Wewe unataka kumtetea Makamba inaonekana.
Ni nani anafurahia utendaji wa Makamba? Utendaji ni kukata umeme kwa visingizio lukuki? Walisema maji, Mungu si Athumani, akaleta mvua. Sasa ndio wakaja na visingizio vya maintanance.
Anataka apewe miaka 4 kama vile ndio tumepata uhuru? Kwanini anataka kukata connection ya regime hii na nyingine?
Serikali haikatiki.
Halafu anadhani kila mtu anapenda madaraka kama yeye. Akiulizwa wajibu wake, anakimbilia kwenye madaraka.
Awajibu. Hakuna wa kudumu kwenye siasa.
Hakuna mwenye hati miliki ya uongozi. Uongozi ni dhamana.
Labda hujaelewa majibu ya Makamba...
Hoja yako na ya Msukuma ni kuhusu kukatikakatika kwa umeme...
Majibu ya Makamba ni kuwa, kama mashambulizi hayo yote ni kwa sababu ya kukatikatika kwa umeme, HILO SIYO TATIZO LAKE...
Binafsi nayaita "mashambulizi" kwa sababu, ukimsikiliza mbunge Msukuma vyema, utatambua mara moja kuwa haulizi kwa nia ya kutaka suluhu ya ishu ya umeme bali lengo lake ni beyond that, likely kutaka ku - undermine integrity ya Waziri Makamba. Watu wa namna hii huwa hawakubali wala kuridhishwa na jibu lolote unless nia yako imetimia. That's how Msukuma is...!
Mimi nadhani Msukuma angemuuliza tu waziri kuwa, kama siyo tatizo lake basi litakuwa tatizo la nani, then from there kama watu wwnye nia ya kuifikia suluhu wajadiliane na kuokoa wananchi na adha hii...?
By the way, kwani ni lini ishu ya umeme wa Tanzania iliwahi kuwa reliable & stable...?
Tatizo la umeme Tanzania ni ni sugu na ni la tangu Uhuru mpaka kesho. Siku zote CCM na serikali yao wamekuwa na short term solutions.
Magufuli hakuwahi kutatua kero ya umeme. Ni utamaduni uleule wa kutafuta suluhusho dogo na la muda mfupi...
And to be honest kabisa, Tatizo la umeme wa Tanzania siyo waziri January Makamba...
Tatizo la umeme wa Tanzania ni CCM na sera zake kuhusu nishati ya umeme kwa ujumla wake akiwemo yeye Kasheku Msukuma, Makamba, Samia na wengine wote...
Ni kuwa, CCM haiwezi kuleta suluhu ya umeme hapa Tanzania. Hawa walishashindwa, hawana mapya. Ni wanafiki na waongo tu...!
Suluhu ni CCM na Sera zake mbovu za nishati ya umeme kuondoka ama kufa kabisa ili kupisha watu wapya wenye mawazo mapya, mipango mipya na sera mpya zenye uelekeo mpya...!!