Ninayoyaona KKKT nimegundua Kanisa Katoliki ndilo kanisa la Kweli

Ninayoyaona KKKT nimegundua Kanisa Katoliki ndilo kanisa la Kweli

Haya yapo hata Kwa Maustadh na Mashehe ni tabia ya mtu.Kuna mtu ana wanawake wanne lakini Bado ana michepuko hapo utasema Waislamu Malaya?Bali ni tabia ya mtu.Nyakati zitakuja ambalo Waafrika tutarudi kwenye Dini zetu tukiachana na hizi futuhi za Waarabu na Wazungu.
Sahau kabisa hili jamaa yangu waafrika kuirudia asili yetu ndiyo basi tena
 
Hakuna kanisa la kweli Duniani!!

Roma ni serikali na dola kamili inayotawala Dunia KWA utaratibu wa siri wala haihusiani na kanisa wala MUNGU muumba!!

Dini ni kivuli cha kupitisha agenda zao kwenye mataifa mbali mbali Duniani!!

Hiyo migogoro ya makanisa MENGINEYO ni mkono wa serikali kupitia Roma,pale wanapoona kanisa fulani linatishia maslahi ya serikali ya kirumi Duniani kote!!

Elewa hivyo itakusaidia sana kuliko unavyofikiri!!

Kuna MUNGU wa kweli hakuna Dini ya kweli,kuna imani ya MUNGU wa kweli hakuna kanisa au dhehebu la kweli Duniani yoote ni mipango ya serikali za siri Roma ikiwa mojawapo!!

Elewa hivyo mkuu itakusaidia kujua migogoro yote ni mipangokazi ya serikalitba Dini,madhehebu yote ni sehemu ya mpangokat wa serikali hii unayoiona!!!

Uwe huru
We mpumbavu unashinda njaa huko kwenu halafu usingizie Roma?migogoro isiyokua na idadi KKKT Roma ndio inasababisha?
 
Unachokikataa ndio unachokiishi, Jitambue.

Dini yako ni Uislam na unasema dini pekee ni Mnyazi Mungu, unapomwabudu Mwenyezi Mungu huwezi kukwepa dini, dini ni kama njia ya Kumwabudu
Naam, dini kwa Mwenyeezi Mungu ni Uislam tu.

Labda huelewi maana ya neno dini. Ukristo siyo dini, ni imani tu za wazungu za wagawe uwatawale.

Wenyewe waliwaletea Ukristo sasa wanayageuza makanisa kuwa Misikiti.
 
Naam, dini kwa Mwenyeezi Mungu ni Uislam tu.

Labda huelewi maana ya neno dini. Ukristo siyo dini, ni imani tu za wazungu za wagawe uwatawale.

Wenyewe waliwaletea Ukristo sasa wanayageuza makanisa kuwa Misikiti.
Sawa kabisa. Ukristo sio dini.

Sasa hebu niambie DINI NI NINI kwa mujibu wa Kamusi/Dictionary?

Kwenye hili swali FaizaFoxy huwa anatia huruma sana.[emoji1787]

Hawezi kulijibu KAMWE. Kwa sababu ukweli anaujua na anajua akijibu kama nilivyouliza Propaganda yake itakufa natural death.
 
Luther wakati mama yake anafariki alikiri ya kwamba 'ni bora kuishi kama mprotestanti na kufa kama mkatoliki'
 
Nyie wagalatia Njaa zitawaua
Duuu nyinyi mlifikiri Shetani ni Allah tu na kwa Mtume Wake ni Mohammad pekee🙃 Msicho jua Shetani anatumika DINI kupotosha huu Ulimwengu na ndyo maana Biblia inamuita MTAWALA wa Ulimwengu huu ( John 16:11).
Na katika Ufunuo 17:1-2 Biblia inaziita Dini zote za Uongo Kahaba ikimaanisha zinadai kumfuata yule Mungu wa Kweli na Wakati huo huo zikijichanganya na Serikali ambazo kimsingi zimejaa ufisadi na kufanya maisha ya watu wa chini magumu.
Katika Ufunuo 17:16&17 Biblia inasema Mungu hatimaye atatia kwenye mioyo ya Viongozi wa Serikali hizi ambazo hizi Dini hujichanganya nazo ili hizo Serikali ziziharibu hizo dini zipotee milele (za kiislam, Kikiristo, kiyahudi na hata Hindu).
Biblia itabaki ya kweli hizo Dini zenu zinawapoteza
Mabishano ya kidini ni ujinga na kipimo cha uelewa mdogo.
Uislam pekee.

