Nini chanzo cha ugomvi wa January Makamba na Musukuma?

Ikumbukwe tu, Musukuma ni PhD holder, msiulizeulize
 
Halafu kuna mtu anasema eti Msukuma ni mfitini; si wajibu hayo maswali? Hapa mbona wala halingwi mtu, kuna issue hapa, ijibiwe issue wala sio mtu. January ajibu maswali ya Msukuma, baaasi
 
Nailed; ukweli watu wanamtetea tu jamaa but ukweli kachemka mbaya kwenye UMEME, mbayazaidi Magufuli aliisha twambia kwamba kwenye umeme, wahuni walikua wakifanya yao, tunao sasa na bado watu wana ujasiri kabisa wa kutetea jambo hili. Kalemani alivyotolewa tu, hata mwezi haukuisha, mgao wa umeme ukaanza, till todate bado umeme sio stable. Sasa hata hili watu wanataka kumtetea mtu kwa maslahi ya nani!?
 
Mtu akisoma ulichoandika, anajua upande wako.
 
January Makamba ni another seti tupu ilioko kwenye system.. huyu na huyo mwingine aliesema aliekatwa makato kwenye simu ampelekee . yaani ma zero fulani hivi yapo kwenye uongozi kwa hisani ya msoga, ila kuna siku kitawaka: wafurahie uongozi kwa sasa. Makamba majibu aliojibu bungeni ni ya kisanii sana ila kwa wapumbavu ndio wanaweza sema kajibu kitu. Cheap politics kwenye mambo ya maana shenzi sana hawa akina kigogo2014 dawa yao iko jikoni.
 
Mkitumaliza sisi, mtaanza kumalizana wenyewe kwa wenyewe, nukuu ya Godbles Lema
 
Shida ya watu katika Tanzania yetu ni akili Huyo msukuma hata kama anaongea pumba katika kuhoji suala la umeme kukatikakatika hovyo anaweza akawa na akili zaidi kuliko Elimu,hivi waziri asiye na akili ila ana Elimu anaweza kusaidia nn kwenye wizara nyeti kama hii.waziri anatakiwa awe na akili kwanza alafu awe na Elimu,akiwa hivyo ataweza kusaidia sana kuitoa wizara hapa ilipo na kuipeleka kwenye hatua kubwa zaidi.Tunapaswa kujua kwamba Hii wizara imepata waziri mpuuzi ambae haelewi nn anatakiwa kufanya na hii yote inatokana na kuwa na Elimu alafu akili HAKUNA sasa hapo huwa lazima haya tunayoyashuhudia yatokee.NCHI INAHITAJI WAZIRI MWENYE VITU VYOTE VIWILI YAANI AKILI NA ELIMU,SASA MAKAMBA HANA KIMOJA YAANI AKILI NDIO MAANA NCHI INAJIKUTA KWENYE MKWAMO WA MGAO MKUBWA WA UMEME.
 
Kwa kifupi kabisa huyu mtu anaitwa Musukuma ni mtu wa hovyo sana na mpenda fitina za kijinga. Ameumiza watu wengi kwa fitina zake za hovyo. Naamini watawala wameelewa uhuni wake. Niishie hapo, inatosha.
Muombe radhi Dr.Musukuma kwa hichi ulichokiandika.
 

Labda hujaelewa majibu ya Makamba...

Hoja yako na ya Msukuma ni kuhusu kukatikakatika kwa umeme...

Majibu ya Makamba ni kuwa, kama mashambulizi hayo yote ni kwa sababu ya kukatikatika kwa umeme, HILO SIYO TATIZO LAKE...

Binafsi nayaita "mashambulizi" kwa sababu, ukimsikiliza mbunge Msukuma vyema, utatambua mara moja kuwa haulizi kwa nia ya kutaka suluhu ya ishu ya umeme bali lengo lake ni beyond that, likely kutaka ku - undermine integrity ya Waziri Makamba. Watu wa namna hii huwa hawakubali wala kuridhishwa na jibu lolote unless nia yako imetimia. That's how Msukuma is...!

Mimi nadhani Msukuma angemuuliza tu waziri kuwa, kama siyo tatizo lake basi litakuwa tatizo la nani, then from there kama watu wwnye nia ya kuifikia suluhu wajadiliane na kuokoa wananchi na adha hii...?

By the way, kwani ni lini ishu ya umeme wa Tanzania iliwahi kuwa reliable & stable...?

Tatizo la umeme Tanzania ni ni sugu na ni la tangu Uhuru mpaka kesho. Siku zote CCM na serikali yao wamekuwa na short term solutions.

Magufuli hakuwahi kutatua kero ya umeme. Ni utamaduni uleule wa kutafuta suluhusho dogo na la muda mfupi...

And to be honest kabisa, Tatizo la umeme wa Tanzania siyo waziri January Makamba...

Tatizo la umeme wa Tanzania ni CCM na sera zake kuhusu nishati ya umeme kwa ujumla wake akiwemo yeye Kasheku Msukuma, Makamba, Samia na wengine wote...

Ni kuwa, CCM haiwezi kuleta suluhu ya umeme hapa Tanzania. Hawa walishashindwa, hawana mapya. Ni wanafiki na waongo tu...!

Suluhu ni CCM na Sera zake mbovu za nishati ya umeme kuondoka ama kufa kabisa ili kupisha watu wapya wenye mawazo mapya, mipango mipya na sera mpya zenye uelekeo mpya...!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…