Haya ndio mapungufu tuliyotengenezewa na waasisi wa taifa hili kwa kufurahia uhuru wa bendera hadi kusahau kufanya mgawanyo wa ardhi kwa kuzingatia umiliki wa awali wa kimila.
Serikali ni project ya wakoloni waliopora ardhi ya waafrika na kuihalalisha kwa mkutano wa kugawana mali ya wizi huko Berlin.
Utata unaojitokeza kuhusu umiliki wa ardhi na mali iliyoko ardhini kati ya Serikali na mwananchi ni ushahidi wa mapungufu ya kutofanya " Land reform" mara tu tulipopata uhuru. Serekali ilirithi mali ya wizi na haikutaka kuirejesha kwa wamiliki halali ambao ni mwananchi, badala yake imejimilikisha na kuwa mali ya Serikali chini ya usimamizi wa Rais.
Bara la ulaya baada ya kwisha vita vya pili vya Dunia,walianza kwa kuirejesha ardhi mikononi mwa wananchi, watu walipimiwa kati ekari 5 hadi 10, ardhi iliyobaki ni akiba, lakini mfumo wa mali ya umma ambayo ni misitu.
Kukosekana kwa sera ya ardhi na uwazi katika kushughulikia ardhi ndio chanzo cha migogoro inayojitokeza kwenye ardhi zetu. Haishangazi kusikia bangi iliyokutwa sahambani kwako ni mali yako wakati dhahabi au maji ya kisima ardhini ni mali ya Serikali......Huu ni ujinga karne!.