abulaaliyah77
JF-Expert Member
- Oct 13, 2021
- 1,750
- 1,158
Cha mtu huliwa na mtu, Chuma ndio huliwa na kutu...kwani akitoka anamkabidhi mkewe amshikie?
Hata mimi nimemlilia Mchengerwa na kulaani uwepo wa Jenista Mhagama
Kweli watumishi mmeumizwa sana Poleni.
naamini Mhe. Rais Mama yetu atalifanyia kazi suala hilo.
Lakini pia kama Jeni ujumbe umemfikia basi ni bora akajiengua mapema kuliko kuja kuenguliwa kwa fedheha, upepo unao vuma dhidi yake sio mzuri hivyo ajitafakari mapema kabla ya hatari.
kama hapo ndipo mlipo fikia kuwa lazima uwe mpiga jungu na fitina ndipo udumu kazini au upande daraja basi watumishi mmeoza.Huu sio ujinga,ni ukweli mchungu.Kati ya hao mabosi mnaoita wenye roho mbaya na wenye roho nzuri wapi huwa wanatumbuliwa?
Yaani siku ukija kuajiriwa sekta binafsi ukawa boss afu ukawa vizuri kwa watumishi wa chini huchukui round.
Ni aidha uwe mnafiki kujifanya unajali watumishi wa chini huku unawafanyia mnayoita roho mbaya wasimamizi wao,ukirogwa tuu ukawa fresh kwa wote ujue uongozi umekushinda.
Lakini kwa manung'uniko haya kama hajatolewa au yeye mwenyewe kujiuzulu basi asubiri kufedheheka.Jaribio lake la vikokotoo namna lilivyozimwa kikatili, nilijua atatumbuliwa on the spot kama ilivyokuwa kwa wengine!
Nikaja kushangaa akaachwa!
Kweli huyu ni kipenzi cha watawala, tunamsagia sumu ya kunguni lakini haiwezi mdhuru vyovyote.
Kwahiyo polisi wapo chini ya utumishi sio?!
Na hao polisi waliopanda vyeo mwezi mmoja baada ya kuwa wamemaliza kozi ni wa level ipi?! Hawa hawa wanaotokea CCP wakiwa kama Private, ndo unataka kusema mwezi mmoja baadae wakawa Makoplo?
Hivi uyu mzee yupo ? Sijamuona akiapa mbele ya Rais Leo.Nadhani atakuwa sawa na yule mzee kawekwa ikulu wizara maalumu
Naunga mkono hojaNaunga mkono hoja pale utumishi hapahitaji wapiga siasa kama huyu mama
Hamna kitu huyo mamaKwani aliopo saizi anashida gani? Au nyie ndiye wenye shida na matatizo? Ameletwa mwingine kukamilisha,kuendeleza na kuboresha pale alipoishia mwenzake.
Eti Mchengerwa alitaka amchunguze Waziri mwenzake na mteule mwenzakeWizara ambayo ukiiangalia chini ya utendaji madhubuti wa mchengerwa , kero mbalimbali zilikuwa zinapatiwa ufumbuzi bila kuonea wala kukandamiza upande mmoja.
Alishaanza kutengeneza mifumo ambayo kwa vizazi vingi mbele vingenyoosha utendaji kazi wa watumishi na maafisa utumishi na mabosi wa maafisa utumishi.
Kifupi kila mtu angefanya kazi kama taratibu za kazi zinavyo taka.
Sio unaamka tu kwakuwa unamamlaka unasitisha likizo, unalimbikiza stahiki za mtumishi, unamcheleweshea haki zake n.k
Hayo yote Mchengerwa naona alikuwa anayanyoosha ipaswavyo.
Pengine siku moja atarejeshwa wizarani kama ilivyotokea kwa waziri wa afya Mwalimu.
kila la kheri
Ila kazi anachapaInasemekana jamaa linazagamua kila sketi inayokatiza mbele, kachukua jiko la 3 mda si mrefu na bado mizagamuo ya kiholela ndo imekithiri.
Pia ni mla rushwa balaa, anajenga gorofa mbili kwa mkupuo sehemu fulani , yaani balaa huyu mkwe wa taifa
Naam anachapa kazi kwerikweri.Ila kazi anachapa
Yaani huyu mama ni porojo tu, wizara hii ni nyeti sana. Tujifunze huko alikotoka kaacha nini cha kukumbukwa tofauti na mchengerwa.Naunga mkono hoja pale utumishi hapahitaji wapiga siasa kama huyu mama
Nihakikishie kwanza kama wewe ni timamu, anyway, mwehu hawezi kujua kama yeye ni mwehu!Hujaona alichofanya Bungeni kusambaratisha Kambi jeuri kwa weledi na ustadi hadi wenyewe wanarukana
Sasa hivi anaenda kusambaratisha makatili waliowekwa kwny Utumishi
Nihakikishie kwanza kama wewe ni timamu, anyway, mwehu hawezi kujua kama yeye ni mwehu!