Nini cha kufanya endapo utakuta dhahabu kwenye shamba au kiwanja chako?

Nini cha kufanya endapo utakuta dhahabu kwenye shamba au kiwanja chako?

Kwa Sheria za Tanzania, unaweza kumiliki ardhi lakini sio kilichopo chini ya ardhi kama madini. Ndivyo nijuavyo, labda kama utaratibu umeshabadilika. Inamaanisha kuwa hata ukigundua dhahabu kwenye shamba lako au kiwanja chako, hutaruhusiwa kuchimba mpaka uwe na leseni.

Sasa chukulia ulikuwa unachimba shimo la choo, na ghafla ukakutana na bonge la dhahabu (nugget) kubwa kama kichwa cha ng'ombe, nini utakachopaswa kufanya Kisheria?

1. Kwenda kuripoti Polisi?

2. Kwenda kutoa taarifa wizarani?

3. Kuujulisha uongozi wa Serikali ya Mtaa?

4. Kwenda kuiuza na kisha kuwasilisha TRA stahiki za Serikali?

Ni hatua gani sahihi utakayopsawa kuchukua?

Nani atakuwa mmiliki halali wa hiyo dhahabu?

Ukijimilikisha bila kutoa taarifa Serikalini utakuwa umetenda kosa, hasa ikizingatiwa kuwa umeichimbua bila kutarajia?
Chota kimyakimya tena peke yako, usithubutu kumjulisha mkeo na asishike jembe mwambie ataharibika mikono kwa kuota sugu.
Kunajamaa aliajiri mtu amchimbie shimo la choo, jamaa aliikuta chepe huku mchimbaji hajulikani alipo
 
Nahisi hapo ni Geita. Ndiyo mkoa wenye hiyo "tabia".
 
Mfano, ukigundua kuwa shamba lako ni "mlima" wa dhahabu, utafanya nini?
 
Attachments

  • #MLIMA_WA_DHAHABU__CONGO_DRC...__Polisi_400_wazunguka_mlimaa__nakuwapora_wanakijiji_zahabu_wal...mp4
    3.7 MB
Kwa Tanzania, si ajabu kukutana na dhahabu wakati wa kuchimba shimo la choo au kisima cha maji. Ilishatokea zaidi ya mara moja.
 
Attachments

  • MGODI_WA_DHAHABU_WAIBUKA_KATIKATI_YA_MAKAZI_YA_WATU_NI_BAADA_YA_MWANA_KIJIJI_KUCHIMBA_CHOO(360p).mp4
    12.1 MB
Sijui kama walinufaika nayo au ndiyo hivyo tena!
 
Attachments

  • Ghana_Teens_Find_Enormous_Gold_Nugget_Possibly_Biggest_in_Countries_History(360p).mp4
    7.8 MB
Mfano, ukigundua kuwa shamba lako ni "mlima" wa dhahabu, utafanya nini?
Utadakwa na Serekali ukatoe maelezo alafu unapokonywa unakua wa kwao wanamuita muwekezaji wewe unatimuliwa bila kupewa chochote upishe uchimbaji uendelee
 
Sijui kama walinufaika nayo au ndiyo hivyo tena!
Ndio hivyo Tena this is Africa my blood huku sio ulaya huku ni bara la Giza ukikutwa nacho ni Cha kwao sio Cha kwako usicheze na nyara za Serekali na tunu za Taifa ukidakwa na nyama ya swala hata robo tu utanyea debe miaka 30 bila rufaa
 
Kama kweli umepata Gold Nuggets sema ili nikushauri kitu chenye Uhalisia coz mimi ni mdau wa Madini....!

Ila kama ni story tu ambazo hazina uhalisia, basi wacha niendelee kusoma Comments.
 
Fikiri umeukuta mzigo kama huu shambani kwako!
Ukikuta shambani shamba linageuzwa kua sio Mali yako tena linachukuliwa na wenyewe wenye nalo wewe ulikodishiwa tu hio Ardhi sio Mali yako ni Mali yao kwa hio upishe wenyewe wenye Mali yao waichimbe wewe utatimuliwa tu
 
Kama kweli umepata Gold Nuggets sema ili nikushauri kitu chenye Uhalisia coz mimi ni mdau wa Madini....!

Ila kama ni story tu ambazo hazina uhalisia, basi wacha niendelee kusoma Comments.
Huna Cha kumshauri mwambie tu aifikishe kwa Mkemia akaisalimishe kabla hajavutiwa pira na msako wa nguvu
 
Hivi melting point ya dhahabu ni ngapi ili uweze kuikata na kuuza kidogo kidogo kwa usalama wako..,...au unaweza kuikata na msumeno tu kama nondo ya kawaida....???
Uiuze wapi? Kabla haujadakwa na kuitwa mtorosha Madini? Hivi mnachukulia poa poa au sio? Jaribu kufanya huo ujinga uone unavyodakwa kirahisi, wewe isalimishe kwa wenyewe wenye ardhi yao waichukue sio Madini mapya dhahabu kwamba umegundua km ilivyotokea kwa yule Mzee wa Tanzanite, ukidakwa unaisalimisha inataifishwa umekula kwako the End
 
Inawezekana kuonekana ni mjadala wa kivivu lakini ni wenye manufaa sana.........

Hivi melting point ya dhahabu ni ngapi ili uweze kuikata na kuuza kidogo kidogo kwa usalama wako..,...au unaweza kuikata na msumeno tu kama nondo ya kawaida....???
Nahisi ni 1000 C ila kahama,Mbeya na baadhi ya sehemu Geita huko na shibyanga kuna sehemu kibao za Kuyeyesha huwa wanazitumia Mabroker...
Ye akitaka kuwa mjanja awasiliane na Broker yoyote awe anamuuzia Wanakula naye deal
 
Kwanza chukua kakipande kadogo ka kuuza kakufanye uwe na ukwasi wa kufanya biashara hiyo hiyo ya madini. Usiwe na haraka, ielewe vizuri biashara na siri zake, ukishaijua utajua namna sahihi ya kufanya usipoteze.

Hata ukipewa bure shamba lenye nyanya tayari kwa kuvunwa kama hujui jinsi soko linavyofanya kazi unazipoteza.
 
Back
Top Bottom