Hakuna mfumo kama wa kanisa kwenye Uislam. Uislam ndiyo dini pekee kwa Mwenyezi Mungu. Kila kitu ni wewe na Muumba wako tu.
Mtuombee tu sio sisi na Wala sio matakwa ya walutheri ni CCM wametuzidi kete
Ulikuwa hujagundua?
Mwanzo nilijua hili kanisa la kkkt ni level moja na Katoliki lakini kumbe ni KICHUGUU NA KILIMANJARO. Sasahivi nimekuwa mtu mzima ndio najua Kanisa Katoliki halistahili kufananishwa na makanisa mengine, yaani Katoliki ni kanisa la kipekee sana na MISINGI YAKE ILIWEKWA NA MMOJA WA WANAFUNZI WA YESU NA YESU NDIYE ALIYETOA TAMKO LA KWAMBA KTK MWAMBA HUU NITALIJENGA KANISA, NA HAKIKA NDILO HILI SASA.

Tofauti na LUTHERAN AMBALO MISINGI YAKE IMEWEKWA NA MARTIN LUTHER AMBAYE ALITOKA KATOLIKI BAADA YA KUANZISHA MGOGORO. NA LAANA HIYO IMEENDELEA KULITESA KANISA LA LUTHERAN ambapo watu wamekuwa wakijiondokea kwenda kuanzisha makanisa mapya, makanisa mengi tunayoyaona mitaani yenye majina ya kilokole waanzilishi wake ni wale waliokimbia LUTHERAN. Na wengi wanaoondoka kwenda kuanzisha makanisa wengi NI WA BINAFSI NA NI KWA AJILI YAO NA SIO KWA AJILI YA KAZI YA INJILI.

Katoliki hakuna mwenye jina kubwa kuliko Kanisa, ila LUTHERAN mchungaji anaweza kuwa mkubwa kuliko Kanisa, mfano Eliaona Kimaro wa K/nyama na Matsai wa Kimara.
Katoliki hakuna maandamano au shinikizo la waumini , lakini LUTHERAN Mchungaji anaweza ku influence waumini waandamane kupinga Maelekezo na Maamuzi ya juu ya taasisi hiyo, NAKUMBUKA KANISA LA ELIAONA KIMARO.
Utaratibu wa kuendesha ibada ndani ya kanisa Katoliki umeendelea kudumishwa karne na karne TOFAUTI NA LUTHERAN AMBAPO KUNA MUDA UKIINGIA UNASHINDWA KUJUA HAPA NI LUTHERAN AU NI KWA MWAMPOSA MAANA NI KURUKARUKA KWA KELELE KAMA DISCO, WAENDESHA IBADA NI KUONGEA KWA MAGUVU NA MAKELELE YAANI KAMA WANAVYOFANYA WAHUBIRI WA KILOKOLE. UKUTE SASA WANAKEMEA MAPEPO.

KIMSINGI NDANI YA IBADA KATIKA MAKANISA YA KKKT HUWA HAKUNA UTULIVU , USTAARABU NA UNYENYEKEVU KAMA ILIVYOKUWA MIAKA YA 1980 ( japo ukienda ujerumani makanisa yao yaliendelea ku maintain litujia ya kanisa) ila hapa kwetu ni vurugu tu.

MWISHO SIKUWAHI KUJUA KAMA MKUU WA KKKT ANAWEZA KUMALIZA MUDA WAKE HALAFU BAADA YA MIAKA KADHAA AKAGOMBEA TENA KITI HICHO. NIMEIONA HII JUZI BAADA YA KUSIKIA ASKOFU MALASUSA AMECHAGULIWA TENA.
Kwa kweli hii inaondoa hadhi ya Kanisa yaani utafikiri chama cha siasa.

Japo mimi ni Mlutheri/KKKT lakini hakika KANISA KATOLIKI NI KANISA SAHIHI NA LITABAKI KUWA NI KANISA LENYE HESHIMA YA KITUME HASA NA HILI NDILO KANISA LA MUNGU
 
Uislam pekee.

Hakuna mfumo kama wa kanisa kwenye Uislam. Uislam ndiyo dini pekee kwa Mwenyezi Mungu. Kila kitu ni wewe na Muumba wako tu.
Kama uislamu ndio dini pekee basi there is no hope for the future.. mungu yule ya kwenye quran ndio awe aliumba mbingu na ardhi? Hilo jambo haliwezekani.
 
