Nini cha kufanya endapo utakuta dhahabu kwenye shamba au kiwanja chako?

Nini cha kufanya endapo utakuta dhahabu kwenye shamba au kiwanja chako?

Uliza ilichomkuta yule Jamaa wa Shinyanga.
Muhimu ni kutuliza munkari.
Chukua sehemu kauze kaboreshe mahali pako kwa kuweka hata kiwanda cha unga wa sembe then usiku unangurumisha machine watu wanajua unaasaga sembe kumbe unaasaga mawe.
Ukijiroga tu utauwawa . Usicheze na pesa
View attachment 2823887
Afunge mashine ya kusaga unga ,azungushie Uzio mrefu sana hilo eneo lake na ulinzi wa kutosha halafu aajiri vibarua miners toka Burundi au Uganda huko
Wabongo ni waropokaji sana
 
Sheria ya kikoloni na iliyopitwa na wakati
Ni wakati wa kupeleka mapendekezo Serikalini ili hii sheria ifanyiwe Marekebisho,haiwezekani unakuta kwenye Shamba lako kitu chochote kile halafu ww mmiliki wa Shamba hupati hata Sumni hio haipo sawa.Serikali kupitia Wizara ya Madini kutunga Sheria ili watu wenye Mashamba nao wafaidike kupitia Mashamba yao kwa kuwa nao wanakuwa wameshawekeza humo ndani ya hayo Mashamba vitu vingi tu.Serikali ilifikirie hili suala hata akija muwekezaji basi huyu mwenye shamba anajua ana asilimia zake.
 
Chota kimyakimya tena peke yako, usithubutu kumjulisha mkeo na asishike jembe mwambie ataharibika mikono kwa kuota sugu.
Kunajamaa aliajiri mtu amchimbie shimo la choo, jamaa aliikuta chepe huku mchimbaji hajulikani alipo
Maeneo ya Geita au kahama Shinyanga ukimiliki shamba au kiwanja ni kawaida kukutana na hicho kitu , kila siku inaibuka migodi huko kwenye makazi ya watu
Watu wanachimba vyoo au makaburi wanaibuka na mawe makubwa ya dhahabu .
 
Afunge mashine ya kusaga unga ,azungushie Uzio mrefu sana hilo eneo lake na ulinzi wa kutosha halafu aajiri vibarua miners toka Burundi au Uganda huko
Wabongo ni waropokaji sana
Fuga mbwa tishio kama Rottweiler hakuna fala kuingia wala kutoka...
Hao dogs wawe wamezungushiwa uzio kuwa huru kuzunguka uzio pande zote ndani kwa ndani, kiasi kwamba hata wachimbaji hawawezi kuwaza kuruka ukuta
 
Sikia.

1. Kama mzigo ni mkubwa, Usithubutu kumwambia yoyote, hata nzi asijue una mzigo ndani au peleka mbali huko kafiche.

Kama mzigo mdogo sijui kg 2 au 3 au chini ya hapo tafuta tu dealers wapo kibao maeneo yenye dhahabu hata akikupiga kidogo hata Milioni 20, 30 sio mbaya mradi uwe salama, Uza mzigo ila usimpe ramani mzigo ulipotoka, bora umdanganye. Usimuamini mtu kwenye masuala ya dhahabu ni hatari Sana. ( Umafia mwingi huko)

Sababu watu wakijua aisee hata ujenge ukuta wa chuma people zitavamia kama mchwa yaani wakiingia jioni Asubuhi utakuta eneo lote ni mashimo tu na fonka za kutosha.

Mfano kuna eneo dhahabu ilifumuka karibu na shule, baada ya muda watoto wanasoma madarasani kumbe wapambanaji wapo chini ya madarasa wanasaka mzigo. Hatari Sana.

2. Kata leseni ya mchimbaji mdogo, ni rahisi tu kama Sheria hazijabadilika ni Tshs 90,000 tu Kwa hekari.

Hapa sasa usikatie leseni eneo ulilopata mzigo, nunua hata heka 3 katia leseni mbali na hilo eneo.
( Hapa sasa kauze mzigo wako Kwenye soko la dhahabu kama mzigo ni mkubwa )

Soma upepo hata mwezi kama eneo lako hilo jipya lipo salama,

Kama likivamiwa sikilizia hadi papoe, halafu sasa kakatie leseni eneo halisi lenye mzigo.

