Nini cha kufanya endapo utakuta dhahabu kwenye shamba au kiwanja chako?

Nini cha kufanya endapo utakuta dhahabu kwenye shamba au kiwanja chako?

Chota kimyakimya tena peke yako, usithubutu kumjulisha mkeo na asishike jembe mwambie ataharibika mikono kwa kuota sugu.
Kunajamaa aliajiri mtu amchimbie shimo la choo, jamaa aliikuta chepe huku mchimbaji hajulikani alipo
Mwenye kisima aliweza kuambulia chochote?
 
Kwanza chukua kakipande kadogo ka kuuza kakufanye uwe na ukwasi wa kufanya biashara hiyo hiyo ya madini. Usiwe na haraka, ielewe vizuri biashara na siri zake, ukishaijua utajua namna sahihi ya kufanya usipoteze.

Hata ukipewa bure shamba lenye nyanya tayari kwa kuvunwa kama hujui jinsi soko linavyofanya kazi unazipoteza.
โœ…๐Ÿ™
 
Uko sahihi. GoldDhahabu amechokonoa mada nzuri sana. Yeye ameeleza wazi kuwa lengo ni kujua utaratibu wa kisheria iwapo hali kama hiyo itatokea. Wengi tunajua kuwa iwapo tukio la la bahati la aina hiyo likitokea, asilimia kubwa watafanya siri na kuuza bila kujulisha umma. Ila nia ya uzi ni kujua kisheria inatakiwa ufanye na consequenses zake...
โœ…๐Ÿ™๐Ÿ™๐Ÿ™
 
Hio - Hiyo
Kua - Kuwa
Sasa kama unashindwa kuandika maneno ya lugha ya kiswahili kwa usahihi wala huwezi kutumia alama za uandishi
Sasa utakuwaje na akili ya kuuza hiyo dhahabu?
Kama unayo, nipe nikuuzie
Lugha fasaha na biashara ya madini ni vitu viwili tofauti mkuu!

~ Arusha kuna Wamasai wanafanya biashara kubwa ya Tanzanite japo hawajui Kiswahili fasaha.

~ Tanzania kuna Wachina wanaofanya mpaka umachinga japo hawakijui Kiswahili fasaha wala Kiingereza fasaha.

Ukishakuwa na mzigo, utauuza ti, hata kama hujui lugha. Hata lugha ya ishara inaweza kutumika.
 
Lugha fasaha na biashara ya madini no vitu viwili tofauti mkuu!

~ Arusha kuna Wamasai wanafanya biashara kubwa ya Tanzanite japo hawajui Kiswahili fasaha.

~ Tanzania kuna Wachina wanaofanya mpaka umachinga japo hawakijui Kiswahili fasaha wala Kiingereza fasaha.

Ukishakuwa na mzigo, utauuza ti, hata kama hujui lugha. Hata lugha ya ishara inaweza kutumika.
Lugha fasaha na biashara ya madini 'no'! vitu viwili tofauti mkuu!
 
Back
Top Bottom