Ningekutana na Rais leo, Nimgemwuliza kwanini amemtoa Mchengerwa Utawala Bora

Mimi ningemuuliza kwanini ameacha kwenye baraza lake la mawaziri wake ambao wanautaka Urais kuliko jambo lolote lile.
 
Kama kweli anaenda kutuzulumu watumishi tutaanda mandamano kwa ajili yake atoke haraka.
 
Wewe unataka kukwanyuliwa. Ile ni wizara ya TISS.
Kumbuka Lissu alisema wanajeshi hawampendi Mabeyo.
 
Hata mimi mama kaniudhi Sana hapa,unamtoa mtu anaetetea watumishi?

Hivi kumbe watumishi ni watu wa kukandamizwa? Kile kijenista ndicho kilileta upuuzi wa kikokotoo afu wanakirudisha tena?
 
Mchengerwa alikuwa anatupa sana faraja na matumaini sisi watumishi,sijui ni kipi kimesababisha atolewe wakati aliimudu vzr wizara ile nyeti.
 
Sijui Nini Kimetokea Kuhusu Huyu Jamaa. At Least He Was A Perfect Fit Among Others.
 
Mama kachemka kwa huyu dogo kuondoka wizara ile kiukweli dogo alideliver sana
 
Kweli jina la wizara ya Gwajima watoe Hilo neno la wanawake maana ukisema Jinsia tayari ni wanaume na wanawake, Ili I sound vizuri na sio kiubaguzi ubaguzi hivi
 
Kwakweli kwa Mchengerwa alijua kweli kuwapambania Watumishi,alijitahidi sana sijui kwanini ametolewa
 
Ndani ya muda mfupi tumeshuhudia mabadiliko makubwa sana kwenye kutatua kero za watumishi has a madaraja. Kwa Mara ya kwanza katika historia mwaka 2021 watumishi wanapanda na kubadilishiwa mshahara mwezi huo huo. Miaka ya nyuma ilikuwa unaweza kupandishwa 2010 mshahara ukabadilika 2012 na ndio maana yanazaliwa malimbikizo.
Mikwala ya Mchengerwa maafisa utumishi hasa wa halmashauri walishaanza kunyooka sasa hivi umetuondolea mtetezi wetu. Hatutaki turudi kwenye miaka ya dhiki unapanda basi kwenda Dsm kufuatilia daraja. Ukitoka hapo uende Hazina ubadilishiwe unasubiri miezi 20.
 
Ninadhani upandishwaji wa madaraja kwa wakati ilikua msukumo zaidi kutoka kwa mkuu wa nchi.
Mchengerwa alikua mtekelezaji tu wa maelekezo kutoka kwa mh. Rais.

Hata awamu iliyopita sio kwamba Mkuchika hakua na uwezo wa kupandisha madaraja kwa wakati bali alitii maelekezo ya mamlaka iliyokua imemuweka
 
Mh. Rais kwakumuondoa Mchengerwa umetukosea sana watumishi wa Nchi hii... Ndani ya Muda mfupi aliohudumu katka UTUMISHI mambo mengi yalibadirika na watumishi walifurahi.. Sasa huyu Mwanamama uliemleta hatufai ata bure sijui ninani aliekushauri utuletee Huyu.. Huyu Muhagama ni Bendera fuata upepo tu kwanza uyu nahisi nae ni Sukuma Gang tunakuomba utuondolee uyu Muhagama uwezo wake ni mdogo sana hana ushawishi wa kuwaagiza maafisa Utumishi miungu watu kwenye maofisi... Mh Rais tunakuomba sana Muhagama ni Big No
 
Ni sahihi kabisa,lakini nadhani mwenye mamlaka na uhalali wa kuamua nini kifanyike kwenye sehemu yake waziri maana kweli ukiangalia malimbikizo yamekuwa ni ugonjwa wa watumishi toka awamu za nyuma isipokuwa kwa awamu hii ya 6 watumishi wamepanda madaraja wengine hata barua hawajazipata lakini mshahara husika umeshaingia tayari.
My take mama kama anasikia iatakuwa ni busara kumrudisha maana hata hivyo siyo mishahara na madaraja tu hapana hata issues zingne za kiutawala jamaa kazifanyia kazi sana na kuleta ahueni kwa walio wengi japo siyo wote.
 
Hakika mkuu, huko nyuma mambo yalikuwa vurugu tupu hasa kwa watumishi wa serikali za mitaa. Mmeajiriwa mwaka mmoja ila mwenzako wa wilaya X anakupita wewe wa Y kwa miaka hata miwili. Nakumbuka mwaka 2018 nilikaa miezi 11 bila kubadilishiwa mshahara nikafunga safari kwenda Dodoma ndio wakabadilisha
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…