Ningekutana na Rais leo, Nimgemwuliza kwanini amemtoa Mchengerwa Utawala Bora

Ningekutana na Rais leo, Nimgemwuliza kwanini amemtoa Mchengerwa Utawala Bora

Ajiengue????utamlisha ww???
Kweli watumishi mmeumizwa sana Poleni.
naamini Mhe. Rais Mama yetu atalifanyia kazi suala hilo.

Lakini pia kama Jeni ujumbe umemfikia basi ni bora akajiengua mapema kuliko kuja kuenguliwa kwa fedheha, upepo unao vuma dhidi yake sio mzuri hivyo ajitafakari mapema kabla ya hatari.
 
Huu sio ujinga,ni ukweli mchungu.Kati ya hao mabosi mnaoita wenye roho mbaya na wenye roho nzuri wapi huwa wanatumbuliwa?

Yaani siku ukija kuajiriwa sekta binafsi ukawa boss afu ukawa vizuri kwa watumishi wa chini huchukui round.

Ni aidha uwe mnafiki kujifanya unajali watumishi wa chini huku unawafanyia mnayoita roho mbaya wasimamizi wao,ukirogwa tuu ukawa fresh kwa wote ujue uongozi umekushinda.
kama hapo ndipo mlipo fikia kuwa lazima uwe mpiga jungu na fitina ndipo udumu kazini au upande daraja basi watumishi mmeoza.
jambo hilo linapaswa liachwe mara moja.
 
Jaribio lake la vikokotoo namna lilivyozimwa kikatili, nilijua atatumbuliwa on the spot kama ilivyokuwa kwa wengine!

Nikaja kushangaa akaachwa!

Kweli huyu ni kipenzi cha watawala, tunamsagia sumu ya kunguni lakini haiwezi mdhuru vyovyote.
Lakini kwa manung'uniko haya kama hajatolewa au yeye mwenyewe kujiuzulu basi asubiri kufedheheka.
 
Simkubali kabisa Jenister na nafasi hiyo hatufai. Ila Mchengerwa anapaswa kujilaumu mwenyewe kwa kutolewa ORUBU. Mama alimuamini lakini akashindwa kuishi matarajio ya mamlaka yake ya uteuzi.

Inawezekana ni mtendaji mzuri. Lakini nyýuma ya pazia kuna makosa/ uhuni mwingi kafanya na kuvunja maadili ya utumishi wa umma ukitilia maanani majukumu na mahitaji ya Wizara aliyokua anaiongoza

Tena hapo kupelekwa Michezo na Utamaduni ni favour tu, alikua apumzishwe kabisa, akawe backbencher Mjengoni
 
Kwahiyo polisi wapo chini ya utumishi sio?!

Na hao polisi waliopanda vyeo mwezi mmoja baada ya kuwa wamemaliza kozi ni wa level ipi?! Hawa hawa wanaotokea CCP wakiwa kama Private, ndo unataka kusema mwezi mmoja baadae wakawa Makoplo?

vyeo vipya mwaka jana na mwaka huu.
level zote sio private.

kuhusu kuwa utumishi sina uhakika ila katibu mkuu ni boss wao pia.
 
Wizara ambayo ukiiangalia chini ya utendaji madhubuti wa mchengerwa , kero mbalimbali zilikuwa zinapatiwa ufumbuzi bila kuonea wala kukandamiza upande mmoja.

Alishaanza kutengeneza mifumo ambayo kwa vizazi vingi mbele vingenyoosha utendaji kazi wa watumishi na maafisa utumishi na mabosi wa maafisa utumishi.

Kifupi kila mtu angefanya kazi kama taratibu za kazi zinavyo taka.

Sio unaamka tu kwakuwa unamamlaka unasitisha likizo, unalimbikiza stahiki za mtumishi, unamcheleweshea haki zake n.k

Hayo yote Mchengerwa naona alikuwa anayanyoosha ipaswavyo.

Pengine siku moja atarejeshwa wizarani kama ilivyotokea kwa waziri wa afya Mwalimu.
kila la kheri
Eti Mchengerwa alitaka amchunguze Waziri mwenzake na mteule mwenzake
 
Inasemekana jamaa linazagamua kila sketi inayokatiza mbele, kachukua jiko la 3 mda si mrefu na bado mizagamuo ya kiholela ndo imekithiri.
Pia ni mla rushwa balaa, anajenga gorofa mbili kwa mkupuo sehemu fulani , yaani balaa huyu mkwe wa taifa
 
Inasemekana jamaa linazagamua kila sketi inayokatiza mbele, kachukua jiko la 3 mda si mrefu na bado mizagamuo ya kiholela ndo imekithiri.
Pia ni mla rushwa balaa, anajenga gorofa mbili kwa mkupuo sehemu fulani , yaani balaa huyu mkwe wa taifa
Ila kazi anachapa
 
Jenista amekaa wizara aliyotoka miaka zaidi ya 8 hakuna lolote alilofanya la maana! angalia mfuko wa jamii wa NSSSF wastaafu wanasumbuka mafao yao hadi wengine wanakufa kwa kukaa miaka mingi bila malipo!
Huyu mama nako huku Utumishi kutakuwa uozo tu kama kule alikotoka!~
 
Hujaona alichofanya Bungeni kusambaratisha Kambi jeuri kwa weledi na ustadi hadi wenyewe wanarukana

Sasa hivi anaenda kusambaratisha makatili waliowekwa kwny Utumishi
Nihakikishie kwanza kama wewe ni timamu, anyway, mwehu hawezi kujua kama yeye ni mwehu!
 
Back
Top Bottom