuwa kilichokuwa kinautia nguvu ugonjwa kimeondoka, dalili za ugonjwa aidha zinaweza kutoweka wakati huo huo au zinaweza kutoweka taratibu kwa kadri muda unavyokwenda. Vyovyote utakavyojisikia ukweli ni kwamba UMEPONA na ni suala la muda tu na uponyaji wako utakuwa dhahiri!! 4. Waambie watu wako wa karibu kuwa UMEOKOKA na UMEPONA, YESU AMEKUOKOA na AMEKUPONYA. 5. Tafuta kanisa la watu waliookoka lililo karibu na wewe na ukawe mshirika hapo. Waambie jinsi ulivyookoka na kupona. Yako makanisa mengi ya watu waliookoka, na mimi napendekeza kwako kanisa la TANZANIA ASSEMBLIES OF GOD (TAG). Na kama ukiukubali ushauri huu na kuamua kuutendea kazi niko tayari kuendelea kukushauri na kukufundisha mambo mengi yamhusuyo MUNGU. Nimekushauri ufanye mchakato huu peke yako ili imani yako iwe kwa YESU na si kwa WATU au kwa "vifaa vya kiroho" kama maji ya upako, mafuta ya upako nk ambavyo huwa havina matokeo ya kudumu katika moyo wa mtu. Kwa msaada zaidi karibu pm.
 
Back
Top Bottom