Hivi nyie mnaokaa kujadili Imani za Watu na miongozo Yao hamuoni Aibu? Wacheni Wafu wazike Wafu Wao. Hayawahusu ukiona huwezi kaanzishe Kanisa lako na Maji ya Upako, Mafuta ya Upako, Keki za Upako, na Mengineyo.
 
Wana matizo uao lukuki, tena makubwa na mazito sana, mengine ni majanga, wanaharibu watoto huko mpaka Umoja wa Mataifa umepiga kelele, msikilize aliyekuwa Rais wa Ufilipino anasema nini. Tazama link:

Bibi huko msikitini kwako hakuna maustadhi,Maulamaa,masheikh wanaolawiti watoto na watu wazima ikiwemo wake zao?
Usichanganye kosa na dini ya mtu.
Bibi mbona umri wako mkubwa unashindwa kupembua mambo madogo kama haya.??
 
Roman Catholic msingi wake umewekwa na Yesu Kristo kupitia Mtume Petro pale Vatican hayo mengine msingi wake uwekwa na mmiliki wake.
Ndo maana katoliki linaitwa church na hayo mengine yenye wachungaji walioa uitwa churches.
Hii nilikuwa sijui
 
KKKT litrujia yao imevurugika kwenye makanisa mengi! Ulokole umewavaa hadi unajiuliza wachungaji wao bado wanasoma falsafa na theology kama zamani?

Mahubiri ya kisasa ndio yametawala na injili ya toba imejifia zamani. Bila kuhubiri kwa makelele, kukemea mapepo, kutabiri n.k ni kama sio ibada.

Siku hizi yupo Yesu mpya anahubiriwa ambaye hana sifa, character wala msimamo ule tunaosimuliwa na wainjili Mathayo, Luka, Yohana na Marko.
Umemaliza kila kitu maana siku hizi watu eanafuata miujiza badala ya liturujia
 
Sasa kijana Kanisa makasii, na mapadri wawe zaidi ya 90% mashoga halafu useme siyo tatizo la kanisa?

Tuwe wa kweli kwenye nafsi zetu, tusidanganyane kutetea maovu, kwa kuwa tumeaminishwa ujinga tu.

Wazungu wameshastuka huko, wanayafunga makanisa na kuyafanya misikiti:

Sio bure wewe ulikua sista wa kanisa katoliki ukazaa ukafukuzwa..sasa chuki ndo zimetaradadi..
Habari yako Sr Fausta..
 
KKKT litrujia yao imevurugika kwenye makanisa mengi! Ulokole umewavaa hadi unajiuliza wachungaji wao bado wanasoma falsafa na theology kama zamani?

Mahubiri ya kisasa ndio yametawala na injili ya toba imejifia zamani. Bila kuhubiri kwa makelele, kukemea mapepo, kutabiri n.k ni kama sio ibada.

Siku hizi yupo Yesu mpya anahubiriwa ambaye hana sifa, character wala msimamo ule tunaosimuliwa na wainjili Mathayo, Luka, Yohana na Marko.
Daaah!!! Wewe jamaa umeongea ukweli halisi. Kinachoendelea ndani ya KKKT ya sasa ni tofauti na ile ya miaka ya 90 kurudi nyuma miaka ya 80s na 70s ambapo hata ukiingia kanisani ile atmosphere na utulivu wa kanisa unahisi hapa kweli kuna roho wa Mungu.
Mchungaji au Mwinjilisti anaposimama madhabahuni ule utulivu wake na unyenyekevu unaona kweli hapa kuna mtumishi muaminifu anayetuhubiria habari njema, hata kwenye nyimbo na kwaya zilikuwa zinaimbwa kwa kumaanisha na sio KWA MAVURUGU KAMA ILIVYO SASA.
Leo hii wachungaji wanachofanya ni kutaka kuwaonyesha waumini jinsi walivyo mahiri kuhubiri ndio maana mchungaji ni kurukaruka na kukimbia kila kona Madhabahuni, kufoka, kukemea, kunena na lugha wanayodai ndio lugha mpya.
YAANI KKKT WAMEJIKUTA WANACHEZA BEAT YA JAMAA ZAO WALIOUKIMBIA ULUTHERI NA KWENDA KUANZISHA MAKANISA YA KILOKOLE.
 
Back
Top Bottom