Nini cha kufanya endapo utakuta dhahabu kwenye shamba au kiwanja chako?

Nini cha kufanya endapo utakuta dhahabu kwenye shamba au kiwanja chako?

Wakikuta bangi shambani mwako ni yako, ila dhahanu ni yao.
Huo ni uonevu kabisa. Sidhani kama nchi za wenzetu wanafanya hivyo. Japo sina uhakika, lakini sidhani kama Kenya na wao utaratibu wao ni kama wa kwetu. Sidhani!
 
Uliza ilichomkuta yule Jamaa wa Shinyanga.
Muhimu ni kutuliza munkari.
Chukua sehemu kauze kaboreshe mahali pako kwa kuweka hata kiwanda cha unga wa sembe then usiku unangurumisha machine watu wanajua unaasaga sembe kumbe unaasaga mawe.
Ukijiroga tu utauwawa . Usicheze na pesa
View attachment 2823887
Natamani nikakute hako kamlima shambani kwangu.
 
kuitoa dhahabu ardhini kama ni masikini unawezs hata kufungwa jela kwa kusingiziwa ili upishe wenye pesa.
Ili upate dhahabu inabidi uwe na pesa nyingi sana.
Hebu tupe hekima yako na wewe mkuu.

Chukulia wewe ni mtu wa kawaida tu, halafu ukakutana na dhahabu kubwa kama kichwa cha ng'ombe shambani kwako, utachukua hatua gani?
 
Hebu tupe hekima yako na wewe mkuu.

Chukulia wewe ni mtu wa kawaida tu, halafu ukakutana na dhahabu kubwa kama kichwa cha ng'ombe shambani kwako, utachukua hatua gani?
Miye ntaikata kidogo alafu naenda mtoni huko nakoga masingizia nimeokota humo. Nawaacha wavurugane humo miye nachomba kidogo kidogo.
 
Hebu tupe hekima yako na wewe mkuu.

Chukulia wewe ni mtu wa kawaida tu, halafu ukakutana na dhahabu kubwa kama kichwa cha ng'ombe shambani kwako, utachukua hatua gani?
Naichukua naiweka ndani. Simwambii mtu yoyote. Hapo cha kufanya nakuwa namega kipande kidogo naenda kuuza.
Naenda mgodini, najifanya nanunua mawe ya dhahabu km sonko kisha nauza mpk mzigo unaisha. H
Hapo simwambii mtu yoyote ile yaani kimya kimya
 
Ushauri wangu kama ni eneo ambalo halina history ya dhahabu (probability ya uwepo wa leseni ni mdogo) nenda tume ya madini usiseme umeiona au kugundua dhahabu we kata kipande kikubwa Hadi kwa watu ambao bado hawajastuka lipia leseni (watakupa utaratibu) baada ya hapo we tangaza Kuna mzigo. Wadau watakuja ruhusu wachimbe we kula asilimia tu......
Huu ujinga sifanyi Laizer angefanya hivi ubilionea angeusikia kwenye bomba
 
Huo ni uonevu kabisa. Sidhani kama nchi za wenzetu wanafanya hivyo. Japo sina uhakika, lakini sidhani kama Kenya na wao utaratibu wao ni kama wa kwetu. Sidhani!
Hapa ukidakwa hio ni kesi tena na eneo unapokonywa linakua Mali ya Serekali wanamtafuta muwekezaji achimbe sio wewe,
 
Kwa Sheria za Tanzania, unaweza kumiliki ardhi lakini sio kilichopo chini ya ardhi kama madini. Ndivyo nijuavyo, labda kama utaratibu umeshabadilika. Inamaanisha kuwa hata ukigundua dhahabu kwenye shamba lako au kiwanja chako, hutaruhusiwa kuchimba mpaka uwe na leseni.

Sasa chukulia ulikuwa unachimba shimo la choo, na ghafla ukakutana na bonge la dhahabu (nugget) kubwa kama kichwa cha ng'ombe, nini utakachopaswa kufanya Kisheria?

1. Kwenda kuripoti Polisi?

2. Kwenda kutoa taarifa wizarani?

3. Kuujulisha uongozi wa Serikali ya Mtaa?

4. Kwenda kuiuza na kisha kuwasilisha TRA stahiki za Serikali?

Ni hatua gani sahihi utakayopsawa kuchukua?

Nani atakuwa mmiliki halali wa hiyo dhahabu?

Ukijimilikisha bila kutoa taarifa Serikalini utakuwa umetenda kosa, hasa ikizingatiwa kuwa umeichimbua bila kutarajia?
Dhahabu ikikutwa shambani mwako siyo yako bali ni mali ya Serikali, lakini bangi ikikutwa shambani mwako ni yako.
 
Kwa Sheria za Tanzania, unaweza kumiliki ardhi lakini sio kilichopo chini ya ardhi kama madini. Ndivyo nijuavyo, labda kama utaratibu umeshabadilika. Inamaanisha kuwa hata ukigundua dhahabu kwenye shamba lako au kiwanja chako, hutaruhusiwa kuchimba mpaka uwe na leseni.

Sasa chukulia ulikuwa unachimba shimo la choo, na ghafla ukakutana na bonge la dhahabu (nugget) kubwa kama kichwa cha ng'ombe, nini utakachopaswa kufanya Kisheria?

1. Kwenda kuripoti Polisi?

2. Kwenda kutoa taarifa wizarani?

3. Kuujulisha uongozi wa Serikali ya Mtaa?

4. Kwenda kuiuza na kisha kuwasilisha TRA stahiki za Serikali?

Ni hatua gani sahihi utakayopsawa kuchukua?

Nani atakuwa mmiliki halali wa hiyo dhahabu?

Ukijimilikisha bila kutoa taarifa Serikalini utakuwa umetenda kosa, hasa ikizingatiwa kuwa umeichimbua bila kutarajia?
Formula hapa ni ile ile tu.

Shamba likikutwa na Dhahabu linageuka kua la Serikali, ila likikutwa na Bangi hilo ni la kwako tum
 
Back
Top Bottom