Facts are stubborn things. Tanzania ni nchi moja ya JMT yenye uraia mmoja, na raia wote wana haki sawa ndani ya JMT.
Yes Tanzania ni nchi moja kwasababu ya Uraia unaothibitishwa na utaifa na Diplomasia.
Swali ni je, kwa Uraia uliopo unatekelezwa kwa vigezo vya Uraia sawa!
Mfano, Raia wa Tanganyika wanajulikana kama Watanzania hutawasikia Wakigoma, Wamtwara au Watanga.
Raia wa Zanzibar wanajulikana kama Wazanzibar wakiongozwa na sheria tofauti na za JMT.
Raia wa Tanzania Bara ambayo kikatiba imetambuliwa kama Tanganyika wanaweza kufanya shughuli popote pale katika eneo la Tanganyika ikiwemo Biashara, Uwakilishi katika ngazi zote, kuanzia mitaa, udiwani, Ubunge n.k.
Raia wa Tanganyika wanaweza kumiliki ardhi eneo lolote la Tanganyika lna kufanya shughuli bila kikwazo
Raia wa ''Tanzania'' kutoka Zanzibar anazo haki zote zilizoanishwa hapo juu ndani ya Tanganyika .
Raia wa 'Tanzania' kutoka Tanganyika hana haki nilizo zitaja hapo awali kule Zanzibar.
Kuna mgao mahususi wa fedha, mipango, Mikopo na misaada kwa Raia wa Zanzibar.
Wapi kuna mpango mahususi wa aina hiyo kwa Raia wa Kigoma, Mtwara, Musoma au Singida?
Raia wa mkoa wa Dar es Salaam wanawakilishwa na Wabunge takribani 8 kwa idadi ya Watu milioni 5
Raia wa Zanzibar wanawakilishwa na Wabunge takribani 80 wanaochaguliwa na watu 2500 kwa jimbo.
Wabunge wote wana kura sawa ndani ya Bunge.
Hii ina maana moja Raia wa 'Tanzania' Zanzibar wana maamuzi na turufu ndani ya Bunge ikiwemo mambo yasiyowahusu ya Tanganyika licha ya uwakilishi mdogo kuliko Diwani wa kata moja ya Tanganyika.
Huioni nguvu ya Raia wa Zanzibar
Hakuna taasisi ya umma kule Zanzibar ikiwemo elimu na Afya na mamlaka au idara zote inayoweza kuajiri Raia wa ''Tanzania ' kutoka Tanganyika kwa vile kuna kifaa cha Ubaguzi kinachoitwa Ukaazi'.
Kitambulisho cha Ukaazi kule Zanzibar ni cha nini ikiwa ni Raia wa nchi moja wenye vitambulisho vya NIDA!
Yes muundo wa muungano wetu adhimu unaruhusu. Muungano wetu ni muungano very unique, kwa upande mmoja ni muungano wa nchi mbili zimeungana kwa union kuunda nchi moja ya JMT yenye uraia mmoja, rais mmoja na Amiri jeshi Mkuu mmoja.
Raia kwa kupitia sheria zao ndio wanaotengeneza mamlaka za JMT kama serikali na Bunge.
Je, Waziri mkuu wa Tanzania ana mamlaka kule Zanzibar?
Ikiwa hana, huyu Waziri mkuu ni wa nchi gani ambayo kuna mipaka ya kazi zake ndani ya JMT
Lakini pia jiuilize ni kweli Waziri mkuu hana mamlaka? Je, muundo wa muungano unasema hivyo?
Ndani ya muungano, muungano wetu ni federation ya nchi mbili, Tanzania bara na Tanzania Visiwani au Tanzania Zanzibar, zenye marais wawili. Sehemu moja ni cha wote, sehemu nyingine ni kwa wenye kitambulisho cha ukaazi.
Sina uhakika kama unafahamu 'Federalism'. Kwa minajili ya mjadala tukubaliane nawe.Ikiwa kuna Tanganyika na Zanzibar, Tanzania ndiyo national government. Zanzibar ina serikali yake, ipi ni ya Tanganyika katika Federal unayoongelea? Unakuwaje na ''one entity'' ukawa na Federation. Hapa nitahitaji elimu yako ya Federation !
Uraia ni mmoja, ila sehemu nyingine ina ukaazi besides uraia!.
Hili la Uraia mmoja mbona halina tatizo! kwanini unakazia mstari huo na huendelei kuwashawishi sisi 'Wajinga' kuhusu concerns zetu. Nilitegemea usema Uraia ni mmoja ndiyo maana hoja zao znajibika abcd
Ujinga wao ni kujidhania raia wa upande mmoja, wana haki zaidi kuliko raia wa upande wa pili.
Hivi huoni kwamba Raia wa Zanzibar wana haki zaidi ya wale wa Tanganyika?
Kwa kutumia Utanzania Raia wa Zanzibar hawabaguliwi wakiwa Tanganyika.
Kwa kutumia Katiba na sheria za Zanzibar, Raia wa Tanganyika hawana haki Zanzibar
Na hapa ndipo kuna msuguano. Kwa mfano, suala la Bandari Zanzibar wanasema haliwahusu.
Mapato ya Bandari za Tanganyika yanalipa mikopo na madeni ya JMT ambayo Zanzibar ni mnufaika, yanagharamia muungano ambazo Zanzibar na yanayoingia BoT ambako Zanzibar wanachota 4.5%.
Kwa kutumia Utanzania, Wazanzibar wanapewa fursa 21% ya ajira zisizo za muungano kama ilivyo kwa Makame Mbarawa, Shaka Hamdu na maelfu yao.Kwa kutumia sheria za Zanzibar Watanganyika hawana nafasi hiyo Zanzibar.
Kwa kutumia Utanzania, Wazanzibar ni wanufaika wa hazina ya ardhi, kwa kutumia Uzanzibar Watanganyika hawana nafasi Zanzibar wakiambiwa ni Wageni. Usawa wa Uraia upo wapi?
Mapato ya gesi ya Mtwara, Dhahabu ya Chunya, Almasi ya Shinyanga, Mawese ya Kigoma, Tanzanite ya Arusha n.k. yanaingia katika pato la Taifa kisha kugawiwa miongoni mwa Raia wa Tanzania.
Mapato ya Tanganyika yanagharamia Muungano (Zanzibar 0%), yanafidia bajeti ya SMZ yanatoka 4.5% kila mwezi kwa Zanzibar. Hivi hawa Raia wa Zanzibar wana umuhimu gani tofauti na Raia wenginE?
Hoja kubwa ambayo hutaki kuwaelewa 'Wajinga' si Uraia sawa! Unaweza kutamka Raia wote ni sawa na ikawa.
Hoja ya Wajinga ni kwamba, kwavile kuna sehemu ya Tanzania inayojulikana kama Zanzibar iliyopewa nguvu zake kwa baadhi ya mambo, tunahitaji Serikali ya Tanganyika itakayosimamia mambo yake.
Ikiwa ni lazima tunaweza kuwa na shirikisho (Federal) la Tanzania kama alivyoeleza Mzee Warioba.
Ikiwa haiwezekani kuna hiyari ya kuishi kama majirani.
Wajinga wa Tanganyika wanasema hivi URAI isiwe sababu ya kuwatwisha Zigo.
Urai usitumike kuhalilisha 'nataka, nipewe na mimi'
''Mambo ni mengi muda mchache ''