3. Hapa Sasa tafuta mchimbaji mzoefu mkubwa mzawa au mwenyeji wa maeneo hayo ingia nae mkataba kwa mwanasheria, kula asilimia.
Kwa sababu hao wachimbaji wakubwa huwa wanaogopwa hakuna kima atavamia eneo lako pia wana uzoefu, mtaji na ulinzi pia wataweka.

Japo lazima atakupiga kiaina ila utakula matunda kiroho safi bila presha.
 
Miye ntaikata kidogo alafu naenda mtoni huko nakoga masingizia nimeokota humo. Nawaacha wavurugane humo miye nachomba kidogo kidogo.
Watakuwekea mtego wa kukufuatilia tu lazima wajue uliko itoa

Kuna Jamaa walikuwa wanachimba choo bahati nzuri wakakutana na mawe ya dhahabu, Jamaa wakawa wanachimba Kwa Siri na wakawa wanapeleka mawe yao kusaga mwilo ya mbali ila Jamaa waliwafanyia upelelezi mpaka wakajua sehemu wanakochimba.
 
Naanzisha karakana ya kufyatua tofali. Mchana tofali usiku dhahabu.
Wabongo ut
Naanzisha karakana ya kufyatua tofali. Mchana tofali usiku dhahabu.
Wabongo utakao waajiri ndio watakao kuchoma ,yaani hiyo inabidi hiyo mbanga ufanye na watu wa mataifa ya nje , kama unataka kuchimba siri iwe yako tu .
Usimhusishe Kenge yoyote wa Tz humu ,na ukivuna vukisha kimagendo kauze kwenye black market za Zimbabwe huko na south Afrika au peleka Nairobi
 
Sitaki nikuvunje moyo lakini ukisoma kifungu namba 6 chote hasa kifungu kidogo cha nne cha sheria ya madini namba 123 ya 2019, huo mzigo sio wako na serikali itautaifisha kwa sababu hauna kibali cha uchimbaji madini.

Cha kukushauri kata kibali cha uchimbaji kwanza ili uweze kuuza mzigo hapo baadae.
Screenshot_20231126_102341.jpg

Nimeambatanisha sheria ya Madini. Ipitie hiyo. Pia jaribu kutafuta marekebisho ya hiyo sheria kama yalishafanyika.
 

Attachments

Kwa hiyo kumbe ni bora ujinyamazie zako na kuiuza kimya kimya.

Lakini Serikali imetoa wapi huo utaratibu? Mbona inawashawishi raia kusema uongo?
Wakati wa Magufuli nilimsikia akisema:..."hizi sheria za ajabu ajabu ndiyo zinasababisha utoroshwaji wa madini nje"...

Nadhani walirekebisha, ukiipata na kuipeleka kwenye soko la madini huulizwi ulipoitoa.

Huyo mchimba choo hakuwa msiri akaropoka, ambapo alipoenda kuipima na kugundua ni dhahabu, ilitakiwa achimbe choo kisichoisha na akipata pesa ya kutosha anawafukuza majirani zake kwa pesa na kupiga fensi na kuanzisha "ujenzi" usioisha.

Na huyo mzungu aliyeficha uso huku akiokota "majabali" ya dhahabu ni wapi huko walikolala usingizi usioamshika?

Mbuga nzima imejaa dhahabu mabonge mabonge, au ni kiini macho cha kimtandao?

Maana jambo hilo haliwezekani kwenye dunia ya leo.
 
SIMPLE KAKATE LESENI YA UNUNUZI WA ZAHABU THEN ZUNGUSHA FENSI.UWANJA WAKO THEN.MEGA KIDOGOKIDOGO UNAPELEKA SOKONI.SIMPLE AND CLEAR KUMBUKA HII KAZI.UNATAKIWA UIFANYE PEKEE YAKO IKIWEZEKANA HAMISHA KABISA FAMILIA YAKO PELEKA SEHEMU.NYINGINE HII INAKUWA SILI YAKO WEWE TU NA MCHIMBAJI WEWE TU.
 
SIMPLE KAKATE LESENI YA UNUNUZI WA ZAHABU THEN ZUNGUSHA FENSI.UWANJA WAKO THEN.MEGA KIDOGOKIDOGO UNAPELEKA SOKONI.SIMPLE AND CLEAR KUMBUKA HII KAZI.UNATAKIWA UIFANYE PEKEE YAKO IKIWEZEKANA HAMISHA KABISA FAMILIA YAKO PELEKA SEHEMU.NYINGINE HII INAKUWA SILI YAKO WEWE TU NA MCHIMBAJI WEWE TU.
✅🙏
 
Back
Top Bottom