Pre GE2025 Ninawapongeza CHADEMA kwa maoni yao ila hoja namba 5 ni ya ovyo

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Akili kubwa
 
Wewe nilishasema utakuwa sawa mpaka urejee tena hospitalini kumalizia matibabu ya magonjwa ya akili yanayokusumbua. Lakini pia ni lazima uache kuvuta mibangi yako.
Mtoto wa mkesha wa mbio za mwenge kwahiyo babako ni Mwenge
 
Kila jimbo liwe na Me na Ke? Hii ni kitu gani jamani? Hebu tuwe serious jamani, me na ke kila jimbo ili iweje, kwa faida ya nani? Kwani kinachoangaliwa ni nini kwa hao wawakilishi wa wananchi?
 
Mkuu majimbo yako 264 kwahiyo wakisema waweke huo usawa tutakuwa na wabunge 528 wa kuchaguliwa ambao ni zaidi ya hawa waliopo. Utakuwa ni mzigo mwingine mzito kwa wananchi.
Viti maalum hatuwahitaji kabisa bungeni maana kazi yao ni kupiga vigeregere tu
 
Sasa vikao vipungue lakini wabunge wajazane
 
Ccm lazima itoke madarakani
 
Hoja ya CDM ya majimbo kupitiwa upya na kupangwa na Tume Huru Ya Uchaguzi kulingana na idadi ya watu hujaiona?
Hawezi kuiongelea maana ni hoja ya kujenga na siyo ya kubomoa
 
Hili ni wazo la Kijinga kutolewa na Chama cha Chadema.....
 
Idadi ya wabunge haina uhusiano na maendeleo maana hata hawa 300 hawareflect maendeleo tulio nayo. Ni mzigo tu kwa walipa kodi na kuongeza ulaji tu. Hata viti maalum ingefutwa tu ili watu haijalishi jinsia wakagombee tu kwenye majimbo.
Hajaeleza impact ya hao Wabunge wawili kila Jambo ktk Maendeleo ya Jimbo....
 
Kumbuka kuna suala la kupunguza idadi ya majimbo ya uchaguzi na posho
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…